Dkt. Bashiru Ally amtaka Bernard Membe kujibu kuhusu kufanya vikao vya kutafuta kura 2020

issenye

JF-Expert Member
Feb 2, 2011
3,781
5,205
MADAI YA KUMKWAMISHA JPM: Katibu mkuu wa CCM, Dkt. Bashiru Ally amemtaka aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje, Bernald Membe kufika ofisini kwake kukanusha madai yanayomkabili.

Bashiru Ally ametema cheche hizi kwa waziri wa zamani wa Mambo ya Nje, Bernard Membe ambaye pia ni mwanachama wa CCM kufika ofisini kwake kuzungumzia tetesi zinazoenea kuwa anafanya mipango ya kutafuta kura 2020.

 
Bernad Membe ni mtu mmoja mwenye akili sana, nadhani ndio kichwa pekee aliebakia LUMUMBA.

1) Anajua kucheza na vichwa vya watu.

2) Anajua wapi aongee na wapi akae kimya.

3) Unapo hitaji aongee, yeye anakaa kimya (anakupima uvumilivu, ustahmilivu, na fikra zako. Kisha uyakanyage).

4) Haulizi swali bila ya kujua majibu kwanza.

5) Intelligent by nature.

*** Dr. Bashiru asifikiri anaweza akashindana nae kisaikolojia, hoja, na uelewa. Na kwa mtazamo wangu amekurupuka kufanya huo wito (na kama si kukurupuka, alipaswa kutumia hata simu kumwita PRIVATELY na kwa kufuata TARATIBU NA KANUNI ZA CHAMA, sio kwa kumtangaza wazi wazi).

*** Mtuhumiwa siku zote hua haitwi KUTHIBITISHA KOSA alilofanya, mlalamikaji ndio hua anatakiwa ATHIBITISHE malalamiko yake kwa mhusika. Hatujawahi kisikia mtu anabaka au kuua halafu anaitwa MAHAKAMANI KWENDA KUTHIBITISHA JINAI ALIOFANYA, bali mlalamikaji ndio anakwenda KUTHIBITISHA MALALAMIKO YAKE dhidi ya MTUHUMIWA (Kisha mtuhumiawa ndio ANAJITETEA). Mbona mlalamikaji (Cyprian Musiba) HAJAITWA NA CHAMA kwenda kuthibitisha malalamiko yake dhidi ya mhusika???? Ili Benard Membe akikutwa na hatia aitwe kujitetea???

*** Kama kuna UKWELI dhidi ya tuhuma hizo, Dr Bashiru si aziweke wazi ili mtuhumiwa akiwa anaenda KUJITETEA ajue kipi cha kujitetea kutokana na mashtaka yaliyopo.

Dr. Bashiru anakua VICTIM mwingine, katika list ya watu watakao pelekeshwa kisaikolojia na Ben Membe. Poor him.

USHAURI, Kama wanahisi Ben Membe ni adui kwa JIWE, basi avuliwe uanachama tu, CCM si wanajifanya hawa bembelezi mtu. Halafu patakua patamu akaungane na Zitto , ndio watakapo mjua ana IQ ya aina gani Membe.

# Zitto 2020
 
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Bashiru Ally amemtaka aliyekuwa mgombea uteuzi wa kugombea kiti cha urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) mwaka 2015 Bernard Membe, ajitokezea ili kujibu tetesi zinazodai kwamba, Membe anafanya vikao vya kutafuta kura 2020 pamoja na kuwa na mipango ya kumkwamisha Rais John Magufuli.
IMG_20181130_211742_816.jpeg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom