msovero
JF-Expert Member
- Jun 30, 2019
- 839
- 1,472
Mama naomba niandike kifupi ili nisikuchoshe kusoma maana najua una majukumu mengi na mazito ya kuwatumikia Watanzania.
Mama, wakati hayati magufuli hajakumbwa na mauti alituahidi ajira 13529 za ualimu. Kati ya hizo ni ajira 8000 tu zimetolewa katika awamu ya kwanza nazo zilitolewa angali bado yu hai.
Leo hii hatuko naye lakini bado kuna kiporo cha ajira zaidi ya elfu 5000 zilizosalia bado hazijatoka na hatma haieleweki kama nazo zimekufa au laah!
Najua wewe ni mama mwenye huruma na upendo, hivyo naomba kukufikishia kilio hiki ukipatie suluhu maana miezi inaenda na matumaini yanazidi kupungua.
Mwisho, tuna imani na wewe mama tunaamini hautatuangusha. Kadhalika tunakutakia kila la heri katika majukumu yako mapya.