Dkt. Bashiru Ally akemea adhabu za viboko zinazofanywa na Maofisa wa Umma

Suala la kuwageuza walemavu kitega uchumi kwa kuwa mba omba kisha mapato achukue tajiri hili ni zaidi ya unyama.
Walistahiki kunyongwa na si viboko tuu.
Hivi viboko ni bashraf tuu ,hawajapelekwa mahakamani , na pengine mahakama iseme hawana hatia , au waambiwe walipe fine au wafungwe miezi 6 tuu.
Yu see
 
Wakati uzi wa ma dc kuwachapa viboko watu mliwasifia kwa mapambio. Leo mwana ccm wemu kawakataza mnamsifia kama kawaida yenu.

Hivi mshaongezewa au bado mnalipwa buku 7?
Mkuu tafuta comment Yangu yoyote inayoonesha Mimi kushabikia uvunjifu Wa haki za binadamu na kuingiliwa kwa Uhuru Wa kimahakama na uilete kama uthibitisho

Kamwe sijawahi kuwa muumini Wa upuuzi huu.
 
Katibu na wewe tumia viboko ndio tutaimalisha uchumi wa kati haraka twende uchumi wa dunia ya kwanza .
Screenshot_20210103-222821.png
 
Raisi Magufuli ndiye anayehusika na kuwapiga viboko Watanzania kwani yeye Raisi ndiye Big Boss wao, acheni kutufanya wajinga, atavuna alichopanda kama anaendeleza chuki hii dhidi ya Watanzania, ...
aiseeh kweli Tunaisoma namba kila raia ....Mkuu
 
Kwa kuwa amepewa rungu la kuisimamia Serikali basi awafukuze kazi kama ilivyotokea kwa DC Mnari miaka ile kule Bukoba
 
Raisi Magufuli ndiye anayehusika na kuwapiga viboko Watanzania kwani yeye Raisi ndiye Big Boss wao, acheni kutufanya wajinga, atavuna alichopanda kama anaendeleza chuki hii dhidi ya Watanzania, ...
Mkuu umekuaje tena....yaani watu wafanye personal decisions tena kwa mihemko then lawama ziende kwa Rais hii sio sawa.
 
Akiwa mkoani Kagera, Ndugu Bashiru Ally ambaye ni Katibu wa CCM amesema anashangaa vitendo vinavyotaka kujikita mzizi kwa maafisa wa Serikali kujichukulia sheria mkononi.

Bashiru Ally amewashangaa maafisa hao wanaoshindwa kutofautisha kazi za mihimili yaani mahakama, Serikali na Bunge.

Bashiru Ally amesisitiza kuwa mwenye mamlaka ya kutoa adhabu ni Mahakama tu na si vinginevyo, Amesisitiza Mahakama ndio yenye uwezo wa kupima kosa na kutoa adhabu.

Ndugu Bashiru amewaonya watendaji hao wa serikali kuacha kuvunja sheria za nchi kwa kuwacharaza watu viboko.

Rais alishasema ukifanya kazi utaonekana lakini si kwa kujipiga piga picha na kuvunja sheria ili uonekane, Kigwangalla aliyafanya hayo lakini sasa ameachwa pembeni tupo nae mtaani bila ulinzi tukitegemea sungusungu na ulinzi shirikishi.
Kukemea bila kuwachukulia hatua waliochapa wenzao ni KUBARIKI vitendo vinavyofanywa na hao maofisa wa UMMA
 
Akiwa mkoani Kagera, Ndugu Bashiru Ally ambaye ni Katibu wa CCM amesema anashangaa vitendo vinavyotaka kujikita mzizi kwa maafisa wa Serikali kujichukulia sheria mkononi.

Bashiru Ally amewashangaa maafisa hao wanaoshindwa kutofautisha kazi za mihimili yaani mahakama, Serikali na Bunge.

Bashiru Ally amesisitiza kuwa mwenye mamlaka ya kutoa adhabu ni Mahakama tu na si vinginevyo, Amesisitiza Mahakama ndio yenye uwezo wa kupima kosa na kutoa adhabu.

Ndugu Bashiru amewaonya watendaji hao wa serikali kuacha kuvunja sheria za nchi kwa kuwacharaza watu viboko.

Rais alishasema ukifanya kazi utaonekana lakini si kwa kujipiga piga picha na kuvunja sheria ili uonekane, Kigwangalla aliyafanya hayo lakini sasa ameachwa pembeni tupo nae mtaani bila ulinzi tukitegemea sungusungu na ulinzi shirikishi.
Ni jambo jema ila ninashangaa ni kwanini Bashiru Ally Kakurwa hakemei na hajakemea pia Mauwaji na Utekwaji wa Wakosoaji wa Awamu ya Tano.
 
Bashiru si maneno matupu, akiongea hivo mwenyekiti wake atakuja kupigilia msumari ,alivyofanya kwa kina makonda kwamba waridhike na vyeo vyao wakikosa kuchaguliwa wasitegemee kuteuliwa, mwenyewe unaona sasa hivi.
Hiyo kusema tu ni jambo kubwa la kupongezwa mkuu,kusema ndio mwanzo wa kukemea
 
Katibu wa ccm kwa sasa ni kama katibu wa vikao tu , hana mamlaka yoyote yale
Sikilize wewe red blood cell,hiyo kusema tu ni hatua nzuri sana mkuu ukizingatia kuwa kulikuwa na dhana kwamba watafichiana na kutokukemeana pale wanapokweda mrama
 
Usiwe unacoment kama mlevi fuatilia comments zangu zote kuhusiana na hii saga nilikuwa nakemea kila siku.

Next time shirikisha ubongo wako kabla ya kuandika ujinga humu.
Big boss aliwahi kumtetea hadharani chalamila alipowacharaza wale wanafunzi wa simu. Ulikemea wapi kama si kupiga makofi ?!
 
Sikilize wewe red blood cell,hiyo kusema tu ni hatua nzuri sana mkuu ukizingatia kuwa kulikuwa na dhana kwamba watafichiana na kutokukemeana pale wanapokweda mrama
Magufuli alimsifia hadharani RC wa Mbeya kwa kuwacharaza wanafunzi kinyume cha sheria za nchi , huyu ndio mteuzi , unadhani usanii wa Bashiru nani atadanganyika nao ?
 
Back
Top Bottom