Dkt. Jakaya Kikwete amtunuku Rais Samia Shahada ya Udaktari wa Heshima UDSM. Sasa ni Dkt. Samia

Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
1,441
7,780
1669811717179.png

Rais Samia amekabidhiwa shahada ya udaktari wa heshima kutoka chuo kikuu cha Dar es Salaam leo wakati wa mahafali ya 52 duru ya 5. UDSM imesema uongozi wa Rais Samia umeleta mageuzi ya kiuchumi na mengineyo, pia umeleta tumaini jipya.

Rais Samia amesemwa kuboresha elimu ikiwemo kujenga vyuo 25, kusaini na benki ya dunia mradi wenye thamani ya bililioni zaidi ya 900 wenye lengo la kuboresha elimu ya juu.

Rais Samia amemshukuru Dkt. Kikwete na baraza la seneti la chuo kikuu cha Dar es Salaam kwa kumpendekeza kupata tuzo hiyo na aliikubali kwa sababu siyo ya kwake pekee bali watanzania.

Rais Samia alisema alijaribu kutafuta shahada hiyo lakini muda haukumpa nafasi

Pia, soma=> Chuo kikuu Cha Dar es salaam kimpe Rais Samia Udaktari wa Heshima katika uongozi na mahusiano ya kimataifa
 
Aliyeidhinisha kutoka Senate ni Kikwete, mkuu wa chuo, ambae nae alipewa hivyo hivyo pale Udom na Mkapa.

Sababu zikitajwa kua
1. Mchango mkubwa kwenye elimu
2. Kutatua changamoto kubwa kwenye jamii.

Sababu ya tatu sijaisikia vizuri lakini tujadili haya yenye kustahili hii doctorate

Umeme, maji, TOZO, uchumi kushuka, ile hotel mbovu ya dodoma imegharimu bil. 9.7 na sasahivi inakarabatiwa kwa fungu jingine, daraja la juzi bil. 7.2, mfumuko wa bei kwenye kila kitu. Hayo ni kwa uchache tuu.

#Honorary causa
Nina kuku wa kuchi pale nyumbani, kwa spidi hii, havuki Christmas #Honorary causa inamhusu. Dr. Kuchi
View attachment 2431733
 
Hivi videgree vya heshima siku hizi havina hata mvuto , uzuri Ni kwamba havina mvuto wowote kwa watanzania

Kipindi Cha nyerere ukisikia mtu kapewa kila mtu anafatilia sio Tanzania hata afrika mzima inajiuliza huyu Ni Nani? Kwa Nini kapewa? Kafanya Nini? Yaani ilikuw bonge la heshima

Ila kipindi Cha kikwete , magufuri na Sasa watu wanaona hamna kitu, Ni udaktari wa heshima wa ccm tu, kusifu na kuabudu

CCM wameharibu Sana elimu yetu
 
Back
Top Bottom