Dkt. Hassan Abbas usipambane na Kikwete siyo saizi yako. Acha kupotosha umma kwa njaa zako

Hiv anapga mishahara miwili au imekaaje?
Huyu Ndugu ameshikilia vyeo viwili:
1.Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,na
2.Msemaji wa Serikali
Sasa ni wakati muafaka akatafutwa mtu mwingine kujaza nafasi ya Msemaji wa Serikali,ili sasa Dr.Abbas ajikite na Ukatibu Mkuu wa Wizara!!
 
Kwanza mambo mengi yalikuwa ni mashinikizo toka mashirika ya kimataifa ya maendeleo ya uchumi Yani WB na IMF na kwa jinsi ilivyokuwa mtu yeyote ambae angekuwepo kama rais wakati huo angefanya hivyo hivyo kwa hiyo sizani kama kulifanyika ugunduzi au ubunifu wa ziada wa kuhitaji pongezi za kiivyo inavyovumishwa!
 
Kama taifa unafukiria tufanye nini kukikomboa kizazi kijacho kutoka kwenye tatizo hili? Mchango wako umenifikirisha sana.
Tunatakiwa tubadili tamaduni zetu.

Kwa mfano, tuheshimu kufikiri kwa kina na kupangilia maneno.

Kikwete alijitahidi sana katika hotuba yake. Kwa kweli Kikwete ame evolve sana katika urais wake na hata sasa baada ya kuwa rais. Ukimsikiliza Kikwete wa 2005 na kabla, umlinganishe na Kikwete wa 2015 na baadaye, kuna tofauti kubwa.

Lakini hata yeye bado ana matatizo katika kujieleza. Amefanya vitu angalau viwili ambavyo vimemletea matatizo.

Amefanya kitu katika Kiingereza wanaita "meandering". Yani kazunguka zunguka sana, mpaka kaacha mianya ya kutafsiriwa vibaya, hata kama hakuwa na nia mbaya.

Kikwete anaweza kuuanganisha bonge la meander, halafu akamalizia na sentensi iliyoachwa hewani akasema "aaah, basi tu". Na kila Mswahili akaondika na tafsiri anayoitaka yeye!

Hii habari ya meandering hata Nyerere nimemsikia. Mwanzo nilifikiri ni repetition for effect (hii hata Martin Luther King Jr. aliifanya katika speech ya "I Have A Dream). Ila nikaja kugundua, speeches makini kabisa za Nyerere zilikuwa ni zile za zamani, alivyozidi kukaa madarakani, no doubt alikuwa anatoa speeches nzuri -huwezi kumlinganisha na mtu kama Magufuli hata kidogo- lakini kadiri na mimi nilivyokua mkubwa na kusikiliza speeches za viongozi wengi wa kimataifa, nikaona Nyerere, especially speeches za uzeeni, alikuwa ana meander.

Halafu nikasoma kitabu cha Paul Bjerk "Julius Nyerere", a very good and impartial book, nikaona Bjerk naye amelisema hili la Nyerere ku meander vile vile nilivyoona mimi kabla.

So, kitu kingine cha kuangalia kwenye mawasiliano ni kujifunza kuwasiliana with a purpose. No meandering. Ikibidi, mtu anataja purpose kabisa, mwanzo. Leo nataka kusema hili na hili na hili. Halafu kila unachosema kinahusiana na message yako. Wenyewe wanasema "Stay on message".

Turudi kwa Kikwete.Kikwete pia hakuwa na maneno ya kuunganisha nia/ ajenda yake na kile alichokisema. Ni kama aliacha gaps ufanye homework kuunganisha mambo mengine aliyoyasema na Mkapa. Alitakiwa kuunganisha kiasi hata mtu ambaye haijui Tanzania akimsikiliza, aelewe kwamba hapa kasema hivi kwa sababu hii. No room for misinterpretation.

Nyerere alikuwa na uwezo mkubwa sana wa kuelezea maneno yake ukamuelewa hapa kasema hivi kwa sababu hii. At his best -when not meandering- alipenda simplicity na ku connect dots kama anafundisha. Nafikiri kwenye hili ndiye the best president.

Utamsikia "Ndugu wananchi sasa nataka kusema hili hili na hili. Hapa ikiwa hivi pale itakuwa vile. Na ikiwa vile ni sawa kwa sababu hii na hii. Ikiwa hivi si sawa kwa sababu hii na hii. Tunataka kufanya hivi, kwa sababu hii na hii". Anahutubia lakini anafundisha hapo hapo. Ndiyo maana akaitwa Mwalimu.

Anakueleza vizuri. Nafikiri kuwa Mwalimu siku nyingi na kuhutubia sana kulimsaidia.

Hiki ni kitu kizuri kujifunza.

Kikwete kwenye msiba alianza na flow vizuri katikati akawa ana freestyle tu.

Sasa tatizo la ku freestyle, kama mtu una mapungufu, ndiyo unaanza kutoa habari kama za Makonda alivyoharibu kwenye msiba wa Mengi. Unaweza kuona unamsifia Mengi, kumbe unakashifu Wachaga. Makonda alifanya hivyo. Kwa Kikwete, unaweza kuona unamsifia Mkapa, kumbe wengine wanatafsiri unampiga vijembe Magufuli.

Mtu kama Mkapa alikuwa na discipline kubwa sana ya kuandika almost kila hotuba yake. Aliheshimu mawasiliano. Alijua kupanga maneno si kazi rahisi kama inavyoonekana.

Kikwete amesema maneno kutoka moyoni, mwishowe akakumbusha Vision 2025, nafikiri kwa nia njema tu ya kuonesha tulipotoka na Mkapa, na kutoa challenge kwa Magufuli (kisaikolojia Magufuli ni Waziri wa Kikwete hata kama sasa ni rais). Watu wametafsiri kama kijembe.

Tunatakiwa kujenga utamaduni wa:-

1. Kuheshimu mawasiliano. Mawasiliano si kitu kidogo kama wengi wanavyofikiri. Kupanga mantiki ni kazi. Kupanga maneno ya kuwakilisha mantiki ni kazi ya ngazi nyingine tofauti. Kufafanua ili ueleweke vizuri ni kazi nyingine. Ku anticipate reaction ya audience yako ni kazi. Wengi tunaona mawasiliano ni kitu rahisi tu.

2.Kuacha kufikiri kwamba kila mtu atafikiri sawa na sisi, au atatuelewa tu. Watu wengi hata wakikosea, wakisahihishwa wanakimbikia kusema "si umeelewa?". Utajuaje nimeelewa wakati umekosea kuwasilisha?

3. Tufundishe watoto matamshi mazuri, clarity katika kujieleza. Tuwajengee msamiati wawe na utajiri wa kujieleza. Tujenge mazingira wajifunze mantiki. Matatizo yetu mengi ya mawasiliano yanatokana na elimu duni ya mantiki. Mtu kama hana elimu ya mantiki ni vigumu hata kupanga maneno ajieleze vizuri.

4. Matatizo ya mawasiliano yana mizizi mirefu kwenye matatizo mengine mapana zaidi. Kwa mfano, nchi yenye watu waliotawaliwa na woga (kuogopa serikali kwa mfano)haiwezi kukosa matatizo ya mawasiliano. Ni vigumu mtu kujieleza vizuri ikiwa unajieleza kwenye mazingira ya woga. Wewe angalia watu wanaohojiwa na Magufuli anavyowatia jambajamba mpaka wanashindwa kujieleza. Mtu hata kama ana points, kwa kuhojiwa kiukali tu na Magufuli anashindwa hata kupanga points zake. Matokeo yake rais akishaondoka mtu ndiyo anakumbuka cha kusema. Tuondoe woga, tusafishe mifumo yetu iwe wazi. Tuache roho mbaya.

Ukimpiga mtoto na kumtisha, usitegemee aje kuwa mtu anayeweza kuwa na mawasikiano mazuri baadaye. Atakuwa mwogamwoga tu.

5.Tuzidishe kusoma. Kusoma kunafungua fikra na kumuwezesha mtu kupata utajiri wa lugha, msamiati, sarufi, dhana mbalimbali na hata kujiamini tu. Pia, kupitia kusoma vitu tofauti, unaweza kupata uthibitisho zaidi wa mambo uliyofikiri unayaona wewe tu. Kwa mfano, nimekitaja kitabu kinaitwa "Julius Nyerere" cha Paul Bjerk. Kwa muda mrefu nimekuwa nikifikiri Nyerere alikuwa ana meander, ingawa si sana, lakini kuna sehemu ali meander na kujirudia rudia over and above the usual dramatic effect level (sikiliza hotuba aliyomsema Oscar Kambona ni malaya na mercenary, karudia saaana tu maneno yale yale). So, nimeliona hili, lakini nikafikiri labda ni mimi tu na critical mind yangu. Nimemsoma Paul Bjerk katika "Julius Nyerere", nikakuta na yeye kaandika hilo.

So, kusoma kunasaidia sana kuweza kujenga sio tu mawasiliani mazuri, bali pia kuongeza elimu.

Mambo ni mengi sana, muda mchache.

Kwa leo naomba niishie hapa.
 
Tunatakiwa tubadili tamaduni zetu.

Kwa mfano, tuheshimu kufikiri kwa kina na kupangilia maneno.

Kikwete alijitahidi sana katika hotuba yake. Kwa kweli Kikwete ame evolve sana katika urais wake na hata sasa baada ya kuwa rais. Ukimsikiliza Kikwete wa 2005 na kabla, umlinganishe na Kikwete wa 2015 na baadaye, kuna tofauti kubwa.

Lakini hata yeye bado ana matatizo katika kujieleza. Amefanya vitu angalau viwili ambavyo vimemletea matatizo.

Amefanya kitu katika Kiingereza wanaita "meandering". Yani kazunguka zunguka sana, mpaka kaacha mianya ya kutafsiriwa vibaya, hata kama hakuwa na nia mbaya.

Kikwete anaweza kuuanganisha bonge la meander, halafu akamalizia na sentensi iliyoachwa hewani akasema "aaah, basi tu". Na kila Mswahili akaondika na tafsiri anayoitaka yeye!

Hii habari ya neandering hata Nyerere nimemsikia. Mwqnzo nilifikiri ni repetition for effect (hii hata Mqrtin Luther King Jr. aliifanya katika soeech yq "I Have A Dream). Ila nikajq kugundua, speeches makini kqbisa za Nyerere zilikuwa ni zike za zamani, alivyozidi kukaa madarakani, no doubt alikuwa qnqtoa speeches nzuri -huwezi kumlingqnisha na mtu kama Magufuli hata kidogo- lakini kadiri na mimi nilivyokua mkubwa na kusikiliza speeches za viongozi wengi wa kimataifa, nikaona Nyerere, esoecially soeeches za uzeeni, alikuwa ana meander.

Halafu nikasoma nikabu cha Paul Bjerk "Julius Nyerere", very good and impartial book, nikaona Bjerk naye amelisema hili la Nyerere ku meander vile vile nilivyoona mimi.

So, kitu kingine cha kuangakia kwenye mawasiliano ni kujifynza kuwasiliana with a purpose. No meandering. Ikibidi, mtu anataja purpose kabisa, mwanzo. Leo nataka kusema hili na hili na hili. Halafu kila unachosema kinahusiana na message yako. Wenyewe eanasema "Stay on message".

Turudi kwa Kikwete.Kikwete pia hakuwa na maneno ya kuunganisha nia/ ajenda yake na kike alichokisema. Ni kama aliacha gaps ufanye homework kuunganisha mambo mengine aliyoyasema na Mkapa. Alitakiwa kuunganusha kiasi hata mtu ambaye haijui Tanzania akimsikiliza, aelewe kwamba hapa kasema hivi kwa sababu hii. No room for misinterpretation.

Nyerere alikuwa na uwezo mkubwa sana wa kuelezea maneno yake ukamuelewa hapa kasema hivi kwa sababu hii. Alipenda simplicity na ku connect dots kama anafundisha.

Utamsikia "Ndugu wananchi sasa nataka kusema hili hili na hili. Hapa ikiwa hivi pale itakuwa vile. Na ikiwa vike ni sawa kwa sababu hii na hii. Ikiwa hivi si sawa kwa sababu hii na hii". Anahutubia lakini anafundisha hapo hapo. Ndiyo maana akaitwa Mwalimu.

Anakueleza vizuri. Nafikiri kuwa Mwalimu siku nyingi na kuhutubia sana kulimsaidia.

Hiki ni kitu kizuri kujifunza.

Kikwete Alianza na flow vizuri katikati akawa ana freestyle tu.

Sasa tatizo la ku freestyle, kama mtu una mapungufu, ndiyo unaanza kutoa habari kama za Makonda alivyoharibu kwenye msiba wa Mengi. Unaweza kuona unamsifia Mengi, kumbe unakashifu Wachaga. Makonda akifanya hivyo. Kwa Kikwete, unaweza kuona unamsifia Mkapa, kumbe wengine wanatafsiri unampiga vijembe Magufuli.

Mtu kama Mkapa alikuwa na discipline kubwa sana ya kuandika almost kila hotuba yake. Aliheshimu mawasiliano. Alijua kupanga maneno si kazi rahisi kama inavyoonekana.

Kikwete amesema maneno kutoka moyoni, mwishowe akakumbusha Vision 2025, nafikiri kwa nia njema tu ya kuonesha tulipotoka na Mkapa, na kutoa challenge kwa Magufuli (kisaikolojia Magufuli ni Waziri wa Kikwete hata kama sasa ni rais). Watu wametafsiri kama kijembe.

Tunatakiwa kujenga utamaduni wa:-

1. Kuheshimu mawasiliano. Mawasiliano si kitu kidogo kama wengi wanavyofikiri.

2.Kuacha kufikiri kwamba kila mtu atafikiri sawa na sisi, au atatuelewa tu. Watu wengi hata wakikosea, wakisahihishwa wanakimbikia kusema "si umeelewa?". Utajuaje nimeelewa wakati umekosea kuwasilisha?

3. Tufundishe watoto matamshi mazuri, clarity katika kujieleza. Tuwajengee msamiati wawe na utajiri wa kujieleza. Tujenge mazingira wajifunze mantiki. Matatizo yetu mengi ya mawasiliano yanatokana na elimu duni ya matiki. Mtu kama hana elimu ya mantiki ni vigumu hata kupanga maneno ajieleze vizuri.

4. Matatizo ya mawasiliano yana mizizi mirefu kwenye matatizo mengine mapana zaidi. Kwa mfano, nchi yenye watu waliotawaliwa na woga (kuogopa serikali kwa mfano)haiwezi kukosa matatizo ya mawasiliano. Ni vigumu mtu kujieleza vizuri ikiwa unajieleza kwenye mazingira ya woga. Wewe angalia watu wanaohojiwa na Magufuli anavyowatia jambajamba mpaka wanashindwa kujieleza. Mtu hata kama ana points, kwa kuhojiwa kiukali tu na Magufuli anashindwa hata kupanga points zake. Matokeo yake rais akishaondoka mtu ndiyo anakumbuka cha kusema. Tuondoe woga, tusafishe mifumo yetu iwe wazi. Tuache roho mbaya.

Ukimpiga mtoto na kumtisha, usitegemee aje kuwa mtu anayeweza kuwa na mawasikiano mazuri baadaye. Atakuwa mwogamwoga tu.

5.Tuzidishe kusoma. Kusoma kunafungua fikra na kumuwezesha mtu kupata utajiri wa lugha, msamiati, sarufi, dhana mbalimbali na hata kujiamini tu. Pia, kupitia kusoma vitu tofauti, unaweza kupata uthibitisho zaidi wa mambo uliyofikiri unayaona wewe tu. Kwa mfano, nimekitaja kitabu kinaitwa "Julius Nyerere" cha Paul Bjerk. Kwa muda mrefu nimekuwa nikifikiri Nyerere alikuwa ana meander, ingawa si sana, lakini kuna sehemu ali meander na kujirudia rudia over and above the usual dramatic effect level (sikiliza hotuba aliyomsema Oscar Kambona ni malaya na mercenary, karudia saaana tu maneno yale yale). So, nimeliona hili, lakini nikafikiri labda ni mimi tu na critical mind yangu. Nimemsoma Paul Bjerk katika "Julius Nyerere", nikakuta na yeye kaandika hilo.

So, kusoma kunasaidia sana kuweza kujenga sio tu mawasiliani mazuri, bali pia kuongeza elimu.

Mambo ni mengi sana, muda mchache.

Kwa leo naomba niishie hapa.
Wakati Mwalimu Nyerere anafariki, kuna Mzungu aliandika anavyomfahamu Nyerere. Lile chapisho nililitafuta sana niliweke hapa sijalipata mitandaoni. Katika kuhama hama nyumba lile jarida nililipoteza.

Yule Mzungu alieleza Mwalimu alipokuwa Edinburgh aliwashangaza kwa uwezo wake wa kusoma mambo na kuyaelezea katika lugha nyepesi na wote wakamuelewa.

Unajua baadhi ya shule za dini wanapata bahati ya kufundishwa jinsi ya kupanga mtiririko wa maongezi kimaandishi na ki hotuba.
 
Ungeweka hizi facts bila kumshambulia Abbas bado inge make sense tu mbona?.

Mkuu:
Ni dalili ya uungwana pindi mtu anapokosea kusahihishwa pasipo kumumunya maneno na aliye kosea ni vyema kukiri, hayati Mzee wetu Benjamin Mkapa ametufundisha hivyo.
 
Mnafik wa kiwango cha lami hawa watakua kuni za kichomea wengine motoni
Dkt abbasi akitafuta kwenye vision 2025 wapi wametaja USD 3000.
1596265553068.jpeg
 
Wakati Mwalimu Nyerere anafariki, kina Mzungu aliandika anavyomfahamu Nyerere. Lile chapisho nililitafuta sana niliweke hapa sijalipata mitandaoni. Katika kuhama hama nyumba lile jarida nililipoteza.

Yule Mzungu alieleza Mwalimu alipokuwa Edinburgh aliwashangaza kwa uwezo wake wa kusoma mambo na kuyaelezea katika lugha nyepesi na wote wakamuelewa.

Unajua baadhi ya shule za dini wanapata bahati ya kufundishwa jinsi ya kupanga mtiririko wa maongezi kimaandishi na ki hotuba.
Nyerere alikuwa New York, kipindi cha TV cha Mrs. Eleanor Roosevelt, former first lady wa US, mke wa Franklin Delano Roosevelt. Mwaka 1959. Kipindi hicho anaenda sana UN kudai uhuru.

Sasa katika ile TV show kukawa na panel, Nyerere akaulizwa.

Nyie Waafrika mnadai uhuru, kweli mtaweza kujumitawala? Mbona kama bado?

Hilo jibu lake sasa.

Akawajibu akawaambia, nyie mmemkuta mtu ana jaketi lake kalivaa, mmemuibia, sasa analidai jaketi lake mumrudishie.

Mnasema hili jaketi halikufai wewe, si saizi yako. Lakini niblangu, nioeni mwenyewe jaketi langu iama linanitisha au halinitoshi si kazi yenu kuamua.

Ikabidi wakubali wenyewe.

Siku nyingine alikuwa anaelezea changamoto za uhuru, hapi kabla ya uhuru anawaandaa watu.

Akasema kulikuwa na wawindaji kadhaa, wote wamekubaliana kuwinda pamoja. Wameqinda vizuri, wameua mnyama. Kazi ya kuwinda wameimaliza vizuri. Tatizo likaja kwenye kugawana nyama. Kila mtu anataka apate zaidi.

Alionya kuhusu mshikamano uliokuwepo kabla ya kupata uhuru kuweza kuvunjika baada ya kuoata uhuru.

Huu mfano mpaka leo huwa nautumia ninaposikia wapinzani wanataka kuungana waweke mgimbea mmoja kwa nia ya kupata urais, wakati hawana muungani wa kweli wa kiitamikadi utakaosababisha waendelee kuungana hata baada ya kupata urais.

Alikuwa na mifano mingi kama hiyo ambayo iliweza kufanya jambo complex liweze kueleweka kirahisi kabisa.

Na mimi nimejifunza sana kutumia mifano ya hivyo kufikisha ujumbe kirahisi.

Sikikiza kuanzia dakika around ya 5 hapo.

Nyerere anawajibu around dakika ya 8.

Hatujui wapi mtu kapiga kijembe, na wapi mtu alikuwa anatoa historia tu ya Vision 2025 kumuenzi Mkapa.

Mimi naona huu mzozo si ugonjwa, huu mzozo ni dalili ya ugonjwa tu.

Ugonjwa wenyewe ni hii roho mbaya na kuweka mbele vijembevijembe.

Kwa sababu, kwa nchi ambayo watu wanaheshimiana na hakuna kuendekeza vijembevijembe, unatakiwa kumpa mtu mwenye heshima yake kama ex president the benefit of doubt.

Baada ya kuwa madarakani tangia uhuru na baada ya kukandamiza upinzani rasmi kwa mabavu ya dola, wazee wa CCM wamejikuta wakikosa mshindani wa nje wa kujipima naye ili kuonyesha tofauti za kiutendaji au hata kumnyooshea kidole kwa utendaji wa ovyo miaka ya nyuma.

Kilichobakia ni kugeukiana wao kwa wao. Kila awamu inapoingia madarakani hujifanya ni taasisi tofauti iliyokuja kuleta “mageuzi makubwa” kusafisha “uozo” ulioachwa na awamu zilizopita! Hii ndio namna yao ya kujisafisha, kujitenga na watangulizi na kujiuza kwa wananchi - kwa kufikiri wanaongoza nchi ya watu wasiojielewa kabisa. Awamu ya 5 ndiyo imekithiri kwa kutumia mkakati huu kiasi kwamba hata serikali na CCM leo zinatambulika kwa jina la mtu mmoja; sio taasisi huru tena.

Kwa mtindo huo, vijembe ni lazima, hakuna namna. Chama ni kimoja. Ili kidumu (survive), ushindani hauna budi kuongozwa na fitna, mipasho na vijembe baina ya watu (individuals). Lissu alishasema: “wakimalizana na sisi watawageukia nyinyi (wa chama tawala)”.

Kwa kifupi, kama hakutafanyika juhudi za dhati kurejesha “sanity” kwenye mfumo wetu wa siasa na utawala, tujue tutaendelea kuongozwa kihuni hadi tufikie hali mbaya sana. Taasisi zetu za utawala hivi leo zinavutia watu wa ajabu ajabu kutuongoza. Wao badala ya kufanya kazi kwa umakini wanatumia rasilimali, nguvu na muda mwingi kufuatilia na kujibu kwa mipasho kila kauli hata za “mitandaoni” zinazohisiwa “kupingana” na utendaji wao.
 
Kuna siku nilimtembelea mzee wangu mmoja, alikuwa kigogo wa usalama.

Basi nikamkuta anaongea na mkewe, ka relax katika family setting.

Hizo story zao basi, weee. Yani walikuwa wanaongea kigogo huyu kam double cross yule, huyu kamzika yule, yule kapigwa na yule. Mpaka nikashangaa.

Kabla ya hapo nilikuwa nafikiri hawa vigogo wameshikana sana, wote wamoja, wamekaa pamoja kujipanga kuwapiga wananchi.

Nikaja kugundua kumbe unavyozidi kupanda juu na fitna zinazidi, mitego inazidi. Hata wenyewe hawapatani.

Na siku zinavyozidi mipasuko inazidi. Zamani ilikuwa viongozi kama kina Nyerere wanaheshimiwa sana, mambo ya mipasuko yanafanywa kisirisiri, mipasuko wanaijua wenyewe ndani. Huku nje wananchi hatujui. Ni kama baba na mama wanapigana chumbani, watoto hawajui. Heshima ya watoto inabaki.

Sasa baada ya enzi ya Nyerere kupita, hawa wengine wote wamekua pamoja, kila mtu anajua mafauki ya mwenzake, wananyukana mbwai mbwai tu.

Umeongelea kuhusu CCM. Kilichotokea ni kike alichokisema Nyerere. Dhambi ya ubaguzi ukianza huachi. Ni kama kula nyama ya mtu. CCM wamebagua wapinzani, wamewalaza chaki, sasa wanaanza kubaguana wenyewe kwa wenyewe. Na ubaguzi wa ndani ulianza chini.

Leo mpaka msemaji wa serikali anaenda kumsema Kikwete!
 
Kubali au kataa, Kikwete hakumtendea haki Magufuli!!!! Unafiki wa Kikwete utaleta matatizo mbeleni. Hayo alitakiwa kumweleza wakiwa chemba si mbele ya kadamnasi. Rules za uongozi zinakataza vitu kama hivyo na uliona JPM alivyolowa.
Mbona mzee baba huwa anawalipua wenzake hadharani
 
Kubali au kataa, Kikwete hakumtendea haki Magufuli!!!! Unafiki wa Kikwete utaleta matatizo mbeleni. Hayo alitakiwa kumweleza wakiwa chemba si mbele ya kadamnasi. Rules za uongozi zinakataza vitu kama hivyo na uliona JPM alivyolowa.
Hivi magufuli anapo wadhihaki watangulizi wake mbele ya kadamnasi kwamba hawajafanya lolote ulishawahi lalamika au ndio mahaba niue?
 
Baada ya kuwa madarakani tangia uhuru na baada ya kukandamiza upinzani rasmi kwa mabavu ya dola, wazee wa CCM wamejikuta wakikosa mshindani wa nje wa kujipima naye ili kuonyesha tofauti za kiutendaji au hata kumnyooshea kidole kwa utendaji wa ovyo miaka ya nyuma.

Kilichobakia ni kugeukiana wao kwa wao. Kila awamu inapoingia madarakani hujifanya ni taasisi tofauti iliyokuja kuleta “mageuzi makubwa” kusafisha “uozo” ulioachwa na awamu zilizopita! Hii ndio namna yao ya kujisafisha, kujitenga na watangulizi na kujiuza kwa wananchi - kwa kufikiri wanaongoza nchi ya watu wasiojielewa kabisa. Awamu ya 5 ndiyo imekithiri kwa kutumia mkakati huu kiasi kwamba hata serikali na CCM leo zinatambulika kwa jina la mtu mmoja; sio taasisi huru tena.

Kwa mtindo huo, vijembe ni lazima, hakuna namna. Chama ni kimoja. Ili kidumu (survive), ushindani hauna budi kuongozwa na fitna, mipasho na vijembe baina ya watu (individuals). Lissu alishasema: “wakimalizana na sisi watawageukia nyinyi (wa chama tawala)”.

Kwa kifupi, kama hakutafanyika juhudi za dhati kurejesha “sanity” kwenye mfumo wetu wa siasa na utawala, tujue tutaendelea kuongozwa kihuni hadi tufikie hali mbaya sana. Taasisi zetu za utawala hivi leo zinavutia watu wa ajabu ajabu kutuongoza. Wao badala ya kufanya kazi kwa umakini wanatumia rasilimali, nguvu na muda mwingi kufuatilia na kujibu kwa mipasho kila kauli hata za “mitandaoni” zinazohisiwa “kupingana” na utendaji wao.
Hii awamu ya tano ni utopolo,yaani hata wanaowalinda akili zao huwa sizielewi kabisa
 
Kwa nchi za wenzetu huyu alitakiwa tayari ameshajiudhuru kwa kukosa weledi kuisemea serikali kitu ambacho hakijui.

Ni mambo ya ajabu msemaji wa serikali kutokujua development vission 2025 ilitaka per capita income ifikie USD ngapi.
Tunakwama wapi Kama taifa. Tusipende kupindisha pindisha mambo hata Yale ambayo Ni documentary planned and known ili kujizolea umaarufu kisiasa
 
Back
Top Bottom