Dkt. Gwajima ahimiza uharaka katika upatikanaji haki kwenye vitendo vya ukatili

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
2,844
2,000
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk Dorothy Gwajima amewaagiza maafisa jamii nchini kote kuhakikisha wanawezesha upatikanaji wa haki kwa wakati kwa wanaofanyiwa vitendo vya ukatili

Gwajima amebainisha hayo leo Jijini Dodoma alipozungumza na vyombo vya habari kuhusiana na mwenendo wa vitendo vya ukatili hapa nchini

“Niwaase maafisa jamii katika halmashauri zote nchini kushughulikia ipasavyo ukatili dhidi ya wanawake, wanaume, watoto na wazee kwa kuhakikisha haki za wananchi wanaofanyiwa vitendo hivyo ikiwemo makundi tete zinapatikana kwa wakati” amesema Dkt. Gwajima.
 

ras jeff kapita

JF-Expert Member
Jan 4, 2015
10,505
2,000
huyu atakuwa ni zaidi ya waziri wa afya, hapa ana act kama waziri wa sheria...mangosha yanatamba sana awamu hii!
Naona hajui mpaka wake, maeneo yake ni magonjwa, dawa na matibabu,Ila naona ndio waziri anayebamba sana kwa sasa hakuna mwingine
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom