Election 2020 Dkt. Bashiru: Tutalirejesha jimbo la Kigoma Mjini mikononi mwa CCM kwa gharama zozote

PavelJr

Member
Joined
Jan 15, 2020
Messages
18
Points
75

PavelJr

Member
Joined Jan 15, 2020
18 75
Dr bashiru aahaidi kumtoa madarakani Zitto Kabwe


======
Katibu Mkuu wa CCM, Dk Bashiru Ally amesema chama hicho tawala nchini Tanzania kinajipanga kuibuka na ushindi wa ubunge katika jimbo la Kigoma Mjini linaloongozwa na Zitto Kabwe (ACT-Wazalendo).

Mwaka 2010 hadi 2015 mbunge wa Kigoma Mjini alikuwa Peter Serukamba wa CCM ambaye katika uchaguzi wa mwaka 2015 alikwenda kugombea jimbo la Kigoma Kaskazini huku Zitto ambaye alikuwa mbunge wa jimbo hilo akienda kugombea Kigoma Mjini.

Katika maelezo yake, Dk Bashiru amesema wapo tayari kulirejesha jimbo hilo mikononi mwa CCM kwa gharama zozote katika uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika Oktoba, 2020.

Akizungumza leo Jumapili Januari 19, 2020 manispaa ya Kigoma Ujiji katika mkutano na wanachama wa CCM na kugawa vitambulisho kwa mabalozi, Dk Bashiru amesema jimbo hilo kwa muda mrefu limekuwa mikononi mwa wapinzani.

"Sababu tunayo, nia tunayo na malengo tunayo hakuna atakayeweza kuturudisha nyuma kwa kasi yetu tunayoendana nayo," amesema Dk Bashiru.

Amesema Serikali imefanya mambo mbalimbali ya maendeleo na wananchi wanajua, kwamba hawawezi kuwachagua tena wapinzani.
 

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Messages
33,366
Points
2,000

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined Sep 22, 2008
33,366 2,000
Katika maelezo yake, Dk Bashiru amesema wapo tayari kulirejesha jimbo hilo mikononi mwa CCM kwa gharama zozote katika uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika Oktoba, 2020.
Kwanza naunga mkono chama chochote kudhamiria kulitwaa jimbo lolote, kwasababu hakuna jimbo lolote ni mali ya mtu yoyote au lina hati miliki ya chama chochote, hivyo Katibu Mkuu wa CCM Dr. Bashiru Ali yuko right.

Katika mazingira ya sasa ya siasa zetu, yaani the political landscape of Tanzania as of now, kwa uchaguzi Mkuu wa 2020, kama kuna Mbunge mmoja wa upinzani mwenye uhakika wa kurejea Bungeni, kwa maoni yangu ni ZZK pekee, kama Zitto asipokuwa ndie mgombea wa urais wa Umoja wa upinzani, then ni Zitto tuu pekee ndie mpinzani pekee mwenye matumaini ya kurejea Bungeni kwa tiketi ya upinzani, kwenda kuiongoza kambi ya upinzani yenye wabunge wengi wa ACT kutoka Pemba na yale majimbo mawili ya Zanzibar.

Sasa kama CCM imepania kumng'oa Zitto, hii maana yake kwa huku bara Bunge lijalo lote litakuwa ni Bunge la CCM predominantly, something which is not good kwa mustakabali na majaaliwa ya Bunge la vyama vingi katika kuisimamia serikali.

Ombi langu kwa CCM, kama ni kulitwaa jimbo la Kigoma mjini, Moshi Mjini, Mbeya, Iringa na Arusha mjini, CCM iyatwae kwa siasa safi na sio kwa kutumia mbinu za hooks and crooks ikiwemo bao la mkono, mbinu hizi huwa hazina matokeo chanya kwa watu waliojitambua.

P
 

Forum statistics

Threads 1,391,984
Members 528,518
Posts 34,094,891
Top