Dkt. Bashiru: Nina barua za wabunge wa upinzani wanaotaka kuhamia CCM. Wapinzani wamekimbia siyo kujitoa

Shigganza

Senior Member
Joined
May 24, 2018
Messages
157
Points
500

Shigganza

Senior Member
Joined May 24, 2018
157 500
external-content.duckduckgo.com.jpg
Katika mahojiano yaliyofanyika kupitia kipindi cha Konani kinachorushwa na ITV, Katibu Mkuu wa CCM, Dkt. Bashiru Ally amesema chama hicho kitaendelea kuwapokea viongozi wa vyama pinzani.

“Tutaendelea kupokea vigogo kutoka vyama vya upinzani, hatuwezi kuwanyima uhuru wa kuhamavyama wanavyovichukia kuja chama wanachokipenda, nina barua za wabunge wa upinzani wanaotaka kujiunga CCM. Nawauliza, hamutaki kiinua mgongo? Wanajibu, potelea pote”


Pamoja na hayo, Dkt. Bashiru pia amesema:


“Wapinzani wamekimbia siyo kujitoa”

"Wananchi wafanye udadisi, vyama hivi vinavyosema vilijitoa vina hali gani kisiasa, demokrasia ndani ya vyama vyao ikoje? Mtandao wao wanachama na viongozi nchi nzima ukoje, hayo ndio yanafanya chama kupimwa kama kina hadhi ya kupewa dhamana ya kuongozi serikali"

"Kabla ya uchaguzi wa serikali za mitaa tuliwatawanya mawakili 1250 kote nchini, kuwapa semina wagombea wetu namna ya kujaza fomu kwa usahihi; fomu za ndani ya chama na za kiserikali, maelfu ya wagombea walishindana kwa kupigiwa kura"

"Sasa kama kuna chama kilijaribu kuonesha demokrasia ya ndani ya kuwapata wagombea, kwa hivyo vyama vilivyojitoa halafu kikajitoa kwa sababu zile, mnitajie na niko tayari kujiuzulu" Dkt. Bashiru Ally, Katibu Mkuu wa CCM’’

"Hao wamekimbia sio kujitoa, kati ya nusu ya viti vilivyokuwa vinashindaniwa hao waliojitoa hawakwenda kuchukua fomu kabisa, tafsiri yake ni hawakuwa tayari kushiriki, wanasema 90% ya wagombea wameenguliwa, hata ukiwa na wagombea 10 kisha 9 wakaenguliwa ni 90%"Dkt.''

"Uchaguzi wa serikali za mitaa ni mgumu kuliko kutafuta mgombea wa urais, mgombea urais unaweza kumtafuta hata hotelini, na ndio maana ni rahisi kwa Mzee Rungwe kuwa mgombea urais kuliko kuwa mgombea wa mtaa wake"

“Hakuna njia ya mkato kuishinda CCM”

"Navishauri vyama vya upinzani nchini kuwa, hakuna njia ya mkato ya kuishinda CCM hii katika uchaguzi, wajifunze walichofanya 2015 kwa kuunganisha nguvu, nje ya kuunganisha nguvu wasahau, ushauri mwingine ni wanzishe vyama vya kitaasisi, hawajachelewa"

"Kama CHADEMA iliyoanzishwa na Mzee Mtei akaicha kwa hiyari na kumuachia Marehemu Makani na Makani kumuachia Mbowe, na Mbowe akafuta vijana akina Zitto na Chacha Wangwe na kumvuta Slaa, kama CHADEMA hiyo ingebaki, CCM ingepata tishio kubwa sana"

"Mwalimu J. K. Nyerere alishawahi kutabiri kama kuna chama kutakuwa tishio kwa CCM ni CHADEMA, kumbe Mwalimu alikuwa anaiangalia CHADEMA ya Mzee Mtei na Mzee Makani, CHADEMA ya Mbowe ni kanjanja"

“Tutaendelea kupokea vigogo wa upinzani”

"Tutaendelea kupokea vigogo kutoka vyama vya upinzani, hatuwezi kuwanyima uhuru wao wa kutaka kuhama vyama wanavyoichukia kuja chama wanachokipenda, nina barua za wabunge wa upinzani wanaotaka kujiunga CCM nawauliza, hamtaki kiinua mgongo? wananijibu potelea pote"

"Demokrasia inapimwa kwa vitu vingi sio uchaguzi peke yake, japo uchaguzi ni jambo muhimu. Demokrasia inapimwa kwa uwepo wa uongozi wa kiraia unaojali maslahi ya umma na kujenga matumaini vizazi kwa vizazi kwamba nchi yao itaendelea kuwa huru"

“Tume huru ni ile inayoaminiwa na kila mmoja”


"Na ukiwa na Tume ya Uchaguzi inayotaka kumridhisha kila mmoja na kutaka kutangaza kila anayetaka kutangazwa kuwa mshindi, hiyo haitakuwa tume huru"

"Tume huru inapaswa kuwa ni tume inayoaminiwa kwa wote wanaoshiriki katika uchaguzi, lakini tatizo kwa wanasiasa wanadhani tume inakuwa huru inapowatangaza kuwa wameshinda" Dkt. Bashiru Ally, Katibu Mkuu wa CCM
 

VAPS

JF-Expert Member
Joined
Jul 10, 2012
Messages
3,334
Points
2,000

VAPS

JF-Expert Member
Joined Jul 10, 2012
3,334 2,000
Bashiru na wenye CCM yao mnaona fahari kujenga mazingira ya siasa za hovyo? Ni kweli hao wabunge, wanasiasa waliounga juhudi na wanaotaka kuunga juhudi wanafanya kwa hoja halisia zenye tija!?
 

Mchizi

JF-Expert Member
Joined
Apr 23, 2009
Messages
1,650
Points
2,000

Mchizi

JF-Expert Member
Joined Apr 23, 2009
1,650 2,000
Tusifurahi wabunge kuhama, tuchunguze chanzo, mm nahis Mbowe anapaswa kupumzika awachie damu changa na fikira mpya.
Lengo lenu mnataka CHADEMA ichague mwenyekiti legelege ili baadae aseme anajiunga na CCM kuunga mkono juhudi. Kwani chama ni chadema tu, washaurini kina Mrema, Cheyo, Lipumba wasigombee tena uenyekiti.
 

Nono

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2008
Messages
1,408
Points
1,500

Nono

JF-Expert Member
Joined Feb 11, 2008
1,408 1,500
Kwakuwa mnawahakikishia kuwachagua na kuwapitisha bila kupingwa kuwa wabunge 2020-2025 kwanini wasije? Hii ni kwakuwa wanafahamu kuwa hata wakigombea kupitia vyama vyao, wasimamizi watawaengua na watakaopitishwa kugombea hawatatangazwa washindi. Hivyo wakijitathmini wanaona bora waendelee kuwepo kwenye ramani ya siasa hadi haya mfanyayo yatakapofikia mwisho kwa aibu kubwa.
 

Karne

JF-Expert Member
Joined
Jun 13, 2016
Messages
3,546
Points
2,000

Karne

JF-Expert Member
Joined Jun 13, 2016
3,546 2,000
Unakuwaje mwanachama wa chama ambacho mtu mmoja tu ndo anauwezo wa kukiongoza akifa na chama kinajifia.

Unless uwe mwehu, hakuna future huko.
 

Forum statistics

Threads 1,390,223
Members 528,114
Posts 34,046,400
Top