Dkt. Bashiru Ally ''amkaanga'' Lazaro Nyalandu

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
13,172
23,974
Katika mahojiano maalum, Mtangazaji Charles Hilary wa Azam TV alianza kwa kumuuliza Dkt. Bushiru Ally kama anadhani Lazaro Nyarandu ni jasiri kwa uamuzi wake wa kuondoka CCM.

Dkt. Bushiru alijibu na kusema katika siasa wakati hutoa majibu halisi, tuna orodha ndefu ya watu walioitwa majasiri. Kwa mfano Dkt. Slaa wakati akiwa Katibu Mkuu na Mgombea Urais wa Tanzania ulikuwa unamuona alivyo jasiri kwenye jukwaa, kihoja na msimamo lakini leo yuko wapi? Tuna orodha ndefu. Kuhangaika na ujasiri wa mtu mmoja mmoja ni kupoteza muda kwa sababu kuna uwezekano hata yeye baada muda akapotea katika uwanja wa siasa.

Swali kuhusu tuhuma za Nyalandu kwa serikali ya Rais Magufuli kuingilia mihimili mingine ya dola na kusema kujiondoa kwake CCM iwe ni chachu ya kuanzisha mjadala wa suala hilo.

Dkt. Bushiru alitoa jibu kwa kusema, mjadala kuhusu serikali kuingilia mihimili mingine ya dola imeanza kabla hata ya Lazaro Nyalandu hajazaliwa.

Dkt. Bushiru alisema, misuguano ya mihimili ya dola kuhusu nani anamwingilia mwenzake ipo sio Tanzania pekee bali duniani kote kwenye nchi ndogo kama Tanzania na nchi kubwa kama Marekani. Hata wakati wa tawala zilizopita nchini mjadala ulikuwepo na kwa maana hii, anachokisema Lazaro Nyalandu siyo kipya.

Dkt. Bushiru alienda mbele zaidi na kusema, mihimili ya dola ni taasisi zinazotegemeana, ingawa zinaweza zikawa na mamlaka ya kiutendaji ya ndani lakini kimfumo, hizi ni taasisi zinazohudumia taasisi kuu moja inayoitwa dola. Hakutakuwa na muafaka/makubaliamo kwa wananchi wote kwa sababu vyombo hivi pia vinaingiliana, vinategemeana, vinasaidiana na vinafanya kazi moja ya kuwahudumia wananchi.

Charles Hilary alimuuliza kuhusu madai ya Nyalandu kuhusu CCM kushindwa kuisimamia serikali.

Dkt. Bushiru alijibu na kusema, huo ni mtazamo wa Nyalandu lakini anachojua yeye CCM ndio inayounda serikali na hakuna mtu aliye na cheo cha kisiasa ambaye hajapitishwa na vikao vya CCM kwa mujibu wa katiba yao lakini kikubwa zaidi, katiba ya Tanzania inasema, hakuna mtu anayeweza kuingia kwenye siasa bila kuidhinishwa na chama cha siasa. Katiba ya Tanzania hairuhusu wagombea binafsi. Kitendo cha mbunge kuhama chama kilichomteua kuwa mbunge kinamuondolea uanachama na ubunge bila hata ya kuandika barua kwa spika wa bunge. Chama ndicho kinachotengeneza serikali kupitia uchaguzi.

VIDEO:
 
Kuna hoja ya Nyalandu anayodai kuhusu CCM kwa sasa kukosa dira.

Kwanza unaposema kwa sasa CCM imekosa dira wakati umekuwa ndani yake kwa kipindi kirefu inabidi utueleze, kipindi cha nyuma ilikuwa na dira gani?

Je, hiyo dira iliyokuwepo kipindi cha nyuma ilikuwa inaonekana kwenye chama alichojiunga nacho? Hajui kuwa wakati akiwa Waziri ndani ya CCM alikuwa anaambiwa na wenye chama alichojiunga kuwa hana maono ya Uwaziri na chama chake hakina dira?

Je, chama alichojiunga nacho kimepata dira baada ya CCM kukosa dira? Au dira inapatikana tu pale yeye unapokuwa Naibu Waziri au Waziri?

Hiyo ''dira'' ya CCM iliyokuwepo ''kipindi cha nyuma'' wakati yeye akiwa Waziri wa Maliasili na Utalii ilimsaidiaje mwananchi hasa mwenye uwezo mdogo kielimu na kiuchumi?

Tujikumbushe ushauri aliotoa Mbunge Joshua Nassari kwa Lazaro Nyalandu katika hii video!
 
Nimeshindwa kusoma Mpaka mwisho maana nimepata kichefuchefu katikati ya andiko
Hilo ni tatizo lako kwa sababu hukulazimishwa kufungua thread na kusoma.

Kumbuka huwezi kuupima ujinga wako kwa kuishi ndani ya fikra zako.

Unanikumbusha kuna mzee mmoja alikuwa anaisifia sana nyumba yake lakini siku moja akapata mwaliko kwenye ufunguzi wa nyumba ya rafiki yake, aliporudi nyumbani akamwambia mkewe alichokiona na kudai amekuwa akijidanganya kuwa nyumba yake ni nzuri kumbe kuna nyumba za rafiki zake ambazo ni nzuri zaidi yake.

Hii ni sawa na maneno ya waingereza yanayosema, ''Thinking beyond the box''.
 
Nimeshindwa kusoma Mpaka mwisho maana nimepata kichefuchefu katikati ya andiko
Ukitaka kuwa critical soma na mawazo ya wengine. Hakuna lolote jipya alilofanya kwa kuhama na sio mtu wa kwanza. Alishanusa kuwa anaandaliwa vikao vya kumhoji kuhusu mwenendo na msomamo wake. Huko anakikwenda akifika aulize kilichomtoa zito kabwe ni nini. Kila chama kina misingi na taratibu zake. Ukiona hazikufai unaondoka kama alivyofanya.
 

Similar Discussions

24 Reactions
Reply
Back
Top Bottom