Dkt. Hellen Kijo: Watanzania hawajawa tayari na maandamano

jitombashisho

JF-Expert Member
Jun 11, 2020
667
2,242
Akihojiwa na Idhaa ya Kiswahili ya Ujerumani mwanaharakati wa siku nyingi wa haki za binadamu ndugu Daktari Hellen amesema Watanzania wengi bado hawapendelei kuitumia haki yao ya kuandamana kudai jambo lolote lihusulo haki zao.

"Iwe hata maandamano ya kuhamasishwa Watanzania wengi bado hawaoni umuhimu wake kwa sababu hawajaguswa nalo na ndiyo maana maandamano mengi hayafanikiwi hapa Tanzania.

"Mfano, kukamatwa kwa viongozi wa upinzani Tanzania, hiyo pekee ilitosha wafuasi wao kuingia barabarani na kudai haki ya wao kuachiliwa pia na kuendelea kudai madai yao kusikilizwa, cha ajabu hata pamoja na hilo, Watanzania bado wapo usingizini na inasikitisha mno," alisema Dkt Hellen.
 
Tarehe 2 imefika nimeamka vizuri kabisa nimejipanga nazama zangu Ubungo kimya, kila mtu yuko busy na mishe zake.
Anyway December inakaribia niruke zangu pipa nitarudi 2025 jiwe akiondoka, kama bado yupo tutapiga kura nitaondoka tena hadi 2030 kama bado mzima. Ngoja tusubiri ni lini watanzania wataamka maana kweli wamelala mno
 
Tunaandamana moyoni. Tumelelewa kinafki ,vitisho na serikali ya CCM.
 
Siungi mkono Dhurma inayofanywa na Serikali ya Magufuli, siungi mkono pia unafiki wa hao viongozi wetu wa upinzani wao tayari wapo nnjee saizi na familia zao vipi kuhusu hao Mama zangu sijui hata km chama kimewawekea mwanasheria Kaka yangu Mdude sijui yupo kwenye hali Gani zaidi Gerezani...
IMG_20201104_103554.jpg
 
Natumai mkuu leo atatoa agizo kufutwa kesi na mashauri ya kisiasa watu wachape kazi.
 
"Ujinga" ni janga kubwa sana ndio maana bado watanzania wanadanganywa na kuwachagua viongozi ambao wanahubiri maendeleo wakidhani kama kufanya maendeleo ni hisani ya viongozi.
Kiongozi akifanya jambo la maendeleo anataka asifiwe na kuabudiwa kama vile kafanya kwa hela yake ya mfukoni mwake na kuwaona watanzania hawakustahili kufanyiwa hayo yote isipokuwa kwa huruma zake tu.

Hapana ifike wakati tujitambue watanzania, hii nchi ni yetu na hawa viongozi tunatakiwa kuwaweka sisi watutumikie na maendeleo ni haki yetu wala sio hisani yao anayeshindwa kufanya kazi tuliyompatia aondolewe na kuwajibishwa juu yake.

Watanzania wengi hawazijui haki zao ndio maana hata kuzidai hawawezi. Kama mtu hata kwenda kupiga kura hajui maana yake atawezaje kudai haki ya kuchagua kiongozi amtakae? Hii nchi bado sana mama Kijo, wewe uko sawa sana. Hawa watawala wetu wanawanyima watanzania haki ya kupata elimu bora ili ujinga uendelee kutamalaki kwenye maisha yao nao watawala waendelee kutawala kupitia ujinga wa watanzania.
 
Kigenge chao waliratibu Mgomo wa Madaktari 2011 baada ya Mgombea wao wa Urais kushindwa 2010,

Baada ya mgomo kupamba moto Muhimbili akatumia hiyo fursa kuhamasisha maandamano kuanzia pale palm beach kwenda Ikulu kumtoa Mamlakani Rais Kikwete, bahati nzuri Watanzania walivyo waerevu walimpuuza kama walivyopuuza Maandamano ya kina Mbowe na Zitto kulilia 'ubunge' wao!
 
Kama anasikitika na sisi tuko usingizini mbona na yeye mwerevu hajaenda huko kuandamana kama anavyohubiri! Huyu mama zero brain.
 
Hizi ni comments za watu wanaodhani yanayowakuta wengine kamwe wao na ndugu zao hayawezi kuwakuta kwa sababu tu wanapiga makofi kuunga mkono udhalimu?!

Btw, huko kwenu na wenyewe mnatumia VPN kama hao wengine au mkigusa tu, shaaaaaa; net yenyewe inachagua na kuona huyu ni Msukule wa Lumumba kwahiyo haitajiki kutumia VPN, au na wenyewe bado mnahangaika kama wale wengine?!
Man, I do not support this Government kwenye suala la uhuru. But Lissu, a western puppet,defender of acacia with all de threat, nuthn happened, chadema that unstable political party. Those if they are elected to lead us, we are fucked up big time.
Bora shetani nilijualo.
 
Back
Top Bottom