Dkt Bashiru: Wanawake jitokezeni kugombea nafasi za uongozi

Egnecious

JF-Expert Member
Jul 8, 2015
875
960
DKT. BASHIRU: WANAWAKE JITOKEZENI KUGOMBEA NAFASI ZA UONGOZI


Leo tarehe 11 Oktoba, 2019 Dkt. Bashiru Ally Katibu Mkuu wa CCM ameanza ziara ya siku mbili mkoa wa Lindi, ambapo amewataka wanawake kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi za uongozi katika uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika mwezi Novemba, 2019.

Ameyasema hayo alipowasili wilaya ya Kilwa ambapo amepokewa na wanachama wa CCM, Viongozi wa Chama na Serikali na kumuongoza kufungua shina la wakereketwa Tawi la Sinza katika kata ya Miteja.

"Tuchague viongozi wenye sifa za uongozi zinazofanana na Rais na Mwenyekiti wa CCM Ndg. John Pombe Joseph Magufuli za uchapakazi na uwajibikazi wa haki".

"Wapo wanawake wanaobaguliwa na kutishwa wanapotaka kugombea nafasi za uongozi, hilo kwenye Chama chetu tunalikemea na tunawataka wanawake wengi wenye sifa wagombee nafasi za uongozi kwa sababu CCM inaamini usawa wa binadamu". Dkt. Bashiru amesisitiza.

Pia amewakumbusha wanachama wa CCM na wananchi wote, waendelee kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika daftari la wapiga kura linaloendelea kuanzia tarehe 8-14 Oktoba, 2019.

Imetolewa na;
CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)
MAKAO MAKUU DODOMA.
IMG_20191011_174722_569.jpeg
IMG_20191011_174722_568.jpeg
 
Back
Top Bottom