Dkt. Bashiru: Baada ya mzee Kikwete kuingia kura zetu (CCM) zilianza kuporomoka

Huo ni ushahidi kwamba CCM ina demokrasia ya kusema ukweli bila kumungunya maneno.

Mlitaka bashiru aseme uongo ili chama kionekane kama kile cha wanamtandao?

Kwani kuna uongo gani katika hayo aliyoyasema Bashiru?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sioni vibaya sana kwa kuwa hili zimwi waliliunda wenyewe! wakalipa power ya kufanya litakavyo! walitarajia yatatukuta wapinzani peke yetu? Hapana! wacha tugawane maumivu!
 
January 19, 2020

'BAADA YA MZEE KIKWETE KUINGIA KURA ZETU ZILIANZA KUPOROMOKA, CHAMA KILIPATA MSUKOSUKO'' BASHIRU

Katibu Mkuu wa CCM Dkt Bashiru anaichambua safari ya kisiasa ya CCM toka mwaka 2015, ambapo kura za CCM ziliporomoka na Magufuli alipata 58%. Fitna na misukosuko ikawa jadi ya chama. Wasemakweli wakawa maadui wa chama na kupelekea kuitwa na Halmashauri Kuu ya Chama NEC wakapewa adhabu na wengine kufukuzwa . wanaCCM wenye nia njema wakaanza kukaa kando na chama kikaanza kuendeshwa na wachache wababaishaji. Watu wanapata kazi ndani ya CCM bila ujuzi wanapata nafasi hizo kiushikaji. Miradi mingi inayohusu watu (Maendeleo ya Watu) ikafa. Hata idadi ya wapiga kura ikaanza kuporomoka kutokana na wananchi kukosa imani na CCM. Watu hawana imani na vyombo vya kusimamia uchaguzi chini ya serikali ya CCM.


Baada ya miaka minne ya Magufuli mambo yamebadilika, yale ya Kikwete niliyoyabainisha yamefutika. Watu wanaimani na uchaguzi, idadi ya wapiga kura imeamua kupanda maarufu.maradufu.

Mkazo ktk Maendeleo ya Watu umezidi kusisitizwa sambamba na Maendeleo ya Vitu chini ya Awamu ya Tano. Bashiru anaendelea tusibishanie ndege, flyovers, madaraja na SGR reli Mpya maana sote tunaona Maendeleo hayo ya Watu na Vitu hivyo tusikazanie matumaini bali vitu halisi tunavyoviona na kuvishika. Matumaini ni matamanio kama mapenzi huwezi kuvipima au kuvishika hivyo haya Maendeleo ya Vitu kama ndege ni maendeleo dhahiri tusiyabishanie.


Bunge limekuwa na heshima hakuna vurugu. Demokrasia na Haki za binadamu imezidi kuzingatiwa kama ilivyoainishwa na Katiba yetu ya nchi. Chaguzi kama za Serikali za Mitaa November 14, 2019 chini ya wizara ya TAMISEMI zimefanyika bila vurugu na CCM imeshinda kwa kishindo asilimia 98%.

Source: Millard Ayo.
Ya mama yako bashiru
 
Huo ni ushahidi kwamba CCM ina demokrasia ya kusema ukweli bila kumungunya maneno.

Mlitaka bashiru aseme uongo ili chama kionekane kama kile cha wanamtandao?

Kwani kuna uongo gani katika hayo aliyoyasema Bashiru?

Sent using Jamii Forums mobile app

..kusema ukweli na kulaumu wengine, lakini siyo Magufuli.

..Yuko aliyesema ni rahisi kumsema vibaya MUNGU kuliko hata kumteta Magufuli.
 
CCM chama cha wanyonge, nawaona CCM wenzangu hapo aka wanyonge wenzangu.

Enzi za Mzee Kikwete chama kiliporwa kwa wanyonge wakakichukua mafisadi CDM, sasa chama kimerudi tena kwa wanyonge na maendeleo yanakuja kwa kasi balaa, Unyonge ni sifa nzuri sana jamani na ni raha sana kuwa mnyonge na ukachagua chama cha wanyonge CCM.. Tumeamua kuwa wanyonge.
Pumbavu hili. Unyonge na ufukara ni laana
 
Njaa kitu kibaya sana, yote hayo ni kutokana na njaa ili amfurahishe bwana wake asife njaa yaani dume zima linaendeshwa kama jike ni aibu kwake huyo mhaya
Kumtukana MTU ambaye alikuweezesha kufika ngazi ya juu na unajua katiba yetu hawezi kukujibu in ukosefu Wa adabu
Lakini Mh. Lissu alituonya kuwa wakimalizana na sisi watakuja kwenu
. Safi sana maana walimjua lakini wakampa nchi awashughulikie tu. Na wao si waliwashughulikia wenzao hadi kuna mawaziri walitumika jela za nje . malipo ni hapa hapa duniani ahera kwa Mungu ni kufunga hesabu


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kumtukana MTU ambaye alikuweezesha kufika ngazi ya juu na unajua kwa katiba yetu hawezi kukujibu ,ni ukosefu Wa adabu na hekima.
Lakini Mh. Lissu alituonya kuwa wakimalizana na sisi watakuja kwenu
. Safi sana maana walimjua lakini wakampa nchi acha awashughulikie tu. Na wao si waliwashughulikia wenzao hadi kuna mawaziri walitumika jela za nje . malipo ni hapa hapa duniani ahera kwa Mungu ni kufunga hesabu


Sent using Jamii Forums mobile app



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wametumwa kumtukana Kikwete wakidhani kwa kufanya wanamjenga mtu wao aliyekosa maarifa ya kuongoza nchi.
"Baada ya miaka minne ya Magufuli mambo yamebadilika, yale ya Kikwete niliyoyabainisha yamefutika. Sasa Watu wana imani na uchaguzi, idadi ya wapiga kura imepanda na kupanda maradufu sana"

Kwa kunukuu tu hayo machache hapo juu, wana CCM hamna Katibu Mkuu ndani ya ofisi yenu nyeti yenye kupaswa kuratibu shughuli za chama, bali bomu lenye kukibomoa na kukipasua chama chenu. Badala ya kufanya juhudi ya kuwaunganisha wanachama na makundi hasimu ndani ya chama, yeye anazidi kukoleza moto.

Atamponza hata huyo anayemsifu na kumuabudu. Ama atakipasua chama chake na kutokea pande lenye nguvu la chama cha kipya cha upinzani chenye nguvu na imara ili utabiri wa Mwl. Nyerere ukapate kutimia. Ama la, atamwingiza anayemsifia ktk historia ya kuwa Rais wa kwanza kutawala kwa miaka mitano tu ndani ya nchi hii.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom