Dkt. Bashiru: Nina barua za wabunge wa upinzani wanaotaka kuhamia CCM. Wapinzani wamekimbia siyo kujitoa

Dkt Bashiru, ifike wakati ueleze mikakati ya chama chetu kuelekeza serikali kuongeza juhudi kwenye kuvutia wawekezaji wa ndani na nje kwenye viwanda, kilimo, mikopo nafuu kwa vijana nk hao wakina Mollel nakadhalika tuliowachukua wametupa faida gani? Siasa nyepesi tuwaachie wale class seven wenzangu Msukuma, Lusinde n.k
 
Shigganza,

Hakika kati ya watu ambao wameharibu credibility yake mapema ni Bashiru Ally!

Niwe mkweli Mimi tangu enzi anajionesha pale Nkrumah 1998/99 akijiita Rais wa Off Campus moyo wangu ulimkataa, nilimwona kama mchumia tumbo fulani!

Alipokuwa lecturer alijipambanua kama mzalendo, muumini wa demokrasia kumbe siye.
 
Hehehe mara pap John Heche ndani ya CCM
We unasikiliza drama za huyo aliyejitoa akili? Hivi apate barua ya kuomba kujiunga asite site kuwachukua mara moja halafu kumpata diwani wa Kakonko mpaka wamteke na kumtishia uhamiaji yeye na baba yake?

Toka CCM ipate mwenyekiti mpiga fix basi kila mtu ni fix tuu kwenda mbele. Ndio maana huyu Bashiru anasema ushindi wa SM 99.9% ni chama kukubalika, kilaza mkubwa huyu.
 
Niamini ukivaa nguo za kijani inabidi uwaze kwa kutumia makalio sio kichwa, ss ww bashiru unamtangazia nani si uwachukue hata Leo? Unazidi kujidhalilisha
uccm ni majanga. wote waliomfahamu bashiru hawaamini kama ndiye huyu. ninachoomba tu awe mkweli katika hili aliloomba la kuthibitishiwa kuwa wenyeviti, madiwani na wabunge wananunuliwa! naona amechoka kuwa KM, anatafuta njia ya kujiuzulu kwa heshima! mlowola wa takukuru hajaondoka na flashi za nassari. wakati zinatayarishwa naomba atueleze kwa nini matokeo ya uchaguzi mkuu yalifutwa kwa dar 1995 na kwa zanzibar 2015? kama ni dosari ni kwa vituo kadhaa ambao wangerudia na mambo yakaenda! atupe jibu kulingana na sayansi ya siasa tumheshimu kama tulivyomheshimu kabla! vinginevyo: penye mbuzi mwizi, wako usimfunge. ataiba tu.
 
Kuna watu wakifa tutamshukuru Mungu na tutaimba mapambio ya kumsifu yeye na kama majeneza yao yatapita karibu tutayatemea mate..huku ndipo walipotaka tufike na tumefika.
 
Kama anazo si aziweke wazi tu? Kwani ni dhambi mtu kuhama chama?

Mimi naona anafanya hivyo ili wapinzania waanze kuchunguzana wao kwa wao na mwisho waitilafiane.
 
Mnawatia hofu ,alafu hawakuwa wapinzani hao mapandikizi ila na wao wawe makini na hao watu wanatafuta mkate tu sio wanafisiemu wa kweli
 
Unakuwaje mwanachama wa chama ambacho mtu mmoja tu ndo anauwezo wa kukiongoza akifa na chama kinajifia.

Unless uwe mwehu, hakuna future huko.
Vipi kuhusu Jiwe anayeendesha nchi vile atakavyo na sisi wengine tumebaki kukenua mdomo tu?! Akifa na nchi itajifia?
 
Idadi ya wapiga kura katika uchaguzi wa serikali za mitaa inatoa picha halisi ya hao wanaojisifia kukimbiliwa na viongozi wa upinzani...
Tujitafakari
 
Kama tukio la kuhama la Meya tu wa Arusha lilimfanya Polepole akaanza kulia-lia kuwa uhamaji wake haujapewa coverage na media, leo hii Bashiru apokee barua za wabunge wa wapinzani alafu aishie kupiga porojo kwenye vyombo vya habari badala ya kuwapokea?
Subiri wake ndio utajua kuwa anazo barua zao. Moja ni ya Lema.
 
Kama mlivyokimbia nyinyi mlivyo tandikwa Zanzibar 25 Octoba 2015 mliufuta uchaguzi na ingalikua mmeshinda si mngeliufuta uchaguzi.
 
Wananjaa hao wanafuata chakula wachukueni tu Ila mtambue upinzani siyo kuwa chadema au cuf au tlp au nccr au act wazalendo.upinzani hata ccm upo.unanishangaza wewe bashiru umesoma lakini huna akilii
 
“Hakuna njia ya mkato kuishinda CCM”

"Navishauri vyama vya upinzani nchini kuwa, hakuna njia ya mkato ya kuishinda CCM hii katika uchaguzi, wajifunze walichofanya 2015 kwa kuunganisha nguvu, nje ya kuunganisha nguvu wasahau, ushauri mwingine ni wanzishe vyama vya kitaasisi, hawajachelewa"

"Kama CHADEMA iliyoanzishwa na Mzee Mtei akaicha kwa hiyari na kumuachia Marehemu Makani na Makani kumuachia Mbowe, na Mbowe akafuta vijana akina Zitto na Chacha Wangwe na kumvuta Slaa, kama CHADEMA hiyo ingebaki, CCM ingepata tishio kubwa sana"

"Mwalimu J. K. Nyerere alishawahi kutabiri kama kuna chama kutakuwa tishio kwa CCM ni CHADEMA, kumbe Mwalimu alikuwa anaiangalia CHADEMA ya Mzee Mtei na Mzee Makani, CHADEMA ya Mbowe ni kanjanja"
Katika mahojiano yaliyofanyika kupitia kipindi cha Konani kinachorushwa na ITV, Katibu Mkuu wa CCM, Dkt. Bashiru Ally amesema chama hicho kitaendelea kuwapokea viongozi wa vyama pinzani.

“Tutaendelea kupokea vigogo kutoka vyama vya upinzani, hatuwezi kuwanyima uhuru wa kuhamavyama wanavyovichukia kuja chama wanachokipenda, nina barua za wabunge wa upinzani wanaotaka kujiunga CCM. Nawauliza, hamutaki kiinua mgongo? Wanajibu, potelea pote”


Pamoja na hayo, Dkt. Bashiru pia amesema:


“Wapinzani wamekimbia siyo kujitoa”

"Wananchi wafanye udadisi, vyama hivi vinavyosema vilijitoa vina hali gani kisiasa, demokrasia ndani ya vyama vyao ikoje? Mtandao wao wanachama na viongozi nchi nzima ukoje, hayo ndio yanafanya chama kupimwa kama kina hadhi ya kupewa dhamana ya kuongozi serikali"

"Kabla ya uchaguzi wa serikali za mitaa tuliwatawanya mawakili 1250 kote nchini, kuwapa semina wagombea wetu namna ya kujaza fomu kwa usahihi; fomu za ndani ya chama na za kiserikali, maelfu ya wagombea walishindana kwa kupigiwa kura"

"Sasa kama kuna chama kilijaribu kuonesha demokrasia ya ndani ya kuwapata wagombea, kwa hivyo vyama vilivyojitoa halafu kikajitoa kwa sababu zile, mnitajie na niko tayari kujiuzulu" Dkt. Bashiru Ally, Katibu Mkuu wa CCM’’

"Hao wamekimbia sio kujitoa, kati ya nusu ya viti vilivyokuwa vinashindaniwa hao waliojitoa hawakwenda kuchukua fomu kabisa, tafsiri yake ni hawakuwa tayari kushiriki, wanasema 90% ya wagombea wameenguliwa, hata ukiwa na wagombea 10 kisha 9 wakaenguliwa ni 90%"Dkt.''

"Uchaguzi wa serikali za mitaa ni mgumu kuliko kutafuta mgombea wa urais, mgombea urais unaweza kumtafuta hata hotelini, na ndio maana ni rahisi kwa Mzee Rungwe kuwa mgombea urais kuliko kuwa mgombea wa mtaa wake"

“Hakuna njia ya mkato kuishinda CCM”

"Navishauri vyama vya upinzani nchini kuwa, hakuna njia ya mkato ya kuishinda CCM hii katika uchaguzi, wajifunze walichofanya 2015 kwa kuunganisha nguvu, nje ya kuunganisha nguvu wasahau, ushauri mwingine ni wanzishe vyama vya kitaasisi, hawajachelewa"

"Kama CHADEMA iliyoanzishwa na Mzee Mtei akaicha kwa hiyari na kumuachia Marehemu Makani na Makani kumuachia Mbowe, na Mbowe akafuta vijana akina Zitto na Chacha Wangwe na kumvuta Slaa, kama CHADEMA hiyo ingebaki, CCM ingepata tishio kubwa sana"

"Mwalimu J. K. Nyerere alishawahi kutabiri kama kuna chama kutakuwa tishio kwa CCM ni CHADEMA, kumbe Mwalimu alikuwa anaiangalia CHADEMA ya Mzee Mtei na Mzee Makani, CHADEMA ya Mbowe ni kanjanja"

“Tutaendelea kupokea vigogo wa upinzani”

"Tutaendelea kupokea vigogo kutoka vyama vya upinzani, hatuwezi kuwanyima uhuru wao wa kutaka kuhama vyama wanavyoichukia kuja chama wanachokipenda, nina barua za wabunge wa upinzani wanaotaka kujiunga CCM nawauliza, hamtaki kiinua mgongo? wananijibu potelea pote"

"Demokrasia inapimwa kwa vitu vingi sio uchaguzi peke yake, japo uchaguzi ni jambo muhimu. Demokrasia inapimwa kwa uwepo wa uongozi wa kiraia unaojali maslahi ya umma na kujenga matumaini vizazi kwa vizazi kwamba nchi yao itaendelea kuwa huru"

“Tume huru ni ile inayoaminiwa na kila mmoja”


"Na ukiwa na Tume ya Uchaguzi inayotaka kumridhisha kila mmoja na kutaka kutangaza kila anayetaka kutangazwa kuwa mshindi, hiyo haitakuwa tume huru"

"Tume huru inapaswa kuwa ni tume inayoaminiwa kwa wote wanaoshiriki katika uchaguzi, lakini tatizo kwa wanasiasa wanadhani tume inakuwa huru inapowatangaza kuwa wameshinda" Dkt. Bashiru Ally, Katibu Mkuu wa CCM
Wakubwa wa Lummumba wanashindana kuweweseka.
Poleni sana, furaha ya kweli ya raha ya ushindi wa kweli imekosekana. Haiwezekani kuilazimisha.
 
Back
Top Bottom