Dkt. Hassan Abbas usipambane na Kikwete siyo saizi yako. Acha kupotosha umma kwa njaa zako

Tabutupu

JF-Expert Member
Nov 26, 2010
13,107
18,322
Nimeona umepost video nyingine kwa kutumia ukurasa wa “Msemaji wa Serikali” ukidai katika Mpango wa Maendeleo wa Taifa 2025 (National Development Vision 2025) ambao ulisainiwa na kuanza kutumika kipindi cha Mkapa hakuna sehemu inataja tunahitaji kufikia kipato cha kila mtu cha USD 3,000.

Kila mtanzania anajua unajibidisha kumjibu Rais Kikwete baada ya kuweka sawa Mpango wa Maendeleo wa Taifa ambao ofisi yako ya Msemaji wa Serikali mlishaanza kudanganya umma kwamba tumefikia kabla ya wakati.

Naomba nikukumbushe yafuatayo:-

1. Katika Mpango wa miaka mitano wa mwaka 2016 ambao ni subset ya mpango wa 2025 ambao huwekwa kila baada ya miaka mitano, bosi wako Rais Dkt John Magufuli katika utangulizi anataja USD 3,000 kama kipato tunachotakiwa kufikia ifikapo 2025. Kwa namna moja unapingana na bosi wako na kumtia aibu na kufanya wananchi tuamini kwamba ndio anakutuma uongee huu utumbo wa darasa la kwanza.

1596173324055.png

2. Pia Kikwete amekuwa Rais wa Tanzania kwa miaka 10, na katika miaka hiyo 10 Mapango huu wa maendeleo alikuwa ndio akiamka nao na kulala nao maana utekelezaji wake wote ulikuwa kwenye mpango huu. Ameutekeleza Mpango huu wa Maendeleo kwa miaka 10, Kikwete hajakurupuka na sio mtu wa kukutupuka.

Kumbuka Kikwete ameshiriki kuuandaa mpango huu 2025 akiwa Waziri wa Fedha 1994 pamoja na Vision ya TRA.

Kuwa na adabu kwa wakubwa zako.

3. Sijui unasoma wapi huo udaku kwamba hakuna sehemu inaeleza kipato cha usd 3,000.

1596174472301.png
4. Watanzania wanaomba uwaombe radhi, Kazi imekushinda. Tunajua Mh. Rais Dkt John Pombe Magufuli hajakutuma ila unajaribu kujipendekeza kulinda kibarua chako wakati Mh. Rais Dkt. John Pombe Magufuli anajua nini maana ya Mpango wa Maendeleo 2025.

Dr. Abbas elimu yako ni kubwa sana ila inatupa mashaka, kwa sababu kwa PhD holder usingeweza kuja na mawazo ya hali ya chini kama hivi na usijue vision 2025 inalenga nini..

HII HOTUBA YA JK MSIBANI NI MOJA YA HUTUBA BORA KWA MWAKA HUU.

Mleta mada asante sana, Kitu kimoja nilichoona kumbe Watangulizi wa mheshimiwa wa sasa walikuwa wana continuity fulani hivi kwa mfano:

1. Kwenye hilo bandiko, maandalizi ya Tanzania Development Vision kumbe yalianza mwaka 1994 wakati wa Mwinyi na Kukamilika mwaka 1999 wakati wa Mkapa

2.Kumbe mwaka 2014 tulishafikia pato la dola 1043 kwa Mtu

3. Sasa leo kufikisha dola 1080 maana yake tumeongeza dola 36 tu

4. Pia nimesoma mahali pengine kuwa sheria ya TRA ilisainiwa mwaka 1995 mwezi August wakati wa Mwinyi na TRA ikaanza june 1996 wakati wa Mkapa

Sasa haya maneno kuwa watangulizi hawakufanya kitu kikubwa kuliko rais wa sasa yanatoka wapi?
 
Nadhani pia Mwinyi anatakiwa kupewa credit , maana wengi wanamtaja mkapa lakini huu mpango umeanza kuota toka 1994 kablanya mkapa kuchukua madaraka.. the same for TRA.

Hii ni sawa na terminal 3, ubungo flyover, nyerere hydropower, tazara flyover, etc kumpa credit magufuli wakati watangulizi wake ndio wameanzisha mchakato.
Mleta mada asante sana, Kitu kimoja nilichoona kumbe Watangulizi wa mheshimiwa wa sasa walikuwa wana continuity fulani hivi kwa mfano:

1. Kwenye hilo bandiko, maanndalizi ya Tanzania Development Vision kumbe yalianza mwaka 1994 wakati wa Mwinyi na Kukamilika mwaka 1999 wakati wa Mkapa

2.Kumbe mwaka 2014 tulishafikia pato la dola 1043 kwa Mtu

3. Sasa leo kufikisha dola 1080 maana yake tumeongeza dola 36 tu

4. Pia nimesoma mahali pengine kuwa sheria ya TRA ilisainiwa mwaka 1995 mwezi August wakati wa Mwinyi na TRA ikaanza june 1996 wakati wa Mkapa

Sasa haya maneno kuwa watangulizi hawakufanya kitu kikubwa kuliko rais wa sasa yanatoka wapi?
 
Huyu Dr Abbas ni takataka kabisa. Wala msipoteze muda wa kujibishana nae.

Hivi unaanze kujibishana na Jakaya Mrisho Kikwete??? Rais mstaafu aliyeishika nchi na kuiendesha kwa miaka 10???? Wewe nani na una nini cha kumshinda kikwete hadi umjibu????

Ndugu zangu, huyu Dr Abbas tumpuuze kama wapuuzi wengine tu!
 
Abbas alikuja na mambo kumi eti ndiyo yaliyotufanya tuingie uchumi wa kati kabla ya malengo kutokana na akili yake inavyowaza ila kwakuwa namjua ni kilaza sikutaka kuumiza kichwa kumjadili.

Hili jamaa lisione tukio au agizo kutoka kwa boss wake yani linakimbilia kwenye media kama dozi ya homa kali kwenda kutoa matangazo.
 
Nadhani hajawahi kusoma mpango wa maendeleo 2025, ameusikia lupaso baada ya kikwete kuweka sawa.

Pia kikwete kasoma uchumi.. ni vyema angeheshimu na kujifunza badala ya kuanza kuleta ugoro huu..
Abbas alikuja na mambo kumi eti ndiyo yaliyotufanya tuingie uchumi wa kati kabla ya malengo kutokana na akili yake inavyowaza ila kwakuwa namjua ni kilaza sikutaka kuumiza kichwa kumjadili.

Hili jamaa lisione tukio au agizo kutoka kwa boss wake yani linakimbilia kwenye media kama dozi ya homa kali kwenda kutoa matangazo.
 
Magufuli hana neno juu ya hilo, wasaidizi wake ndio wanapotosha..

Magufuli anajua target ya 2025.
Kubali au kataa, Kikwete hakumtendea haki Magufuli!!!! Unafiki wa Kikwete utaleta matatizo mbeleni. Hayo alitakiwa kumweleza wakiwa chemba si mbele ya kadamnasi. Rules za uongozi zinakataza vitu kama hivyo na uliona JPM alivyolowa.
 
Back
Top Bottom