Dkt. Chriss Cyrilo (MD): Mwongozo wa wizara ya Afya nchini Tanzania unasema hadi sasa hakuna dawa ya kutibu ugonjwa wa covid19.

Sasa ni wapi madaktari wamethibitisha kuwa hii dawa inatibu korona, tofauti na DJ Rajoelina? Sometimes tufuate wataalam hizi abracadabra haziwezi kutufikisha popote,yale ya kikombe cha babu wa Loliondo yanataka kujirudia
Ni wapi ulisikia corona anaumwa hata atibiwe?
 
Hayo mambo ya kina doctor mwaka , wapi na wapi na MD , kwenye MD hakuna hivyo vitu.

Toka lini MTU kaenda hospital kakutwa na malaria doctor akamuandikia akatumie muarobaini .

Sent using Jamii Forums mobile app

Wengine hatumjui Dr Mwaka lakini kwa tiba lishe hakuna mwingine hapa Tz na ndio maana Kigwangala alikuwa na kiroho jiba sana kwa elimu ya yule bwana
 
Kwani huko Madagascar hakuna wataalamu?

Waliomhakikishia Rais wa nchi yao ni hao wataalamu
Sasa ni wapi madaktari wamethibitisha kuwa hii dawa inatibu korona, tofauti na DJ Rajoelina? Sometimes tufuate wataalam hizi abracadabra haziwezi kutufikisha popote,yale ya kikombe cha babu wa Loliondo yanataka kujirudia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nafasi kibao chadomo wala si za kugombania, hulijuwi hilo?
Ivi kumbe na huyu dada na yy hua anatafuta uteuzi, duuh pole, sema awam hii raisi anawaamini wapinzani Sana , anawaita wajiunge na ccm kisha anawateua , ccm vindaki ndaki wanabaki wanatoa macho . pole Sana Dada kazi unayo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimewahi kuona mtu katapeli mtu au kikundi cha watu au taasisi. Pia nimewahi kuona taasisi au kikundi cha watu kimetapeli mtu.

Katika maisha yangu sijawahi kuona nchi imetapeli nchi. Hili ni tukio la kwanza kwangu.
 
Wewe hujawahi kumuona au kumsikia Dakatari akikwambia kula aina Fulani ya chakula. Au matunda?

Kama si alternative medicine ni nini hicho?

Tanzania kwa "wasomi" kama wewe tuna Safari ndefu sana ya kwenda.
FaizaFoxy
Daktari= Dakatari

Hivyo shule mlienda somea ujinga?
In FaizaFoxy's voice
 
Naiona Madagascar ikipiga hela na kujijenga kiuchumi, kesho yakiibuka mengine msisite kwenda kukwapua.

Tanzania eeeeh, nchi yangu eeeh.... mwanangu kua uyaone.

2030.
 
Nimewahi kuona mtu katapeli mtu au kikundi cha watu au taasisi. Pia nimewahi kuona taasisi au kikundi cha watu kimetapeli mtu.

Katika maisha yangu sijawahi kuona nchi imetapeli nchi. Hili ni tukio la kwanza kwangu.

Hivi mratibu wa mchongo huu ni serikali au kuna ‘babu’ wa Madagascar.?
 
-Anaandika Dr.Chriss Cyrilo (MD)
____________________
Mwongozo wa wizara ya Afya nchini Tanzania unasema hadi sasa hakuna dawa ya kutibu ugonjwa wa covid19. Wakati huohuo tunaarifiwa kuwa serikali imepokea shehena ya dawa ya kukinga na kutibu covid19 kutoka Madagascar. Je serikali kupitia wizara ya afya itabadili muongozo wake, iseme kuna dawa ya kutibu covid19 kutoka Madagascar?

Ijulikane kwamba kwa mujibu wa mwongozo wa WHO na tafiti zilizofanyika hadi sasa, asilimia 80 ya wagonjwa wa Covid19 hupona wenyewe bila kuhitaji matibabu. Asilimia 20 hulazimika kupatiwa matibabu (kutokana na kuwa na magonjwa mengine). Na miongoni mwao asilimia 2 hadi 5 hufariki dunia.

Kwa lugha rahisi ni kuwa, kati ya watu 100 wanaoambukizwa virusi vya Corona, watu 80 hupona wenyewe bila kupata matibabu yoyote. Na pengine bila kuhisi dalili zozote kwamba wana maambukizi. Watu 20 waliobaki hupata dalili na huhitaji matibabu. Miongoni mwa hao 20, watu wawili hadi watano hufariki dunia.

Inawezekana wewe msomaji wa andiko hili ukawa na maambukizi ya virusi vya corona na usiwe na dalili zozote na ukapona bila kutumia dawa yoyote. Ikitolea hivyo means upo kwenye lile kundi la asilimia 80.

Tunaposisitiza umuhimu wa tafiti, ni kuepuka kusema dawa imetibu watu ambao pengine wangepona wenyewe hata bila kuhitaji dawa. Je! Dawa kutoka Madagascar inatibu wale asilimia 2-5 wanaofariki? Au inatibu wale 15% ambao hupona kwa kutibiwa magonjwa nyemelezi? Au inatibu wale 80% ambao hupona wenyewe bila kuhitaji dawa yoyote. Hakuna jibu kwa sababu hakuna utafiti uliofanyika.

Madagascar wanaendelea na tafiti, WHO wanafanya utafiti na taasisi nyingine kubwa za afya duniani zinaendelea na utafiti kuhusu dawa hiyo. Kwahiyo sisi kusema dawa hii inakinga na kutibu corona maana yake ni kwamba tupo mbele ya majira kuliko WHO na taasisi nyingine za utafiti. Infact WHO wenyewe hawaiiti dawa bali kinywaji cha mitishamba (herbal drink).
_
Kwahiyo na sisi tunaweza kuisaidia Madagascar katika utafiti wa dawa hii kupitia taasisi zetu za utafiti wa tiba kama vile NIMR, kabla ya kusema hadharani kuwa dawa hii inatibu au kukinga.!
Sio kila dawa ni lzm itambuliwe na WHO au wizara ya afya,za kienyeji utumika bila kusubiri uhakiki
 
Back
Top Bottom