Dkt. Benson Bagonza: Wakati wa Mwalimu ukimsifia anakushusha cheo. Enzi hizi ukisifia unapandishwa cheo

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
21,271
47,271
Alikuwa akihojiwa na Maulid Kitenge kuhusu kusifia kila kitu yeye akasema, hajui kutaga yai lakini yai bovu analijua, ‘mimi kama kiongozi wa dini wajibu wangu ni kuangalia wapi panahitaji kunyooshwa sio wapi panahitaji kusifia, wakati wa Mwalimu ukimsifia anaku- demote siku hizi ukisifia sifia unapandishwa’.

Kwamba aliyebuni "zidumu fikra za mwenyekiti wa chama" alishushwa cheo! Au hii si fikra bali ombi?
====
Kwa kweli siwezi kusifia kwa unafiki maana ninahisi nitastukiwa.
 
Hawa wapenda kusifiwa na Machawa wameua CCM ya Nyerere imekua, Chama maiti.
Punzika Kwa Amani Mwlimu , CHADEMA tutairudisha nchi kwenye mwelekeo ulio sahihi.
 
Kwamba aliyebuni "zidumu fikra za mwenyekiti wa chama" alishushwa cheo! Au hii si fikra bali ombi?
====
Kwa kweli siwezi kusifia kwa unafiki maana ninahisi nitastukiwa.
Aliye buni hilo neno zidumu fikra sahihi za mwenyekiti wa chama.

Alikuwa sahihi maana kipindi hicho chama ndiyo kilikuwa ndiyo kinashika hatamu.

Leo hii ni tofauti kabisa maana tupo kwenye mfumo wa vyama vingi.

Ndiyo maana hata serikali ya zanzibar ina mchanganyiko wa viongozi .
Wengine wanatoka vyama vya upinzani na wengine wa ccm wote wapo kwenye baraza la mawaziri.
 
Magufuli hakupenda kusifiwa ila kusifikiwa ni huyu sijui mnamwita Hangaya.

Magufuli yeye alikuwa analazimisha asujudiwe kama Mungu kazi ambayo hata viongozi wa dini walikuwa wakimfanyia.

Ccm ina watu wa hovyo sana. Very useless people masquerading as leaders.
 
Kuna sifa zingine mtu akikusifia mkate vibao, kama Bananga alivyoropoka kwa Rais alitakiwa awe ameswekwa ndani na kuhojiwa,ila kwa kuwa ndio tunayoyapenda kuyasikia basi tunachekelea tu
 
Siwamekopi kwa lile jendawazimu liendazake lililkua likisifiwa tu unalamba kitengo aliyejaribu kumkosoa tu alikula shaba na kutupwa baharini akiwa kwenye kiroba, kuna dhambi kubwa sana inawatafuna watawala wa taifa hili ni muda tu utaamua
 
Back
Top Bottom