Dkt Bashiru: Uchaguzi sio namba uchaguzi ni uamuzi wa umma

Egnecious

JF-Expert Member
Jul 8, 2015
875
960
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Bashiru Ally amewakumbusha baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa nchini maana halisi ya uchaguzi ni maamuzi ya Umma si kama ambavyo wamekuwa wakieleza kwa kupotosha kuwa, uchaguzi ni namba.

Ameyasema hayo tarehe 13 Januari, 2020 alipokuwa akihutubia viongozi wa mashina,matawi, Kata na wajumbe wa Halmashauri Kuu ya wilaya za Handeni na Kilindi Mkoani Tanga.

“Nimewasikia baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa, wanasema uchaguzi ni namba. Uchaguzi sio namba, uchaguzi ni uamuzi wa umma, namba ni kitu cha baadae, waambieni wanaosema uchaguzi ni namba waache kugeuza uchaguzi kama mchezo wa kamari au bingo, uchaguzi ni uamuzi wa wananchi juu ya mustakabali wao.”

Amesisitiza zaidi kuwa, wananchi hufanya hivyo kabla ya siku ya kupiga kura, siku ya kupiga kura ndio siku ya kudhihirisha uamuzi wao, lakini uamuzi wao huanza kufanyika tangu uchaguzi ulipoisha.

Hivyo Katibu Mkuu ameeeleza kuwa, CCM inauona uchaguzi kama zoezi muhimu sana linalohusu uamuzi wa wananchi juu ya mustakabali wa taifa lao, uamuzi wa wananchi juu ya wananchi wenzao wanaofaa kuwaongoza kwa maendeleo yao, uamuzi wa wananchi juu ya chama chenye sifa, kinachoaminika, kinachoweza, chenye rekodi ya kuongoza nchi na sio vinginevyo.

Wakati huo huo Dkt. Bashiru amewahakikishia wananchi msimamo wa CCM kuendelea kuisimamia serikali kutekeleza kila kilichoahidiwa na kisichotekelezwa huelezwa ni kwa nini hakijatekelezwa, hivyo mwaka huu ni mwaka wa wanaCCM wote kuueleza umma yote yalioahidiwa yametekelezwa kwa kiasi gani, yepi yametekelezwa vizuri, yepi yametekelezwa kwa wastani na yepi ambayo Chama kitaongeza nguvu zaidi.

Aidha Katibu Mkuu ametumia mkutano huo wa ndani kuwataka wenyeviti wa Vijiji na Mitaa, watendaji wa mitaa na Halmashauri, kuwa wabunifu na kung’amua fursa za maendeleo, na kwa wakuu wa mikoa na wilaya kusimamia ubunifu kwa watendaji ili kuwawezesha wananchi kupiga hatua kwa haraka.

Viongozi mbalimbali wakizungumza kabla ya kumkaribisha Katibu Mkuu, wameonesha kuridhishwa na kasi kubwa ya utekelezaji wa Ilani ya CCM licha ya changamoto mbalimbali ambazo wanaendelea kuzishughulikia na kuzitafutia majawabu ikiwa ni pamoja na kasi ya usambazaji wa umeme vijijini.

Mkutano huo umehudhuriwa na wanachama, viongozi wa Chama na Serikali wakiongozwa na Kaimu Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga Ndg. Mohamed Salim Ratco (MNEC), Mkuu wa Mkoa wa Tanga Ndg. Martin Shigela, wajumbe wengine wa Halmashauri Kuu Bi. Mwantumu Zodo, na Bi. Catherine Kitandura na wabunge wa Mkoa wa Tanga.

Katibu Mkuu yupo Mkoani Tanga kwa ziara ya kikazi ya siku nne, ambapo ziara hiyo imelenga kuimarisha na kuhuisha uhai wa Chama katika ngazi za Mashina na Matawi.

Imetolewa na;
Said Said Nguya
Afisa Habari
Ofisi ya Katibu Mkuu
Chama Cha Mapinduzi (CCM)

IMG-20200113-WA0063.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukihamia ccm na kuvishwa miguo ya kijani
Unapotea nakupoteza kila kitu kichwani
Alifundisha tofauti na yale anayoyafanya kwa vitendo. Sio yule wa Udsm tena huyu kwasasa hana tofauti na kibajaji, nikama Asumpta nk.

..hivi Dr. Al Bashiri haoni AIBU kufanya mikutano huku wenzake wa vyama vya upinzani wamezuiliwa?

.
 
Ukihamia ccm na kuvishwa miguo ya kijani
Unapotea nakupoteza kila kitu kichwani
Alifundisha tofauti na yale anayoyafanya kwa vitendo. Sio yule wa Udsm tena huyu kwasasa hana tofauti na kibajaji, nikama Asumpta nk.

..halafu hana lolote la maana analozungumza.

..ukisikiliza hotuba zake ni sawa na mtu asiyekuwa na kazi, mzururaji.
 
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Bashiru Ally amewakumbusha baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa nchini maana halisi ya uchaguzi ni maamuzi ya Umma si kama ambavyo wamekuwa wakieleza kwa kupotosha kuwa, uchaguzi ni namba.

Ameyasema hayo tarehe 13 Januari, 2020 alipokuwa akihutubia viongozi wa mashina,matawi, Kata na wajumbe wa Halmashauri Kuu ya wilaya za Handeni na Kilindi Mkoani Tanga.

“Nimewasikia baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa, wanasema uchaguzi ni namba. Uchaguzi sio namba, uchaguzi ni uamuzi wa umma, namba ni kitu cha baadae, waambieni wanaosema uchaguzi ni namba waache kugeuza uchaguzi kama mchezo wa kamari au bingo, uchaguzi ni uamuzi wa wananchi juu ya mustakabali wao.”

Amesisitiza zaidi kuwa, wananchi hufanya hivyo kabla ya siku ya kupiga kura, siku ya kupiga kura ndio siku ya kudhihirisha uamuzi wao, lakini uamuzi wao huanza kufanyika tangu uchaguzi ulipoisha.

Hivyo Katibu Mkuu ameeeleza kuwa, CCM inauona uchaguzi kama zoezi muhimu sana linalohusu uamuzi wa wananchi juu ya mustakabali wa taifa lao, uamuzi wa wananchi juu ya wananchi wenzao wanaofaa kuwaongoza kwa maendeleo yao, uamuzi wa wananchi juu ya chama chenye sifa, kinachoaminika, kinachoweza, chenye rekodi ya kuongoza nchi na sio vinginevyo.

Wakati huo huo Dkt. Bashiru amewahakikishia wananchi msimamo wa CCM kuendelea kuisimamia serikali kutekeleza kila kilichoahidiwa na kisichotekelezwa huelezwa ni kwa nini hakijatekelezwa, hivyo mwaka huu ni mwaka wa wanaCCM wote kuueleza umma yote yalioahidiwa yametekelezwa kwa kiasi gani, yepi yametekelezwa vizuri, yepi yametekelezwa kwa wastani na yepi ambayo Chama kitaongeza nguvu zaidi.

Aidha Katibu Mkuu ametumia mkutano huo wa ndani kuwataka wenyeviti wa Vijiji na Mitaa, watendaji wa mitaa na Halmashauri, kuwa wabunifu na kung’amua fursa za maendeleo, na kwa wakuu wa mikoa na wilaya kusimamia ubunifu kwa watendaji ili kuwawezesha wananchi kupiga hatua kwa haraka.

Viongozi mbalimbali wakizungumza kabla ya kumkaribisha Katibu Mkuu, wameonesha kuridhishwa na kasi kubwa ya utekelezaji wa Ilani ya CCM licha ya changamoto mbalimbali ambazo wanaendelea kuzishughulikia na kuzitafutia majawabu ikiwa ni pamoja na kasi ya usambazaji wa umeme vijijini.

Mkutano huo umehudhuriwa na wanachama, viongozi wa Chama na Serikali wakiongozwa na Kaimu Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga Ndg. Mohamed Salim Ratco (MNEC), Mkuu wa Mkoa wa Tanga Ndg. Martin Shigela, wajumbe wengine wa Halmashauri Kuu Bi. Mwantumu Zodo, na Bi. Catherine Kitandura na wabunge wa Mkoa wa Tanga.

Katibu Mkuu yupo Mkoani Tanga kwa ziara ya kikazi ya siku nne, ambapo ziara hiyo imelenga kuimarisha na kuhuisha uhai wa Chama katika ngazi za Mashina na Matawi.

Imetolewa na;
Said Said Nguya
Afisa Habari
Ofisi ya Katibu Mkuu
Chama Cha Mapinduzi (CCM)

View attachment 1322675

Sent using Jamii Forums mobile app
Sijawahi kuzielewa kauli zake tangia awe KM
 
Upuuzi tu. Hamna lolote la maana analoongea.
Sijui kwanini? Taking yourself too seriously while other people don't.
 
..halafu hana lolote la maana analozungumza.

..ukisikiliza hotuba zake ni sawa na mtu asiyekuwa na kazi, mzururaji.

Polepole
.....uchaguzi ukiwa haki na huru ccm ijiandaye kukabidhi madaraka

.......alipigania sana katiba mpya ya Jaji warioba na tume huru ya uchaguzi ( baada ya kuingia ccm kama sio yeye anafanya madudu ya kutisha)

Nape
..... ccm itashinda kwa vyovyote hata kwa bao la mkono ( baada ya kuchomolewa uwazir, akili zimemrudi....majuto nimjukuu)

Makamba
.....kikwete aliwabatiza kwa maji, Huyu atawabatiza kwa moto ( sasa anabatizwa yeye senior na junior wake kwa moto. Akili zinamrudia)

Bashiru
Alifundisha haki, alihubiri mahitaji ya katiba bora alifundisha utii wa sheria nk (ameingizwa huko chamani ccm nakulambishwa Asali, kasahau yote..... Siku anatolewa/anaacha madaraka ya uccm atakumbuka maana Mungu atamrejeshea akili zake sahihi)
Na wengineo wengi ndani ya ccm

CCM nijinamizi linabadilisha akili bora za watu kuwa za hovyohovyo
 
Sasa kama sio numbers mbona mnapeleka majahazi yaliyojaa watu usiku usiku

Dr. ulienda kusomea upikaji wa Togwa?!
 
Back
Top Bottom