Dkt. Emmanuel Nchimbi alishindwa Uwaziri ameshindwa Ubalozi tutampeleka wapi?

kifupi kirefu

JF-Expert Member
Oct 29, 2018
539
3,507
Dr. Emmanuel Nchimbi akiwa Waziri wa Mambo ya ndani ndipo iliposhamiri matukio ya kuteswa waandishi wa habari ikiwemo kifo Cha Mwangosi huko Iringa.

Baada ya kuonekana Hana Jambo lolote alilofanikiwa kwenye Wizara hiyo na baada ya kumuunga mkono Lowasa chama kikamkataa.

Akazunguka kidogo Kwa mwamvuli wa Lowassa upinzani lakini akatishwa Kwa kashfa ya kula fedha za ujenzi wa jengo la UVCCM na kupelekea kuanza mchakato wakumfikisha mahakamani.

Alipoona dola imemgeuka kumulika maovu yake akaenda kuomba msamaha kama alivyofanya Nape ndipo JPM akamsamehe na kumpeleka Ubalozini Brazil. Toka ameenda Ubalozi hajawahi kufanya kitu chochote si kwa sababu nyingine bali ni kwa sababu ya uwezo mdogo wa kimkakati.

Leo tumeshuhudia ameondolewa Ubalozini na naamini atarejea nchini. Wakati anarejea nchini. Akiwa njiani wapo watu wanatudanganya kwamba huyu ni jembe la siasa lakini jiulize amefanya nini kwenye siasa? Amewahi kufanikisha mpango gani endelevu Kwa nchi hii?

Mfumo wa siasa za Tanzania hasa siasa za CCM unategemea dola na siyo nguvu ya mtu. Nchimbi Kwa alivyo hata akipewa mabilioni Leo akitoe chama kwenye makucha ya dola kiweze kujisimamia awezi kushawishi mtu yeyote. Hivyo kumwona mtu aliyefeli kama shujaa ni kupumbaza werevu Kwa maisha ya kujipendekeza. I believe there is no strategy in Nchimbi and will never be.
 
He's a hopeless dude, just like January and Nape! Hawa watu wameingia kwenye system kwa kubebwa, siyo kwa kufanya kazi wao wenyewe mpaka wakaonekana. Kama Rais Samia anategea kuzungukwa na watu kama hawa asitegemee mafanikio yoyote.
 
Rais anateua watu wenye kashifa na tuhuma mbaya huko nyuma.

Na Hawa ndo watu wake kina MAROPE, NYAPE, MWIGU, NCHIMBIMBI, MZITO KABWELA, LIZI.

ndo safu yake eti anaijenga,afu kesho watu wakimpopoa anasema hatokubali
 
He's a hopeless dude, just like January and Nape! Hawa watu wameingia kwenye system kwa kubebwa, siyo kwa kufanya kazi wao wenyewe mpaka wakaonekana. Kama rais Samia anategea kuzungukwa na watu kama hawa asitegemee mafanikio yoyote.
Kwani namba moja yeye kaingia system kwa kubebwa au kwa kufanya kazi yeye mwenyewe? Tuanzie hapo kwanza kabla ya kuwajadili wateule wake.
 
Emmanuel Nchimbi hajiwezi asilani. Yeye ni Kobe aliyekuwa mtini baada ya mwenye Kobe kumuweka mtini.

DNA ya Nchimbi ni sawa kabisa na ya Bashite aka Paul Makonda. Nchimbi kafoji PhD, Bashite alifoji O-Level. Nchimbi ndiye muasisi wa utekaji wa akina Dr Ulimboka, mauaji ya Mbauda Kanisani na Mwangosi.

Bashite aliteka kuna Roma, Dewji na mashambulizi ya Lissu, mauaji Ben Saanane.

Emmanuel Nchimbi asijifanganye kabisa, haendani na falsafa ya Rais SSH
 
Da mapema mmeanza kumshambulia mzee wa wawatu.subirini 2025 ndio kampeni zianze sio sasa hivi.
Tunajua urais ni Taasisi yeyote anauweza.
 
He's a hopeless dude, just like January and Nape! Hawa watu wameingia kwenye system kwa kubebwa, siyo kwa kufanya kazi wao wenyewe mpaka wakaonekana. Kama rais Samia anategea kuzungukwa na watu kama hawa asitegemee mafanikio yoyote.
Hata waimba mapambio tegemewa mnaanza kuwa kana mlio waimbia mapambio miaka nenda Rudi, ama kweli Dunia inaenda Kasi kweri kweri🤔.
 
Dr. Emmanuel Nchimbi akiwa Waziri wa Mambo ya ndani ndipo iliposhamiri matukio ya kuteswa waandishi wa habari ikiwemo kifo Cha Mwangosi huko Iringa. Baada ya kuonekana Hana Jambo lolote alilofanikiwa kwenye Wizara hiyo na baada ya kumuunga mkono Lowasa chama chama kikamkataa. Akazunguka kidogo Kwa mwamvuli wa Lowasa upinzani lakini akatishwa Kwa kashfa ya kula fedha za ujenzi wa jengo la UVCCM nakupelekea kuanza mchakato wakumfikisha mahakamani. Alipoona dola imemgeuka kumulika maovu yake akaenda kuomba msamaha kama alivyofanya Nape ndipo JPM akamsamehe na kumpeleka Ubalozini Brazili. Toka ameenda Ubalozi hajawahi kufanya kitu chochote si kwa sababu nyingine bali ni kwa sababu ya uwezo mdogo wakimkakati.

Leo tumeshuhudia ameondolewa Ubalozini na naamini atarejea nchini. Wakati anarejea nchini. Akiwa njiani wapo watu wanatudanganya kwamba huyu ni jembe la siasa lakini jiuize amefanya Nini kwenye siasa? Amewahi kufanikisha mpango gani endelevu Kwa nchi hii?

Mfumo wa siasa za Tanzania hasa siasa za CCM unategemea dola na siyo nguvu ya mtu. Nchimbi Kwa alivyo hata akipewa mabilioni Leo akitoe chama kwenye makucha ya dola kiweze kujisimamia awezi kushawishi mtu yeyote. Hivyo kumwona mtu aliyefeli kama shujaa nikupumbaza werevu Kwa maisha yakujipendekeza. I believe there is no strategy in Nchimbi and will never be
Wale wote ambao tangu wanatoka shule hujiingiza katika siasa za ccm huwa wenye roho mbaya mfano ni huyu, makonda-bashite, mwigulu, sabaya etc..

ccm wanajijua wenyewe
 
Back
Top Bottom