Dkt. Bashiru anaweza kuondolewa Bungeni kwenda kulitumikia Taifa sehemu atakayokuwa huru kutumia taaluma yake?

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
May 18, 2019
762
6,980
Dr. Bashiru ni Mbunge wa kuteuliwa ambaye kama walivyo Wabunge 19 wa upinzani ameonyesha kushindwa kabisa kurejesha confidence na taaluma yake ndani ya bunge. Nakubali ndugu yangu huyu alikengeuka akajione next to president but may be hakuwa yeye Bali waliomzunguka.

Dr. Bashiru ameshiriki kuwapeleka Bungeni Wabunge asiimia Kubwa waliopo Sasa, wengi wasingepita ila Kwa figusu za Bashiru walipita. Anamkono Kwa akina Mdee na naamini endapo akina Mdee wangeakikishiwa usalama wao Leo Hii wakaeleza walifika vipi Bungeni naamini Bashiru atatajwa. Tukumbuke hata kuapishwa walikula kiapo Nje ya Ukumbi wa Bunge.

Kutokana na msongo wa mawazo alionao Dr. Anatakiwa akakae sehemu hata kama hadhi yake ni ndogo basi atulie apunguze stress za masimango yakivitendo anayopitia. Anapitia sonona isiyo na kifani na naamini anatamani kuondoka ila ataelewekaje?

Kuliko kuendelea kulipwa posho Bure Bungeni huku akiwa azalishi Wala kuchangia chochote Bora apangiwe KAZI nyingine kama Polepole. Aliowapigania waingie Bungeni bila UCHAGUZI huru Leo wanamwangalia kama ibanana , so sad.
 
Kuliko kuendelea kulipwa posho Bure Bungeni huku akiwa azalishi Wala kuchangia chochote Bora apangiwe KAZI nyingine kama Polepole. Aliowapigania waingie Bungeni bila UCHAGUZI huru Leo wanamwangalia kama ibanana , so sad
Tafauti na polepole, bashiru hana kelele zozote.. So, wacha asome magazeti tuu, au arudi chuo kufundisha.

Kumbuka polepole alikuwa anatishia kufurusha 'wahuni' a.k.a. 'chawa' kwa kuwafukizia moshi !!!
 
Inasemekana yey ndiye alikuwa anakwenda kuwa next president baaada ya jiwe .jiwe ameona yey ndiye mriddh wake ndio maana akamtoa chamani na kumleta hapo Kama kmk, sijui nchi ingekuwaje Kam mkomunist wa namna ile kupata madarak makubwa.
 
Nampongeza Mwandishi wa aya hii kuhusu Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuweza kuondolewa Bungeni, isipokuwa naomba kutofautiana naye kwa HOJA za Kisheria na KIKATIBA kama basi katiba inafuatwa..


Kwa Mwanafunzi yeyote wa sheria aliyemaliza somo la LW 102 Constitution and Legal Systems of East Africa na ambaye yupo Mwaka wa Pili au wa Tatu na amesoma na kuelewa Administrative Law LW 203 atashangaa sana Namna gani Mkuu wa Mhimili 1 anavyoweza kumwondoa Mtumishi wa Mhimili mwingine hasa kwa kuzingatia dhana ya Separation of Powers as stipulated by Montesquieu,

Ukweli wa Kikatiba upo hivi;

ibara ya 67(1) inazungumzia SIFA za mtu kuwa Mbunge qualifications na 67(2) a - h inazungumzia SIFA ZA KUMZUIA MTU KUCHAGULIWA AU KUTEULIWA, yaani hii inaongelea makatazo ya Mtu kuwa Mbunge, bado hajawa Mbunge ila kama anataka kuwa MP akiwa na sifa hizi haruhusiwi, hasa iliyotumika kimakosa kumwondoa Mbunge ile inayosema (g) ikiwa mtu huyo AMESHIKA madaraka ya AFISA MWANDAMIZI katika utumishi wa serikali ya Jamhuri ya Muungano isipokuwa madaraka ambayo RAIS anaweza au anatakiwa kukabidhi kwa Mbunge kwa mujibu wa Katiba hii au sheria iliyotungwa na Bunge"

Neno Afisa Mwandamizi kwa mujibu wa interpretations of laws ni Katibu Mkuu Kiongozi, Katibu Mkuu wa Wizara au Naibu Katibu Mkuu, UBALOZI sio Afisa Mwandamizi na ndio maana watu huacha ubalozi na kuja kugombea Ubunge na tuna mabalozi ambao ni wabunge kama Mhe.Balozi Mulamula, Balozi Bashiru,Nk

Yaani haiwezekani Mtu ambaye ni MBUNGE (DIPLOMATS) akageuzwa kuwa AFISA MWANDAMIZI kwa sababu Mbunge ni SENIOR kwa AFISA Mwandamizi

Kwa mfano 2016 wakati Mhe Balozi Dr.Posi anateuliwa kuwa Balozi, ilibidi yeye Mwenyewe KUJIUZULU UBUNGE baada ya Rais kuzidisha idadi ya wabunge 5 wanaoruhusiwa kikatiba,Mbunge ASIPOANDIKA BARUA YA KUJIUZULU AU KUFUKUZWA UANACHAMA, HAKUNA NAMNA YA KUMWONDOA UBUNGE unless kwa masharti mengine ya Kikatiba.

Kitendo cha leo kuapishwa kwa Mhe Nahodha kuwa Mbunge kumefanya IDADI ya wabunge walioteuliwa na Rais kufikia 6 ambayo ni kinyumbe cha Katiba inayoruhusu wabunge 5 wanaume na 5 wa Wanawake,

Kikatiba POLE bado ni Mbunge kwa sababu hajajiuzulua na kuteuliwa kuwa Balozi hakuondoi mtu kuwa Mbunge,

yaani Mbunge kamwe hawezi kuteuliwa kuwa Katibu Mkuu Kiongozi wa Wizara na hata Uteuzi wa Dr Bashiru kuwa KMK na kuteuliwa kuwa Mbunge ilikuwa ni KUVUNJA KATIBA ibara ya 67(g) ambayo pia imeVUNJWA kutaka kuaminisha umma kuwa POLE sio Mbunge.

Mtoto anaweza kuwa MTU mzima, lakini Mtu mzima kamwe hawezi kuwa Mtoto; Mbunge ni Mkubwa kwa Katibu Mkuu, sasa inawezekanaje kumgeuza Mbunge kuwa AFISA MWANDAMIZI?/

Kwa kuhitimisha hoja hii, haiwezekani kwa RAIS kumwondolea Mbunge ubunge wake isipokuwa kwa Mbunge kujiuzulu au kuvuliwa Uanachama wa chama cha SIASA au masharti mengine ya Kikatiba kama kushitakiwa mahakamani au masuala ya maadili ya Viongozi au kukosa mikutano 3 ya Bunge bila kibali cha Spika"

Ieleweke kuwa POLE ni mbunge kwa sababu huwezi kumgeuza Baba kuwa Mtoto ila Mtoto anaweza kuja kuwa Baba
 
Tafauti na polepole, bashiru hana kelele zozote.. So, wacha asome magazeti tuu, au arudi chuo kufundisha.

Kumbuka polepole alikuwa anatishia kufurusha 'wahuni' a.k.a. 'chawa' kwa kuwafukizia moshi !!!

Umefurahisha siku yangu, imenikumbusha enzi za JKT Ruvu ukiingia Bar wee piga yowe la ...Heei! Wote wah7sika utawajua Polepole kongole
 
Maisha ni kama chupi ya ndani utake utavaa utake utavaa.
Chawa wa magu wanapitia kipindi kigumu Sana
 
Back
Top Bottom