DKT BASHIRU ZIARANI MOROGORO

SautiYaMnyonge

JF-Expert Member
May 13, 2018
439
742
Na Mwandishi Wetu

Katibu Mkuu wa CCM Dk Bashiru Ali Kakurwa leo 9 Februari, 2019 amefanya ziara kikazi ya siku moja mkoani Morogoro ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 42 ya kuzaliwa kwa Chama Cham Mapinduzi

Katika kata ya Msowero wilaya ya Kilosa Katibu Mkuu Bashiru alishiriki ujenzi wa Taifa zahati ya Msowero katika jengo la kujifungulia wakinamama wajawazito linalojengwa kwa nguvu za wananchi.

Baadae alipata nafasi ya kuwatembelea wagonjwa majumbani kuwasalimia na kuwatakia afya njema nawapone haraka ili kuungana katika ujenzi wa Taifa.

Aidha Katibu Mkuu Bashiru alipata nafasi ya kuzungumza na viongozi wa chama na Serikali katika viwanja shule ya Msingi Tame ambapo pia alisikiliza changamoto mbali mbali zinazowahusu wananchi wa wilaya ya Kilosa.

" Kazi Ni Kipimo cha Utu,Chapa Kazi Tulinde Uhuru na Utaifa Wetu"
Miaka 42 ya Kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi

#MorogoroYaKijaniInawezekana #TuwePamoja #TusikubaliKugawanyika
IMG-20190209-WA0072.jpeg
IMG-20190209-WA0064.jpeg
IMG-20190209-WA0063.jpeg
IMG-20190209-WA0062.jpeg
IMG-20190209-WA0066.jpeg
IMG-20190209-WA0068.jpeg
IMG-20190209-WA0074.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni unafiki mtupu. Kama wangekuwa na dhamira njema wasingewazuia viongosi wengine wandamizi kufanya yale ambayo nao wanaona ni muhimu.

Hakuna kiongozi wa CCM anayefanya jambo lolote kwa dhamira njema. Wamejaa unafiki na siasa za hadaa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni unafiki mtupu. Kama wangekuwa na dhamira njema wasingewazuia viongosi wengine wandamizi kufanya yale ambayo nao wanaona ni muhimu.

Hakuna kiongozi wa CCM anayefanya jambo lolote kwa dhamira njema. Wamejaa unafiki na siasa za hadaa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Unafiki uliotukuka nauona pale kutembelea wagonjwa majumbani. Alitumia vigezo gani na aliwatembelea wangapi? Sasa hivi kwasababu uchaguzi wa serikali za mitaa umekaribia ndio wanajifanya wakarimu. Wanatuharibia chama hawa. Wafanye vitu sahihi lakini siyo ulaghai.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom