Dkt. Hassan Abbas usipambane na Kikwete siyo saizi yako. Acha kupotosha umma kwa njaa zako

Tuombe Mungu tusije rudi ligi ya mchangani tena..
Hiyo 3000 USD kwa 2025 ni ndoto za Alinacha. Mpaka hapo tushafail Magu kaongeza kidogo sana kwa miaka mitano. Miaka mitano ijayo hata 2500 hawezi kufika.
 
Katafute wewe PhD yako kama unaona Ni rahisi kupatikana
Hivi unaamini PHD za wabongo?? Izo PHD zao zinaleta mabadiriko gani kwa watanzania zaidi ya wao baadae kuingia kwenye siasa na kugombea vyeo vya kisiasa???

Sikiliza ndugu ukiona PHD ulaya ujue kuna tafiti kabambe imefanyika na hiyo tafiti imetumika kwenye maisha ya binadamu na kuleta matokeo Chanya kweli.

Achana na PHD za kibongo ambao wote wanaishia kuwekeza kwenye siasa, kufungua bar na pubs
 
Angalia mkapa alivyo tupaisha. Kisha mtu anaanza kujitutumua.
IMG-20200728-WA0016.jpeg
 
Kabakisha miaka mitano tu(kwanza sijui kama atashinda) , tuone kama anaweza kuvaa viatu vya BWM au JK.

Uongozi ni zaidi ya ukali na kutumbua, na kuongea kwa hisia kali

BWM hakuwa mtu wa maujiko ujiko lakini mambo aliyofanya nchi hii ni mazito!. Mifumo mingi nchini ina alama zake!
Alama kweli ameacha, zile roho za wapemba alizosimamia na kubariki vyombo vya dola viuwe, ni alama ambayo itafutika siku ya malipo mbele ya Muumba Mbingu, Dunia na vilivyo ndani yao
 
PHD holder anafungua bar
Hivi unaamini PHD za wabongo?? Izo PHD zao zinaleta mabadiriko gani kwa watanzania zaidi ya wao baadae kuingia kwenye siasa na kugombea vyeo vya kisiasa???

Sikiliza ndugu ukiona PHD ulaya ujue kuna tafiti kabambe imefanyika na hiyo tafiti imetumika kwenye maisha ya binadamu na kuleta matokeo Chanya kweli.

Achana na PHD za kibongo ambao wote wanaishia kuwekeza kwenye siasa, kufungua bar na pubs
 
Bado miaka 2025 haijafika ila kutegemea GDP kukua kutoka US dola 1043 hadi US dola 3000 ndani ya miaka 10 ni upuuzi labda tuuze nchi ndo tutafanikiwa

Mkapa alikuta pato la mtu ni dola 170 mwaka 1995 kaondoka 2005 likiwa ni dola 500, aliliongeza takriban mara mbili, yaani by around 200%

Sasa huyu kaikuta around 980, basi kwa kuwa tunaambiwa yeye ni mchapakazi hodari basi naye aiongeze mara mbili yaani

980 aliyoikuta +(980x2) =2940 ambayo ni approximately =3000

lakini so far kaongeza sh 100 tu ndani ya miaka 5, maana yake kuna uwezekano wa kuongeza 100 nyingine tu ndani ya miaka mingine mitano, hapo lengo la dola 3000 litakuwa ni ndoto tu kwa utawala huu
 
Alama kweli ameacha, zile roho za wapemba alizosimamia na kubariki vyombo vya dola viuwe, ni alama ambayo itafutika siku ya malipo mbele ya Muumba Mbingu, Dunia na vilivyo ndani yao

Siyo yeye aliyeamuru, yeye alikuwa nje ya nchi.

waulize akina Sumaye na Dr Omar Ali Juma ndo walikuwa nyumbani incharge.

Yeye anachukua responsibility kwa sababu alikuwa mkuu wa dola lakini hakuamuru watu wachapwe risasi
 
Nadhani hata Dr abbas atakua na bar yake somewhere, anacho kosea ni kupita bar kabla ya kwenda ofisi ndio matokeo haya tunayo yaona
Hata mie nawaza ivo. Tanzania hakuna PHD Kuna wahuni tu wanaotaka kutunisha CV zao kwa kuwa na degree tatu.

Niamini mimi Tanzania hakuna PHD ,PHD ziko ulaya, Marekani na Asia huko. Huku tuna wahuni wenye degree tatu tu!!
 
Nimeona umepost video nyingine kwa kutumia ukurasa wa Msemaji wa serikali ukidai katika mpango wa maendeleo wa Taifa ambao uliasisiwa na Mkapa hakuna sehemu inataja tunahitaji kufikia kipato cha kila mtu cha USD 3,000.

Kila mtanzania anajua unajibidisha kumjibu JM Kikwete baada ya kuweka sawa mpango wa maendeleo wa taifa ambao ofisi yako ya msemaji wa serikali mlisha anza kudanganya umma kwamba tumefikia kabla ya wakati.

Naomba nikukumbushe yafuatayo.

1.Katika Mpango wa miaka mitano wa mwaka 2016 ambao ni subset ya mpango wa 2025 ambao huwekwa kila baada ya miaka mitano, bosi wako Dr John Magufuli katika utangulizi anataja usd 3,000 kama kipato tunacho takiwa kufikia ifikapo 2025. Kwa namna moja unapingana na bosi wako na kumtia aibu na kufanya wananchi tuamini kwamba ndio anakutuma uongee huu utumbo wa darasa la kwanza.

2. Pia Kikwete amekua Rais wa Tanzania kwa miaka 10, na katika miaka hiyo 10 Mapango huu wa maendeleo alikua ndio akiamka nao na kulala nao maana utekelezaji wake wote ulikua kwenye mpango huu. Tofauti na mtu kama Dr Abbasi ambaye upo tu kuonyesha sura kwenye vyombo vya habari nna kupalilia kakitambi kaendelee kuonekana. Kiukweli utatia Aibu.

3. Sijui unasoma wapi huo udaku kwamba hakuna sehemu inaeleza kipato cha usd 3,000.

4. Watanzania wanaomba uwaombe radhi, Kazi imekushinda. Tunajua Dr magufuli hajakutuma ila unajaribu kujipendekeza kulinda kibarua chako wakati Dr Magufuli anajua nini maana ya mpango wa maendeleo 2025.

Dr Abbasi elimu yako inatupa mashaka kama hata kusoma tu unapata shida.
J. Kikwete rais bora huyo msemaji amevimbiwa na kodi zetu
 
Back
Top Bottom