Dkt. Hassan Abbas: Wasemaji wa vilabu msiropoke na acheni porojo, zingatieni maadili

craq

JF-Expert Member
Mar 22, 2017
835
1,000
"Wasemaji ninaowaongoza, wazingatie kuna maadili ya kuwa Msemaji kama vile taaluma ya habari ambayo inatuongoza, tumeshatoa mafunzo kwa Wasemaji wa Vilabu vya Mpira, tumeona kuna changamoto kweli wakati mwingine badala ya kuhamasiha Watu kwenda viwanjani unakuta Msemaji anahamasisha vurugu, Msemaji anasema Watu fulani wasije uwanjani ukija tutakutoa”- Dk. Hassan Abbas, Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali

“Wasemaji wafahamu usemaji sio kuropoka, usemaji una maadili yake kwahiyo tumeshatoa mafunzo kwa Wasemaji wa Vilabu vyote vya michezo mbalimbali, huku tunakokwenda tunataka kuona mabadiliko kwahiyo ni muhimu kwa Viongozi na Vyama vya Michezo kuhakikisha Wasemaji wao sio waropokaji isipokuwa ni Watu wanatimiza wajibu wa kitaaluma na kikatiba lakini sio porojo na uropokaji"-Dr.Abbas
 

Loftins

JF-Expert Member
Oct 1, 2017
8,546
2,000
Ulaya msemaji ni kocha mkuu.

Yeye ndiye anajua kila kitu kuhusu timu hivyo ni mtu sahihi zaidi kuulizwa na kutoa update.

Bongo sasa...
Pole sana huenda wewe ni mtizamaji tu wa mipira ya ulaya na wala sio mfuatiliaji!

Timu zote unazozijua za ulaya zina wasemaji wake na baadhi kama si zote zina waandishi wao, tv zao pamoja na radio zao.
Taja timu yoyote unayohisi haina msemaji nikutajie jina lake
 

Castr

JF-Expert Member
Apr 5, 2014
21,805
2,000
Pole sana huenda wewe ni mtizamaji tu wa mipira ya ulaya na wala sio mfuatiliaji!

Timu zote unazozijua za ulaya zina wasemaji wake na baadhi kama si zote zina waandishi wao, tv zao pamoja na radio zao.
Taja timu yoyote unayohisi haina msemaji nikutajie jina lake
Taja msemaji wa timu yoyote ya uingereza anayeelezea mbinu, matarajio ya timu ya msimu, majeruhi na uwezo wa wachezaji.
 

Loftins

JF-Expert Member
Oct 1, 2017
8,546
2,000
Taja msemaji wa timu yoyote ya uingereza anayeelezea mbinu, matarajio ya timu ya msimu, majeruhi na uwezo wa wachezaji.
Shida yako ni ndogo wewe ni mpenzi mtazamaji tu.

Kubishana na wewe itakuwa ni kujipa kazi isiyo na maslahi yoyote.

man.jpg

structure ya manchester united kwenye issue za tech.

pole sana aisee mpira ni zaidi ya uujuavyo
 

Castr

JF-Expert Member
Apr 5, 2014
21,805
2,000
Shida yako ni ndogo wewe ni mpenzi mtazamaji tu.
kubishana na wewe itakuwa ni kujipa kazi isiyo na maslahi yoyote.
View attachment 1720905
structure ya manchester united kwenye issue za tech.

pole sana aisee mpira ni zaidi ya uujuavyo
Timu za nje zina msemaji kwa ajili ya ishu kama mapato, faida, madeni, hasara na vitu kama hivyo.

Ishu za timu na wachezaji hua zinamalizwa na kocha. Kwakua umesema haipo hivyo mtaje msemaji yeyote anayeongelea maswala ya timu na wachezaji huko Ulaya.
 

kibaravumba

JF-Expert Member
Dec 21, 2012
6,246
2,000
Kumbe ukiwa utopolo hata usome vipi hutojificha.

Nawaona humu utopolo mnavyokimbzwa na mafanikio ya Simba.Yaani chuki na husda zenu dhidi ya Simba mnataka kuzionesha mkijifichia kwa msemaji wa Simba?Kwani wasemaji wengine hamuwaoni?Hamkumbuki msemaji mamluki mmoja aliwahi kusema Morrison ni mchezaji wa utopolo?Au uzushi wake kuwa Morrison amegombana na coach?

Msemaji wa serikali ni msomi sidhani kama alikuwa anamsema Haji kwa mafumbo,bali alisema tu kwa ujumla ili kuzuia usemaji usio fuata misingi ya maadili ya uanahabari.Mfano mtu anasema waamuzi wanashirikiana na TFF na serikali kuikandamiza timu fulani ili timu nyingine ifanikiwe bila ushahidi wowote.Huu ndio uropokani.

Sidhani pia msemaji wa serikali hajui utani uliopo kati ya watani wa jadi hadi apoteze muda kuzungumzia utani huo kama vitu serious sana.Ninachoona ni tafsiri yenu tu wanautopolo kwa kuwa mnaumizwa sana na mafanikio ya Simba.
Mlitaka Simba ishinde international matches wakiwa wanyong'onyevuu.Acheni wivu,husda na chuki dhidi ya mafanikio ya Simba.Kinachowatesa sio kauli ya Haji Manara,bali ni mafanikio ya Simba.
 

Mbeya City Spurs I

JF-Expert Member
Jan 6, 2021
488
1,000
Taja msemaji wa timu yoyote ya uingereza anayeelezea mbinu, matarajio ya timu ya msimu, majeruhi na uwezo wa wachezaji.
Bongo msemaji wa klabu anazungumzia mpaka mbinu zitakazotumika mchezoni. Anakwambia kabisa tutacheza mpira wa pasi. Anazungumzia pia majeruhi na hali za wachezaji. Hizo zote msemaji wake apaswa kuwa kocha.

Ndiyo kwa mfumo wetu tunahitaji wasemaji kama akina Manara na Nugaz au Masau Bwire ili wazungumzie masuala ya nje ya kikosi/uwanja; ticketing, usafiri, nk ambayo kwa wenzetu ulaya huwekwa kwenye media outlets zao. Sisi bado hizo outlets hazijawa common kiasi cha kutohitaji wazungumzaji.

Ila wazungumzaji na klabu zao wawe professional, waache ubabaishaji.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom