mwanamwana
JF-Expert Member
- Aug 1, 2011
- 1,076
- 4,113
Katibu Mkuu wa CCM, Dkt. Bashiru Ally Kakurwa akiwa Chato wakati wa kuwanadi wagombea wa CCM ameonya kwamba kuna wazushi wanasema kwamba CCM inatafuta viti vingi vya Ubunge ili wakiingia Bungeni wabadili Katiba ili Rais Magufuli aongezewe muda.
Ameongeza kwamba Rais Magufuli anaomba miaka mitano mingine na muda wake ukiisha basi hataongeza hata sekunde moja ya Utawala.
Dkt. Bashiru amesema:
"Mgombea wetu wa Urais Dkt. Magufuli anaomba kura kwa ajili ya kipindi chake cha pili, akimaliza hapo hataongeza hata sekunde. Uvumi kwamba kupitia wingi wa wabunge wa CCM atabadilisha Katiba ili aendelee kuongoza, ni uongo. Upuuzeni"