Dkt. Bashiru: Tundu Lissu anaumwa 'Ugonjwa wa Deko'

Etwege

JF-Expert Member
Jul 4, 2018
2,222
2,000
Katibu mkuu wa CCM Dkt Bashiru Ally akiwa ziarani Morogoro ametaja ugonjwa unaomsumbua Tundu Lisu kuwa ni deko .
Dalili za ugonjwa wa deko ni zarau ,majivuno ,kuota kuwa rais wa Tanzania ,kulialia, na kujikomba kwa wazungu.

Sababu ya ugonjwa wa deko ni malezi mabaya ya utotoni na inaonekana Lisu amelelewa kimayaimayai sana, ndiyo maana anadeka mpaka jitu zima la uzeeni.
------

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Bashiru Ally, amesema Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (CHADEMA), anaumwa ugonjwa wa deko huku akimuomba Rais Dkt. John Magufuli aanze kutibu ugonjwa huo.

Kauli hiyo aliitoa juzi wilayani Kilosa mkoani Morogoro, katika ziara yake ya kazi ikiwa ni sehemu ya maadhimino ya miaka 42 ya kuzaliwa kwa CCM.

Dk. Bashiru alidai Lissu amekuwa akisema uongo katika nchi za Ulaya huku akiota siku moja atakuwa Rais wa Tanzania.

Wakati mtendaji huo wa juu wa CCM akiyasema hayo, Lissu amekuwa akiendelea na ziara yake katika nchi za Ulaya.

Kwa sasa yupo Marekani akieleza kile alichodai hali ya demokrasia nchini na kupigwa kwake risasi.

Dkt. Bashiru alidai dalili za ugonjwa wa aina ya Tundu Lissu ni kusema uongo, dharau, deko, uonevu, kiburi, majivuno.

“Ila shukrani ya punda ni mateke. Namuomba Rais wetu (Dkt. John Magufuli) aanze kutibu ugonjwa wa deko unasomesha watu wanazunguka kutukana nchi yao na Rais wao kisa ugonjwa wa deko.

“Yupo msomi mmoja anaitwa Tundu Lissu ameugua ugonjwa wa deko, anadeka hajui jembe kwa maisha yake, hajui mpunga unalimwaje wala samaki wanavuliwaje.

“Hajapanda bodaboda muda mrefu na watoto wake hawasomi shule hizi anazunguka dunia nzima kutuchafua.

“Tunao Tundu Lissu wengi Serikalini tumewaamini tumewapa dhamana ila ukiwatembelea ofisini wanadeka, mara nyingine hawapo, wanajipendelea wao,” alisema Dkt. Bashiru na kuongeza:

“Ugonjwa huu unaambukizwa na tumeulea na wauguzi na madaktari wa ugonjwa huu ni Watanzania nyie wenyewe. Huu ugonjwa hatari, unaambukizwa ni hatari kuliko Ukimwi.

Anasema tumeweka Kifungu kwenye Katiba ya CCM cha kuzuia watu kugombea urais siyo kweli ni uongo”.

Dkt. Bashiru alisema dalili za ugonjwa huo wa deko ni ubinafsi, kuota urais wa Tanzania kuwa na kiburi na kwenda Ulaya kuzungumza lugha za wakoloni lakini sasa anayemwita dikteta amefuta mashamba kwa ajili ya wanyonge.

“Nilipomskiliza nikasema ni muongo na kwa sababu anaumwa ugonjwa unaitwa Tundu Lissu, basi yupo kwenye hali mbaya.

“Ugonjwa wa Tundu Lissu ni hatari ila unaponyeka, amuache Rais (Dkt. John Magufuli) atumikie wanyonge.

“Watendaji wote wa serikali ambao hawataki kupona ugonjwa huu watafute serikali nyingine, ajira ni hiyari waandike barua waseme chama hiki hakipendi dhurlma, mimi nadhulumu, hakipendi uongo mimi muongo, uachie madaraka,” alisema.

For the English Audience
The Secretary-General of the Ruling Party (CCM), Dr. Bashiru Ally, said Singida East MP Tundu Lissu (Chadema), suffers from "childish behavior" while urging President Dr. John Magufuli to start treating the disease.

The statement was made yesterday in Kilosa district in Morogoro, on his official visit as part of the celebration of CCM's 42nd birthday.

Dr. Bashiru claimed Lissu had been lying in European countries while dreaming he would one day become President of Tanzania.

While the CCM executive said this, Lissu has been continuing his tour in European and American countries. He is currently in the United States explaining what he claimed for democracy in the country and his shooting.

Dr. Bashiru claimed that the symptoms of the "Lissu syndrome" are lying, scorn, malice, bullying, pride, arrogance. He says we have put a clause in the CCM Constitution to prevent people from running for president.

Dr. Bashiru said the symptoms of the plague were selfish, dreaming of the presidency of Tanzania being proud and going to Europe to speak the colonial languages but now the so-called dictator has cleared the fields for the weak.

zipompa

JF-Expert Member
Aug 19, 2014
6,052
2,000
huyu dr. bashiru na dr. mollel wana mtindio wa ubongo hata sura zaonesha hivyo

mtu mzima kuongea mambo ya kitoto ni kukaribisha kudharauliwa na kupuuzwa

kama humfahamu dr. bashiru ukisoma hayo maneno unaeza hisi ni msanii kama mhogo mchungu ama bambo ukija ambiwa ni katibu wa chama kikubwa unashikwa na mshangao
 
Ndikwega

JF-Expert Member
Feb 1, 2012
5,863
2,000
Katibu mkuu wa CCM Dkt Bashiru Ally akiwa ziarani Morogoro ametaja ugonjwa unaomsumbua Tundu Lisu kuwa ni deko .
Dalili za ugonjwa wa deko ni zarau ,majivuno ,kuota kuwa rais wa Tanzania ,kulialia, ushoga na kujikomba kwa wazungu.

Sababu ya ugonjwa wa deko ni malezi mabaya ya utotoni na inaonekana Lisu amelelewa kimayaimayai sana, ndiyo maana anadeka mpaka jitu zima la uzeeni.

Katibu Mkuu CCM: Tundu Lissu Anaumwa Ugonjwa wa Deko na Kiburi | MPEKUZI

Sent using Jamii Forums mobile app
Mbona hizo Sifa ni Kama Zote anazo yeye Bashiru! Kweli DAB and her Company wameshikwa Pabaya na Mwanaume Survivor yoka Singida. TL hivyo hivyo, maana Tanzania kwasasa limegeuka Taifa linaloongozwa na Mashetani!
 
Etwege

JF-Expert Member
Jul 4, 2018
2,222
2,000
huyu dr. bashiru na dr. mollel wana mtindio wa ubongo hata sura zaonesha hivyo

mtu mzima kuongea mambo ya kitoto ni kukaribisha kudharauliwa na kupuuzwa

kama humfahamu dr. bashiru ukisoma hayo maneno unaeza hisi ni msanii kama mhogo mchungu ama bambo ukija ambiwa ni katibu wa chama kikubwa unashikwa na mshangao
Jikite kwenye hoja

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hawachi

JF-Expert Member
Nov 25, 2018
12,120
2,000
Katibu mkuu wa CCM Dkt Bashiru Ally akiwa ziarani Morogoro ametaja ugonjwa unaomsumbua Tundu Lisu kuwa ni deko .
Dalili za ugonjwa wa deko ni zarau ,majivuno ,kuota kuwa rais wa Tanzania ,kulialia, ushoga na kujikomba kwa wazungu.

Sababu ya ugonjwa wa deko ni malezi mabaya ya utotoni na inaonekana Lisu amelelewa kimayaimayai sana, ndiyo maana anadeka mpaka jitu zima la uzeeni.

Katibu Mkuu CCM: Tundu Lissu Anaumwa Ugonjwa wa Deko na Kiburi | MPEKUZI

Sent using Jamii Forums mobile app
Huyu Batuli ilibidi awe mirembe sema ccm yote hakuna mzima.
 
chaliifrancisco

JF-Expert Member
Jan 17, 2015
13,471
2,000
Yani ukitaka ujue jinsi Lissu anavyo wafanya wabaya wote waweweseke na kuota ndoto huku wakitembea angalia tu idadi ya nyuzi wanazoanzisha kwa siku.

Yani asubuhi hii tu nimeshaona nyuzi sio chini ya kumi mpya za Lissu. Inaonekana dawa imepenya vizuri mpaka kwenye bone marrow 😂

Mwaka huu tutaona na kusikia mengi sana na hapa ndio kwanza dose imeanza tayari watu washalewa dawa.

💉💉💉💊💊💊
 
Mr. Zero

JF-Expert Member
Jun 5, 2007
12,129
2,000
Katibu mkuu wa CCM Dkt Bashiru Ally akiwa ziarani Morogoro ametaja ugonjwa unaomsumbua Tundu Lisu kuwa ni deko .
Dalili za ugonjwa wa deko ni zarau ,majivuno ,kuota kuwa rais wa Tanzania ,kulialia, ushoga na kujikomba kwa wazungu.

Sababu ya ugonjwa wa deko ni malezi mabaya ya utotoni na inaonekana Lisu amelelewa kimayaimayai sana, ndiyo maana anadeka mpaka jitu zima la uzeeni.

Katibu Mkuu CCM: Tundu Lissu Anaumwa Ugonjwa wa Deko na Kiburi | MPEKUZI

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa design Hii ya viongozi.... Hivi Tanzania tuna laana gani au tumemkosea nini Mungu.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom