Zanzibar 2020 Dkt. Hussein Mwinyi afika Ofisi za ZEC na kuchukua fomu za kuteuliwa kugombea Urais

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Hussein Mwinyi amefika Ofisi za Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) na kuchukua fomu za kuteuliwa kugombea Urais wa Zanzibar

Wagombea wanatakiwa kurejesha fomu za uteuzi Septemba 09, 2020 kabla ya saa 10 jioni. Tume ya Uchaguzi visiwani humo itafanya uteuzi wa wagombea Septemba 10
 
NIMEONA KUMBE WANAANZA LEO?
Maneno ya ZEC haya:-

''The candidates for the presidency, representation and councillorship will have between August 26 and September 9, 2020 to pick and return the candidature nomination forms prior to the nomination day on September 10. ''
 
Haya ndiyo ya Husein Mwinyi aliyosema leo katika Ilani yake.

Umoja.
-Kuondoa Matabaka.
-Upemba na Uuunguja.
-Ukusini na Ukaskazini.
-Udini.
-Na maeneo mengine.
Uchumi
-Zanzibar ya viwanda.
-Utalii wa kisasa.
-Bandari ya kisasa.
-Uvuvi wa Bahari kuu wa kisasa.
Jiandaaeni kwa ajira makhsusi kwa wazanzibari tuuu kwanza kabla ya wengine.

Hivyo ni vipa umbele vyake Mh.Mwinyi Makamo wa Kwanza wa Raisi mtarajiwa wa CCM Zanzibar.

Kwa muktadha huu sijaona kwa nini waliopita walishindwa kuyafanya haya?
Jibu ni Rahisi tuu,
Mfumo wa Muungano ndio shida.
Dr.Shein litaka kuchimba Mafuta, Kujenga Bandari Kubwa, na kufanya Uvuvi wa Bahari kuu yote Bara wamemkatalia na Kumblock.
Hivi yeye atawezeje?
Ili aweze kuyafanya hayo ni lazima Akubali Kuwa Mkuu wa Mkoa wa kanda ya Zanzibar na hayo yawe chini ya Jamuhuri ya Muungano.
Kwa hili Hatudanganyi.
Tunamtaka Simba Wa Nyika alete mabadiliko ya Mfumo wa Muungano.
 
Huyu mwepesi kwa maalim (shikamoo) ameisha wajipa kupiga mabomu kama mwaka 2000, 2010 &2015
 
Back
Top Bottom