Dkt. Jakaya Kikwete kuwa mwenyekiti wa Bodi ya GPE ni fursa kwa Tanzaina; Wizara ya Elimu Changamkeni, Ndalichako usisale

Ngungenge

JF-Expert Member
Jun 11, 2016
2,862
3,190
Mh. Rais Mstaafu Dr Jakaya kikwete kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa bodi ya Global Partnership for Education ni mafanikio makubwa kwa sekta ya elimu ya Tanzania.

Global Partnership for Education ni moja ya taasisi kubwa inayofadhiri miradi ya elimu duniani.

Nchi yetu imekuwa ikifanya jitihada mbalimbali za kuhakikisha sekta ya elimu inaimarika.

Kama hivi sasa Mh. Rais Samia amepambana kuhakikisha kila jimbo linapata fedha za ujenzi wa shule ili kila mtoto wa Tanzania apate elimu bora.

Sasa ni wakati wa wataalamu wa wizara kutazama fursa za kupata misaada kutoka shirika hili kubwa.

Napenda kutoa rai kwa wizara ya elimu na wadau wa elimu wasibweteke, huu ni wakati wa kutumia ushawishi wa Mh. Dr. Jakaya Kikwete kupata misaada mahususi na kuhakikisha sekta ya elimua inakuwa.

Ushauri wa Maeneo yanayotakiwa kuangaliwa ni pamoja na

1. Kuboresha miundombinu ya elimu mkianza na shule za muda mrefu na shule zenye wanafunzi wengi kupita uwezo wao.

2. Kuangalia namna gani mtasaidia vijana wenye taaluma ya ualimu kuajiriwa katika mfumo wa kudumu au wa muda mfupi.

3. kusaidia upatikanaji wa vifaa vya kujifunzia hasa kuelekea elimu kidigitali ili kujenga vijana wenye ushawishi.

4. Kujengea uwezo wataalamu wa elimu

Jengeeni uwezo wataalamu wenu ili waweze kutafuta fursa za kidunia kuinua elimu.

Tumshukuru Mungu kwa kumuweka hai Mh. Rais Mstaafu Dr. Jakaya Kikwete.

Kumbukeni msipochangamkia fursa hizo, nchi nyingine zitaomba na hatimaye fedha zitaenda kwao hasa kenya na uganda.

Tunahitaji kuchangamkia fursa.

RAIS SAMIA
#KAZI IENDELEE
 
Kwenye mapendekezo yako hujaweka kubadili mitaala ya elimu. Wakati nchi zilizoendelea zinafundisha namna ya kuweka alam kwenye saa ya ukutani, mitaala yetu inakwambia uchore saa ikionyesha saa sita kamili mchana. Au wanafundisha wajibu wa waziri wa nishati ni upi, sisi tunafundisha kutaja jina la waziri.
 
Naunga Mkono hoja Wizara wachukue mapendekezo haya
 
watu ndio kwanza wanapata ulaji hakuna atakekumbuka hayo yote hata kidogo
kimsingi miradi inamifumo ya usimamizi na udhibiti kikubwa tupate hela kwanza halafu tutajua tutabanana vipi kuhakikisha vinafanya malengo yaliyokusudiwa
 
Na bado atapanda sana Mkwere yule! si mnmsema alikuwa anakula kona tuuu!! sasa nasema hivi na Mbinguni mtamkuta akipiga Story na sir God! wenye roho mbaya watarudi waliko toka wakijua wamekosea kuuumbe ndo Mungu mwenyewe yule!!

hawatakaa warudie tena kwenda safari ile ni mara moja tuuuu! anapewa mtu! tnamuombea Rais wetu bora aliyewahi kutokea Tanzania hii!! tembeeni kifua mbele kikwete ni Mtu!
 
Mh. Rais Mstaafu Dr Jakaya kikwete kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa bodi ya Global Partnership for Education ni mafanikio makubwa kwa sekta ya elimu ya Tanzania.
Global Partnership for Education ni moja ya taasisi kubwa inayofadhiri miradi ya elimu duniani.
Nchi yetu imekuwa ikifanya jitihada mbalimbali za kuhakikisha sekta ya elimu inaimarika.
Kama hivi sasa Mh. Rasi Samia amepambana kuhakikisha kila jimbo linapata fedha za ujenzi wa shule ili kila mtoto wa Tanzania apate elimu bora.
Sasa ni wakati wa wataalamu wa wizara kutazama fursa za kupata misaada kutoka shirika hili kubwa.

Napenda kutoa rai kwa wizara ya elimu na wadau wa elimu wasibweteke, huu ni wakati wa kutumia ushawishi wa Mh. Dr. Jakaya kikwete kupata misaada mahususi na kuhakikisha sekta ya elimua inakuwa.
Ushauri wa Maeneo yanayotakiwa kuangaliwa ni pamoja na
1. Kuboresha miundombinu ya elimu mkianza na shule za muda mrefu na shule zenye wanafunzi wengi kupita uwezo wao.
2. kuangalia namna gani mtasaidia vijana wenye taaluma ya ualimu kuajiriwa katika mfumo wa kudumu au wa muda mfupi.
3. kusaidia upatikanaji wa vifaa vya kujifunzia hasa kuelekea elimu kidigitali ili kujenga vijana wenye ushawishi.
4. Kujengea uwezo wataalamu wa elimu

Jengeeni uwezo wataalamu wenu ili waweze kutafuta fursa za kidunia kuinua elimu.
Tumshukuru Mungu kwa kumuweka hai Mh. Rais Mstaafu Dr. Jakaya Kikwete.

Kumbukeni msipochangamkia fursa hizo, nchi nyingine zitaomba na hatimaye fedha zitaenda kwao hasa kenya na uganda.
Tunahitaji kuchangamkia fursa.

RAIS SAMIA
#KAZI IENDELEE

Alikuwa rais akashindwa kuleta hiyo fursa na kubadili elimu yetu, ndio ataleta fursa sasa akiwa huko uchochoroni?
 
Kwenye kumtambulisha toa Hiyo Dr sio Dr yeye.
Kwa kuwa PhD ya heshima haitumiki kwenye utambulisho.
Na huwezi kusikia Dr Julius Kambarage Nyerere au Dr Mkapa na wote Wana PhD za heshima ila walikua wanajua hazitumiki kumtambulisha muhusika Kwa kuwa ni za heshima.
 
Back
Top Bottom