Dkt. Bashiru: Baada ya mzee Kikwete kuingia kura zetu (CCM) zilianza kuporomoka

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
21,247
24,108
January 19, 2020


Katibu Mkuu wa CCM Dkt Bashiru anaichambua safari ya kisiasa ya CCM toka mwaka 2015, ambapo kura za CCM ziliporomoka na Magufuli alipata 58%. Fitna na misukosuko ikawa jadi ya chama. Wasemakweli wakawa maadui wa chama na kupelekea kuitwa na Halmashauri Kuu ya Chama NEC wakapewa adhabu na wengine kufukuzwa

WanaCCM wenye nia njema wakaanza kukaa kando na chama kikaanza kuendeshwa na wachache wababaishaji. Watu wanapata kazi ndani ya CCM bila ujuzi wanapata nafasi hizo kiushikaji. Miradi mingi inayohusu watu (Maendeleo ya Watu) ikafa.

Hata idadi ya wapiga kura ikaanza kuporomoka kutokana na wananchi kukosa imani na CCM. Watu hawana imani na vyombo vya kusimamia uchaguzi chini ya serikali ya CCM.

Dkt. Bashiru katika kikao hicho na wanaCCM anasema wote tunaona Baada ya miaka minne ya Magufuli mambo yamebadilika, yale ya Kikwete niliyoyabainisha yamefutika. Sasa Watu wanaimani na uchaguzi, idadi ya wapiga kura imepanda na kupanda maradufu sana.

Mkazo ktk Maendeleo ya Watu umezidi kusisitizwa sambamba na Maendeleo ya Vitu chini ya Awamu ya Tano.

Bashiru anaendelea kujadili na kuwaomba rai wanaCCM tusibishanie ndege, flyovers, madaraja na SGR reli Mpya maana sote tunaona Maendeleo hayo ya Vitu na Maendeleo ya Watu hivyo tusikazanie ktk kitu 'matumaini', bali vitu halisi tunavyoviona na kuvishika. Matumaini ni matamanio kama mapenzi huwezi kuvipima au kuvishika na hayana uhalisia hivyo haya Maendeleo ya Vitu kama ndege ni maendeleo dhahiri tusiyabishanie.

Bunge limekuwa na heshima hakuna vurugu. Demokrasia na Haki za binadamu imezidi kuzingatiwa kama ilivyoainishwa na Katiba yetu ya nchi. Chaguzi kama za Serikali za Mitaa November 14, 2019 chini ya wizara ya TAMISEMI zimefanyika bila vurugu na CCM imeshinda kwa kishindo asilimia 98%.

Source: Millard Ayo.
 
CCM chama cha wanyonge, nawaona CCM wenzangu hapo aka wanyonge wenzangu.

Enzi za Mzee Kikwete chama kiliporwa kwa wanyonge wakakichukua mafisadi CDM, sasa chama kimerudi tena kwa wanyonge na maendeleo yanakuja kwa kasi balaa, Unyonge ni sifa nzuri sana jamani na ni raha sana kuwa mnyonge na ukachagua chama cha wanyonge CCM.. Tumeamua kuwa wanyonge.
 
Hivi nikianza form one mwakani inaweza kunichukua miaka mingapi ili niwe na PHD, Msaada tafadhali.
Tufanye hesabu kidogo..

Kuanzi form 1 yako

mpaka olevo = 4 Years

Mpaka Alevo = 2Years

Mapaka chuo = 3 Years (Kama wewe ni ngwini, kama utasome MD au engineering tenga miaka 4 au 5)

Mpaka masters = 2 Years.

Mpaka PhD = 3 to 4 Years

Jumla => 4 + 2 + 3 + 2 + 4 = 15 Years!
 
..miaka ya zamani wapiga kura wengi walikuwa wamezaliwa au kukua wakati wa sera ya chama[ ccm ] kushika hatamu.

..kipindi cha Mwinyi na Mkapa ilikuwa ni vigumu kwa vijana na watu wazima kuvipokea vyama vya upinzani kwasababu ya malezi waliyopitia wakati wa mfumo wa chama kimoja.

..miaka ya karibuni wapiga kura wengi wamezaliwa na kukua wakati wa mfumo wa vyama vingi. Mfumo wa vyama vingi umeanza kuzoeleka na kukubaliwa na wananchi wengi zaidi.
 
Back
Top Bottom