Dkt. Bashiru awahimiza wana CCM Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kuenzi miaka 100 ya fikra za Mwalimu

Uzalendo Wa Kitanzania

JF-Expert Member
Mar 8, 2020
740
1,000
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Bashiru Ally amewahimiza wanaCCM wa Chuo Kikuu Cha Dar es salaam kuenzi miaka 100 ya fikra za Mwalimu Nyerere, Aprili 2022.

Ameysema hayo leo tarehe 21 Februari, 2021 akizungumza na Umoja wa Vijana wa CCM Chuo Kikuu Cha Dar es salaam.

"Mwaka kesho Aprili, Baba wa Taifa Mwl. Nyerere atatimiza miaka 100 ya uhai wake tangu Aprili, 2022 azaliwe mpaka sasa. Kutakua na sherehe kubwa katika nchi yetu, na kwa Chama Chetu lazima tudhihirishe kabisa kwamba tunamuenzi baba wa Taifa mwaka kesho mwezi Aprili."

"Na mimi nipendekeze hapa mbele yenu kwamba, WanaCCM hapa Chuo Kikuu Cha Dar es salaam, muwe mstari wa mbele katika maandalizi ya sherehe hizo, kwa sababu miaka 100 ya utoto wake, malezi yake, maisha yake ya kisiasa, maisha yake ya kiraia, mpaka anafariki na hadi sasa yamebeba urithi mkubwa wa Taifa letu Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam kikiwepo"

Aidha, Katibu Mkuu pamoja na mambo mengine amesisitiza umuhimu wa Utunzaji wa mazingira kutokana na kutoridhishwa na usafi katika Jiji la Dar es Salaam.

Imetolewa na;
Said Said Nguya
Afisa Habari
Ofisi ya Katibu Mkuu
CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)
 

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
8,786
2,000
Naona Bashiru ana wazo kama hili au amepitia uzi huu

 

tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
39,437
2,000
Hapo wanataka kusherehekea miaka 100 ya siku aliyozaliwa Nyerere, au miaka 100 ya mawazo yake? Kama ni kusherehekea mawazo yake basi miaka 100 bado, na kama kusheherekea miaka 100 ya kuzaliwa kwake, sioni mantiki ya jambo hilo, labda kama wanataka kulisha watu mitazamo ya kijamaa aliyokuwa nayo Nyerere.
 

Kiranga

JF-Expert Member
Jan 29, 2009
56,158
2,000
Mtu amefariki atatimizaje miaka 100 ya uhai wake mwaka kesho?

Watanzania wengi mtu anaweza kuwa na Ph.D ya Political Science, lakini kujieleza mgogoro.

Tena kwa Kiswahili, wala si Kiingereza.
 

CCM MKAMBARANI

JF-Expert Member
Mar 15, 2017
811
500
Lazma tukubali kuwa kama tunataka ujamaa basi tuuboreshe ueendane na nyakati lkn si wa enzi zile
 

Bishweko

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
2,865
2,000
The Great Hima Empire..
Hivi kweli huyu ndiye mwenye PhD...alafu Katibu Mkuu Kiongozi anaongea na Wanaccm..
Wabongo ni ndezi kweli.
Kaka Lissu baki huko uliko ili Taifa alikufai
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom