Dkt. Chriss Cyrilo (MD): Mwongozo wa wizara ya Afya nchini Tanzania unasema hadi sasa hakuna dawa ya kutibu ugonjwa wa covid19.

Francis12

JF-Expert Member
Sep 30, 2016
7,533
22,276
-Anaandika Dr.Chriss Cyrilo (MD)
____________________
Mwongozo wa wizara ya Afya nchini Tanzania unasema hadi sasa hakuna dawa ya kutibu ugonjwa wa covid19. Wakati huohuo tunaarifiwa kuwa serikali imepokea shehena ya dawa ya kukinga na kutibu covid19 kutoka Madagascar. Je serikali kupitia wizara ya afya itabadili muongozo wake, iseme kuna dawa ya kutibu covid19 kutoka Madagascar?

Ijulikane kwamba kwa mujibu wa mwongozo wa WHO na tafiti zilizofanyika hadi sasa, asilimia 80 ya wagonjwa wa Covid19 hupona wenyewe bila kuhitaji matibabu. Asilimia 20 hulazimika kupatiwa matibabu (kutokana na kuwa na magonjwa mengine). Na miongoni mwao asilimia 2 hadi 5 hufariki dunia.

Kwa lugha rahisi ni kuwa, kati ya watu 100 wanaoambukizwa virusi vya Corona, watu 80 hupona wenyewe bila kupata matibabu yoyote. Na pengine bila kuhisi dalili zozote kwamba wana maambukizi. Watu 20 waliobaki hupata dalili na huhitaji matibabu. Miongoni mwa hao 20, watu wawili hadi watano hufariki dunia.

Inawezekana wewe msomaji wa andiko hili ukawa na maambukizi ya virusi vya corona na usiwe na dalili zozote na ukapona bila kutumia dawa yoyote. Ikitolea hivyo means upo kwenye lile kundi la asilimia 80.

Tunaposisitiza umuhimu wa tafiti, ni kuepuka kusema dawa imetibu watu ambao pengine wangepona wenyewe hata bila kuhitaji dawa. Je! Dawa kutoka Madagascar inatibu wale asilimia 2-5 wanaofariki? Au inatibu wale 15% ambao hupona kwa kutibiwa magonjwa nyemelezi? Au inatibu wale 80% ambao hupona wenyewe bila kuhitaji dawa yoyote. Hakuna jibu kwa sababu hakuna utafiti uliofanyika.

Madagascar wanaendelea na tafiti, WHO wanafanya utafiti na taasisi nyingine kubwa za afya duniani zinaendelea na utafiti kuhusu dawa hiyo. Kwahiyo sisi kusema dawa hii inakinga na kutibu corona maana yake ni kwamba tupo mbele ya majira kuliko WHO na taasisi nyingine za utafiti. Infact WHO wenyewe hawaiiti dawa bali kinywaji cha mitishamba (herbal drink).
_
Kwahiyo na sisi tunaweza kuisaidia Madagascar katika utafiti wa dawa hii kupitia taasisi zetu za utafiti wa tiba kama vile NIMR, kabla ya kusema hadharani kuwa dawa hii inatibu au kukinga.!
 
Tuacheni tupige nyungu..
Tupige kikombe made in Madagascar..

Tunaongozwa na wanaSIHASA...
Wataalam miongozo yenu, tutaiangalia baada ya kumaliza KUPIMA VIPIMIO VYA VIPIMIO VYA VIPIMO...ref Elizabeth na Jabir co.

Everyday is Saturday......................... :cool:
 
Dawa zikija tutatumia zisipo saidia tutaendelea kujifukiza
 
Hayo mambo ya kina doctor mwaka , wapi na wapi na MD , kwenye MD hakuna hivyo vitu.

Toka lini MTU kaenda hospital kakutwa na malaria doctor akamuandikia akatumie muarobaini .

Sent using Jamii Forums mobile app

Wewe hujawahi kumuona au kumsikia Dakatari akikwambia kula aina Fulani ya chakula. Au matunda?

Kama si alternative medicine ni nini hicho?

Tanzania kwa "wasomi" kama wewe tuna Safari ndefu sana ya kwenda.
 
Wewe hujawahi kumuona au kumsikia Dakatari akikwambia kula aina Fulani ya chakula. Au matunda?

Kama si alternative medicine ni nini hicho?

Tanzania kwa "wasomi" kama wewe tuna Safari ndefu sana ya kwenda.
Sasa ni wapi madaktari wamethibitisha kuwa hii dawa inatibu korona, tofauti na DJ Rajoelina? Sometimes tufuate wataalam hizi abracadabra haziwezi kutufikisha popote,yale ya kikombe cha babu wa Loliondo yanataka kujirudia
 
Back
Top Bottom