Dkt. Chaula: Elimu ya afya ya uzazi kwa mtoto wa kike ni muhimu

PendoLyimo

JF-Expert Member
Sep 30, 2014
879
956
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt. Zainab Chaula amesema kuwa elimu ya afya ya uzazi kwa mtoto wa kike ni muhimu kwa sababu wanatakiwa kulindwa na kukingwa na changamoto zinazowakabili katika mazingira yao ya makuzi ili waweze kutimiza ndoto zao na jamii kwa ujumla

Dkt. Chaula ameyasema hayo wakati akizindua tovuti ya Shirika lisilo la Serikali la Action Girls Foundation jijini Dodoma leo tarehe 31.08.2021 ambapo alilipongeza Shirika hilo kwa kazi nzuri ya kuwajengea msingi bora watoto wa kike ili kuepukana na changamoto mbalimbali zinazokwamisha ndoto zao ikiwemo mimba za utotoni

“Nimefurahishwa na shughuli zinazofanywa na Shirika hili za kulinda ndoto za mtoto wa kike kwasababu wanawake wengi waliofanikiwa ndoto zao pia zililindwa na watu wengine”, alizungumza Dkt. Chaula

Amesema kuwa mashirika yasiyo ya Kiserikali ni sehemu ya mafanikio ya Serikali ndio maana kuna Sheria ya Public Private Parternership (PPP), hivyo mashirika haya pamoja na asasi za kiraia kwa kushirikiana na Serikali yanafanya kazi kubwa ya kutoa elimu ya afya ya uzazi na haki za mtoto wa kike ili kuwajengea uwezo wa kujitambua na kutimiza ndoto zao

Dkt. Chaula amezungumzia msingi wa msichana bora unaanzia katika makuzi kulingana na jamii inayomzunguka na Serikali inatoa chachu ya mafanikio kwa kutengeneza Sera kanuni taratibu sheria na miongozo zinazoelekeza ni namna gani ya kumlinda msichana huyu dhidi ya mazingira hatarishi ambayo yanaweza kuzima ndoto za mtoto wa kike

Ameongeza kuwa ili kufikia mafanikio hakuna njia ya mkato na mtoto wa kike ana nguvu ya kujenga au kubomoa taswira yake kwa muonekano, mazungumzo na matendo yake mwenyewe

Naye Mkurugenzi wa Huduma za Afya na Lishe wa TAMISEMI, Dkt. Ntuli Kapologwe ambaye pia ni Mjumbe wa Bodi ya Shirika hilo amesema kuwa Shirika hilo ni wadau wakubwa wa Serikali katika kuhakikisha wanapambana na mimba za utotoni na kumfanya mtoto wa kike ajitambue na kuweza kujali thamani yake kuwa na mchango wao kwa Taifa

Amesema kuwa taasisi hiyo imekuwa ikishirikiana na Ofisi ya Rais TAMISEMI pamoja na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto katika kuhakikisha kuwa wanaweza kuinua thamani ya mtoto wa kike na kusaidia mapambano dhidi ya changamoto zinazomkabili mtoto wa kike

Amesema kuwa Serikali pekee haiwezi kuyafikia maeneo yote bila ushiriki wa asasi za kiraia na taasisi zisizo za Serikali ambapo kwa upande wa Serikali inatoa ushirikiano wa kutosha ili kufikia malengo yaliyowekwa ya kitaifa na kimataifa

Kwa upande wa Mkurugenzi wa Shirika lisilo la Kiserikali la Action Girls Foundation, Bi Rabia Saad amezungumzia shirika hilo kuwa linafanya kazi ya kukuza uelewa wa wasichana juu ya afya ya uzazi na haki ambapo programu zao zinawafikia wasichana walio ndani na nje ya shule kwa kukuza uelewa wao juu ya afya ya uzazi, jinsia na hedhi salama kwa kutoa taulo za kike kwa wanafunzi wenye uhitaji.

Ameongeza kuwa hadi sasa Shirika hilo limeshawafikia zaidi ya vijana 1500 kupitia klabu za afya za shule za sekondari katika wilaya ya Mpwapwa Mkoani Dodoma na uwajengea uwezo wanafunzi, walimu walezi wa klabu, wazazi na kushirikisha watoa huduma za afya katika kufikisha elimu ya afya ya uzazi kwa vijana hao.

Mkurugenzi huyo ameseme kuwa katika kipindi cha miaka 2 ya Shirika hilo limeshirikisha waelimishaji rika takriban 300 nje ya shule, ambao wamefundishwa juu ya VVU / UKIMWI na hatua za kuzuia ukatili wa kijinsia kwa kushirikiana na wadau mbalimbali pamoja na Wizara ya Afya ambapo kampeni za uhamasishaji walizozifanya zimefikia zaidi ya watu 500,000 katika mkoa wa Dodoma kupitia vipindi vya redio za hapa.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari
 
Hivi huyu Katibu ni Dokta PhD? Au dokta wa mifugo au binadamu. Najaribu kuona kama mawasiliano na udaktari wa viumbe vinashabihiana. Maana wizara aliyopo ni ya kitaalam sana. Isije kuwa kawekwa wizara isiyoendana na ujuzi wake. Katibu Mkuu ni nafasi ya weledi sana.
 
Ni daktari wa binadamu kama alivyo Waziri wa Wizara hiyo Ndugu Ndugulile

Naibu Katibu Mkuu pekee pale Dr Yonazi ndio Mtaalam wa Mawasiliano

Nawasalimu wote kwa jina la TANZANIA
 
Itakuwa mawasiliano ya Akili na Mwili wa mwanadamu
Nimefuatilia CV yake kumbe ni daktari wa binadamu, sasa najiuliza daktari wa binadamu na masuala complex ya TEHAMA wapi na wapi..

.huyu mama angepelekwa kuwa Katibu Mkuu Afya au TAMISEMI awe ana deal na afya za wananchi hapo wizara ya TEHAMA awekwe mtaalam wa TEHAMA ili tukimbie TEHAMA ndo kila kitu.

sasa kumweka mtu ambae hilo si eneo lake inakuwa vigumu kushauri ipasavyo na kuunda sera latest.

Tujifunze kwa wenzetu Rwanda
 
Ni daktari wa binadamu kama alivyo Waziri wa Wizara hiyo Ndugu Ndugulile

Naibu Katibu Mkuu pekee pale Dr Yonazi ndio Mtaalam wa Mawasiliano

Nawasalimu wote kwa jina la TANZANIA
Ingefaa sana Mheshimiwa Rais afikirie kupangua hii wizara ya TEHAMA awaweke manguli wa TEHAMA kuanzia Minister na Katibu Mkuu kuweka watu wasiopaswa wanapoliticise TEHAMA badala ya kuleta utaalamu ukimweka hapo nafasi ya Katibu Mkuu wizara ya TEHAMA mtaalam wa TEHAMA kama DG wa TCRA nk utaona mambo yatavokuwa mubashara.
 
Nimefuatilia CV yake kumbe ni daktari wa binadamu sasa najiuliza daktari wa binadamu na masuala complex ya TEHAMA wapi na wapi..

.huyu mama angepelekwa kuwa Katibu Mkuu Afya au TAMISEMI awe ana deal na afya za wananchi hapo wizara ya TEHAMA awekwe mtaalam wa TEHAMA ili tukimbie TEHAMA ndo kila kitu.

sasa kumweka mtu ambae hilo si eneo lake inakuwa vigumu kushauri ipasavyo na kuunda sera latest.

Tujifunze kwa wenzetu Rwanda

Huyo mama before hajaenda huko mawasiliano alikua Afya kipindi kile cha corona ndo inapamba moto huyu mama alisimamia professionalism JIWE akamtoa Afya akampeleka mawasiliano. JIWE alimpenda huyu mama kibinafsi ndo maana hakumtumbua Kama Ndumgulile ila akambadilishia tu wizard. Inasemekana ndiye aliyemwokoa JIWE katika saga la ile sumu Dodoma.
 
Saga la sumu?
 
Back
Top Bottom