Ad majorem
JF-Expert Member
- Aug 11, 2018
- 819
- 1,286
Wanasheria mtusaidie. Sheria inasemaje pale mtumishi wa Umma anapochaguliwa kuwa Kiongozi kwenye chama cha siasa? Je, nafasi yake ya Utumishi wa Umma inakoma au anaweza kuomba likizo Wakati akifanya kazi za chama na akaendelea kuwa mtumishi wa Umma? Turejee yaliyotokea kwa wafanyakaz wa serikali waliotia nia kugombea nafasi mbalimbali za Uongozi Wakati wa uchaguzi mkuu uliopita. Kitendo kilichosabaabisha mishahara yao izuiliwe. Ni kwa mantiki hiyo naamini utumishi wa Umma wa Bashiru ulikoma alipokubali na kuapishwa kuwa Katibu Mkuu wa chama. Yaliyoendelea baada ya hapo ni uchafuzi tuu.