Dkt. Bashiru ameikumbusha CCM kuwa ni chama cha wakulima na wafanyakazi siyo walanguzi!

ego

JF-Expert Member
Apr 10, 2013
1,620
1,407
Kauli ya Dr Bashiru na mjadala ulioibuka unatosha kufanya tathmini ya chama.

Sisi tukiwa elimu ya msingi tulifundishwa kuwa CCM ni chama cha wakulima na wafanyakazi, je hivi kweli chama chetu hiki kinasimamia hiyo misingi iliyoasisiwa na waasisi wake?

Hotuba ya bashiru iliashiria mwana CCM anayejua misingi ya chama ni nini lakini pengine akiona "gepu" kati ya misingi na utekelezaji wa sasa. Hotuba ile ililenga kuamsha tena hari ya wakulima.

Lakini ukisikiliza waliomjinu, wote wanazungumzia bajeti iliyotengwa katika kilimo na sio wakulima wamepiga hatua gani?

Chama kijitafakari kama yawezekana kuna watu wa kati wanaonufaika na mikakati inayowekwa na kufanya tabaka la chini la wakulima na wafanyakazi wasipate neema. Hawa watu wa kati ndiyo huitwa walanguzi.
 
Back
Top Bottom