Uchaguzi 2020 Dkt. Bashiru: CCM imefanya kampeni za kistaarabu

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Wakati kampeni za uchaguzi Mkuu zikielekea ukingoni Katibu Mkuu wa CCM Dk Bashiru Ali amesema chama chake kimefanya kampeni za kisasa na kistaarabu.

Dk Bashiru amesema licha ya mikutano ya chama hicho kufurika watu wengi haikuwa ya ghadhabu na hasira bali upendo na furaha vilitawala.

Amesema watanzania wote waliohudhuria mikutano ya CCM wanatambua kuwa mikutano ilikuwa na utulivu mkubwa licha ya kuwa na watu wengi.

Katibu Mkuu huyo amesisitiza kuwa katika kuelekea kusherehekea ushindi wa chama hicho amani itaendelea kutawala.

“Tujitahidi sana ushindi wa CCM uambatane na kudumisha amani, utulivu na upendo kwa watanzania wote. Uwe chanzo cha kudumisha amani na umoja wa taifa letu.

Tujitokeze Oktoba 28 kupiga kura kwa uhuru na hiari yetu na kuichagua CCM iendelee kubaki madarakani kwa ajili ya kuleta maendeleo kwenye taifa hili,” amesema
 
Uchaguzi huu CCM inashinda kwakua upinzani haukua na mtu wa maana, CCM inatakiwa ianze kutekeleza irani ya chamachake kwa kuzingatia mahitaji halisi ya wananchi. kama upinzani ukijitambua uchaguzi wa 2025 unaweza kuwapa CCM changamoto halisi za kisiasa.
 
Mnaota....Kungekuwepo na uhakika wa kushinda Mizengwe, Mbinu ovu na Janjajanja ya nini si Mnapendwa. Mnajifaliji na kutaka kutuaminisha kuwa ushindi ni kiurahisi kivile?
 
Wakati kampeni za uchaguzi Mkuu zikielekea ukingoni Katibu Mkuu wa CCM Dk Bashiru Ali amesema chama chake kimefanya kampeni za kisasa na kistaarabu...
Bashiru anatambuwa kuwa ccm inaruhusiwa kufanya hata yale ambayo wenzao hawaruhusiwi kufanya, CCM ipo juu ya sheria. Polisi hawawezi kumzuia magufuli kusimama kwenye kituo kilicho nje ya ratiba.
 
Wakati kampeni za uchaguzi Mkuu zikielekea ukingoni Katibu Mkuu wa CCM Dk Bashiru Ali amesema chama chake kimefanya kampeni za kisasa na kistaarabu...
Kuwaengua wagombea wa ubenge na udiwani wa upinzani ni ustaarabu?
Kuwapa wagombea wa upinzani adhabu za kutofanya kampeni kwa makosa ambayo CCM wanayafanya wagombea wake ni ustaarabu?

Kuwateka na kuwapiga baadhi ya wanchama wa upinzani ni ustaarabu?
Kutowaapisha baadhi ya mawakala wa upinzani ni ustaarabu?

Bora Hashim Rungwe alikuwa mstaarabu kwa kuwaletea watu ubwabwa kwenye kampeni zake.
 
Ni sahihi lkn ustarabu unaweza kuwekewa alama (marks) kwa asilimia labda angesema ni kwa asilimia ngapi CCM imefanya kampeni za kistarabu

Walioko pembeni ndio sasa wangeweza kupima asilimia hizo kwa kuangalia kampeni tangu zimeanza mpk kuelekea ukomo.
 
Wakati kampeni za uchaguzi Mkuu zikielekea ukingoni Katibu Mkuu wa CCM Dk Bashiru Ali amesema chama chake kimefanya kampeni za kisasa na kistaarabu...
Waliowapeni msaada nao walifanya kistaarabu pia au laa.
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Wakati kampeni za uchaguzi Mkuu zikielekea ukingoni Katibu Mkuu wa CCM Dk Bashiru Ali amesema chama chake kimefanya kampeni za kisasa na kistaarabu...
Msistizo ingekuwa hivi: Tujitahidi sana ushindi wa CCM uwe wa HAKI na uambatane na kudumisha amani, utulivu na upendo miongoni mwa watanzania.
 
Kampeni za ccm zilikuwa chafu na zenye kuhatarisha aman. Sote tumeona Mikutano ya CHADEMA mara kadhaa imevurugwa na either uvccm au police kwa maelekezo kutoka CCM.

Vilevile, CCM wanamshambulia LISSU kuwa ni wakala wa Mabeberu na mashoga. Hili wamelishikia bango kweli ilihali Lissu anazingatia takwa la katiba yetu, ya kwamba kila raia ana haki ya faragha.
 
Wakati kampeni za uchaguzi Mkuu zikielekea ukingoni Katibu Mkuu wa CCM Dk Bashiru Ali amesema chama chake kimefanya kampeni za kisasa na kistaarabu...
Huyu Mhutu ajiandae kurudi Burundi baada ya uchaguzi.
 
Back
Top Bottom