Nyendo
JF-Expert Member
- Jun 4, 2017
- 1,190
- 4,103
Dkt. Hussein Mwinyi yupo LIVE anajibu maswali ya moja kwa moja kutoka kwa wananchi.
Barabara na uchumi mkubwa
Amesema Swala la barabara Unguja na Pemba ni swala muhimu na pia wanapozungumzia uchumi mpya ina maana watahitaji umeme mwingi zaidi na wanatafuta njia ya kuweza kuwa na uchumi mkubwa zaidi na kwa kuwa na umeme mkubwa na wa uhakika .
Utalii
Amesema bado wana fursa kubwa ya kuongeza utalii mwingine kama utalii wa historua katika maeneo ya kale, utalii wa fukwe za baharini na kuhakikisha utalii unakuwa wa aina yake yaani unakuwa utalii wenye tija kubwa.
Ajira
Amesema watazalisha ajira laki tatu kutoka kwenye uchumi mpya wanaotaka kuujenga kutoka kwenye uvuvi, barabara, viwanda, mafuta na gesi hivyo ni imani yake ajira zitapatikana na huduma za jamii zitaboreshwa kama umeme na maji na huko kote ajira zitazalishwa.
Diaspora
Amesema ili uchumi uweze kukua ni lazima sekta binafsi zishiriki hivyo hata hao watanzania wanaoishi nnje watashirikiana nao a yeye anaahidi iwapo atakuwa Rais wa awamu ya nane basi atawatumia hao maana ni sekta muhimu.
Ardhi ya kilimo
Amesema Zanzibar hawana ardhi kubwa ya kilimo lakini wana zao lenye thamani kubwa zao la karafuu na wana mazao ya viungo ambayo yanasoko kubwa hivyo watayatumia hayo kukuza uchumi na pia amedI muda umefika wa kujenga viwanda ili kuliongezea thamani zao hilo kuliko kuliuza likiwa zao ghafi.
Swala la maendeleo ya kisiwa cha Pemba
Amesema lengo ni kuhakikisha na Pemba inapiga hatua na serikali ya awamu ya nane wataweka juhudi za makusudi ili na Pemba ipige hatua za maendeleo kama Unguja.
Ajira kwa vijana
Amesema kuhusu swala la kuwakomboa vijana na ukosefu wa ajira amedai kuwa ataborsha mfuko kwa ajiri ya kuwawezesha vijana kujiajiri na atatoa mafunzo kwa vijana ili wawweze kukidhi vigezo vya kuweza kuajiriwa.