Dkt. John Pombe Magufuli akikubali tu, niko tayari kumpokea kijiti hicho 2025

Kabende Msakila

JF-Expert Member
Oct 7, 2020
1,382
1,246
JF members, and Tanzanians!

Dkt John Pombe Magufuli amefanya mengi mazuri kwa taifa letu la Tanzania - ni ngumu kutaja kwa jina kila alichofanya lakini kwa uchache - elimu, afya, barabara na vivuko, uwajibikaji, makusanyo na kodi, matumizi ya fedha za umma na kukomesha Ufisadi ni miongoni mwa vita aliyoshinda nchini.

Vita ambayo bado ni ngumu kutokana na ongezeko la idadi ya watu ni pamoja AJIRA kwa vijana, mkakati wa kuwainua WAKULIMA, habari na vyombo vya habari, uwiano mkubwa wa mishahara ya watumishi wa Umma, kukawizwa kwa pensheni za wastaafu, na Katiba ya Warioba.

SASA
Dkt John Pombe Magufuli akiridhia nimpokee kijiti cha urais baada ya muda wake kufikia mwisho kikatiba basi maeneo niliyotaja hapo juu nitayapa kipaumbele bila kusahau core "muungano wetu na kulinda maslahi ya watangulizi wangu ambao ni Dkt John Pombe Magufuli, Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, Mzee Ally Hassan Mwinyi, na familia ya mwasisi wa taifa Mwl Nyerere".

Kwa kuwa kuisha kwa uchaguzi mmoja ndiyo mwanzo wa uchaguzi mwingine basi nasubiri kipenga kipulizwe ili nipokee kijiti hicho kwa mwaka 2025 - 2030.

Siwachoshi niwasilishe
Mungu ibariki Tanzania
Mungu mbariki Rais Magufuli!

Msakila M Kabende
Kigoma
11/01

***********
Hongera sana Dkt John Pombe Magufuli - ukiwa bukoba jana umelihakikishia taifa kwamba hutawania nafasi hiyo tena 2025. Endelea kutafakali ikikupendeza nikupokee kijiti hicho 2025 - 2030. Nitaendeleza mema yote uliyoanzisha na nitaboresha mahali penye udhaifu.

******************
Huyu mbunge anayetaka Rais kuongezewa muda natofautiana naye - JPM asikubali, watu wa kuongoza wapo wengi

xxxxxxxxxxxxx
Dkt John Pombe Joseph Magufuli, tuletee Katibu Mkuu wa CCM mwenye uwezo wa kiakili, mbunifu na mzalendo. CCM kipindi alipoletwa Wilson Mkama tulibaridika sana - CCM kipindi alipoletwa Cpt John Chiligati kuwa Mwenezi tuliyumba sana pia

Tutafutie kijana, tutafutie mzalendo kama wewe - tuletee mtu asiyependwa na CDM, ACT, CUF, ili nchi hii tuendelee kuitawala.
01 Machi, 2021
 
Hii nchi ilibidi iongozwe na watu ambao wamefsnya mambo ya pekee kwa jamii, mtu Kama Bakheresa,Charles Kimei, Tundu Lisu, January Makamba, kuliko kuwapa watu wanaotaka kutajirika kupitia migongo ya Watz.
 
Anyway kama una milioni moja ya kununua ile fomu yao ndoto yako inaweza kutimia.
 
Vita ambayo bado ni ngumu kutokana na ongezeko la idadi ya watu ni pamoja AJIRA kwa vijana, mkakati wa kuwainua WAKULIMA, habari na vyombo vya habari, uwiano mkubwa wa mishahara ya watumishi wa Umma, kukawizwa kwa pensheni za wastaafu, na Katiba ya Warioba.
Umeandika ujinga mtupu.

Hakuna hata kimoja cha kuongeza pato la taifa au la serikali.

Kichwa chako kimeajaa matumizi tu ya serikali na vitu visivyoingizia hata Mia serikali.
 
Wewe ndiye yule kulima aliyechukua fomu 2015? Hongera kwa ujasiri ulioonesha mwaka huo! Ila hapa umeshafeli mkuu ina maana familia ya Mkapa yenyewe hutailinda?
 
Peleka siasa zako za Kenya huko! akikubali kwani idhini yake ndo kura za Watanzania wote!?
Kwani Kenya wana siasa gani tofauti na Tanzania? Wakati Mwl Nyerere anang'atuka alimsimamia Mwinyi (ikawa), kipindi Mwinyi amemaliza muhula wake alimsimamia Ben Mkapa (ikawa), imeendelea hivyo mpaka wakati Dkt John Magufuli anasimama watangulizi wake walimwamini na leo (imekuwa).

Sasa ukenya unatoka wapi? Dkt Magufuli ni wa kanda ya ziwa mimi niko kanda ya magharibi, Dkt Magufuli ni msukuma mimi ni muha, - hapa hakuna hoja ya kufananishwa na wakenya ambao ukabila umewatawala

Tanzania hilo halipo
 
🤣🤣🤣🤣🤣

Mnaifanya siasa kuwa nyepesi namna hiyo eeee?!!!

Yaani CCM yenye wanachama milioni 12....upewe wewe nafasi ya upendeleo kwa KUJINADI MWENYEWE TU ha ha ha ha ha duuuh......

Nilitegemea muda ukifika uchukue fomu na kuomba kuteuliwa Urais km wenzako wengine.....sikujua utakuja KIENYEJI NA KITOTO namna hiyo loooooh kweli MAGUFULI amefanya URAIS uonekane RAHISI....

Hongera kwake JPM na CCM ya awamu ya 5!!!
 
🤣🤣🤣🤣🤣

Mnaifanya siasa kuwa nyepesi namna hiyo eeee?!!!

Yaani CCM yenye wanachama milioni 12....upewe wewe nafasi ya upendeleo kwa KUJINADI MWENYEWE TU ha ha ha ha ha duuuh......

Nilitegemea muda ukifika uchukue fomu na kuomba kuteuliwa Urais km wenzako wengine.....sikujua utakuja KIENYEJI NA KITOTO namna hiyo loooooh kweli MAGUFULI amefanya URAIS uonekane RAHISI....

Hongera kwake JPM na CCM ya awamu ya 5!!!
Nachotamani ni kuwa kiongozi si mtawala wala boss - mamlaka ya kiuongozi yanatolewa na Katiba
 
Back
Top Bottom