Dkt. Bashiru: Aliye na dola ndiye ananufaika nayo kubaki madarakani, hata CHADEMA ikiingia madarakani ikaondolewa kwenye dola ni uzembe wao

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,868
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Bashiru Ally akifanya mahojiano na kituo cha utangazaji ITV amenena haya kuelekea uchaguzi Oktoba 2020.


HOTUBA KWA UFUPI

Bashiru.jpg

CCM imejiandaa kushinda kihalali, na ushindi wenyewe sio wa Oktoba, ulianza kutafutwa tangu 2015,hiyo ndio tiketi yetu

Tatizo kubwa tulilokuwa nalo katika nchi yetu wananchi walishaanza kupoteza imani katika mchakato wa uchaguzi, na kuna wakati tumefikia hatua ambayo wanaojiandikisha idadi yao inakuwa kubwa lakini wanaojitokeza kwenda kupiga kura idadi inapungua hilo si jambo zuri.

Nasikia watu wanasema uchaguzi uwe huru na haki,lakini lazima tupanue tafsiri ya haki,eneo kubwa ambalo tunahitaji kuwekeza nguvu zaidi ni ushiriki wa vijana na akinamama,haya ni makundi ambayo mara nyingi hutumika na wanasiasa lakini hayanufaiki na jasho lao.

Hakuna atakayeteuliwa ndani ya CCM hasa waliyopo madarakani, bila kwenda kwenye rekodi ya utendaji wao..hakutakuwa na uteuzi wa bure.

Ukishika mbili zote zinaweza zikachomoka, aliye na dola ananufaika na dola hiyo kubaki madarakani, huo ni ukweli hata CHADEMA ikiingia kwenye dola kuiondoa kwenye dola utakuwa ni uzembe wake kwa sababu ana nafuu na faida yakuwa na dola.

Ninachoomba mimi wanasiasa wenzangu wafate sheria,maelekezo na taratibu,kwasababu nchi hii tukigeuza kuwa wakati wote ni kusema chochote na kufanya chochote..tutatafutana,ni vizuri tukawa na utaratibu wa kutujengea nidhamu.

Ni shabaha yetu kufika 50/50 lakini ni safari ndefu na ngumu lakini tutafika, hakuna kurudi nyuma, kwa ufupi ni mapambano.

Mchakato wa katiba mpya ni kiporo kilichochacha, ukila utaumwa matumbo.

Wanaosubiri sisi tulegelege kwenye kutumia dola kubaki kwenye dola watasubiri sana, hata Trump kumuondoa ngumu, kuna nafuu kubwa na faida kubwa chama kilichopo madarakani kutumia nguvu za dola kufanya mambo ya kujenga imani kwa wapiga kura ili kiweze kubaki madarakani. Aliye na dola ndiye ananufaika na dola ile kubaki madarakani, huo ni ukweli na hata CHADEMA ikiingia madarakana ikaondolewa kwenye dola ni uzembe wake. Kwasababu ana nafuu na faida ya kuendelea kubakia.

Ukidhulumu mtu nikajua natafuta dola ishughulikie mtu aliyedhulumu ili nibaki madarakani, na kwakweli zamu hii ninahakika ya kushinda uchaguzi kwa sababu nitatumia dola barabara.

Ninachojua mimi hakuna mikutano iliyozuiliwa,na Polepole ni Katibu wa Itikadi na Uenezi anatangaza tuliyoyafanya ili CCM isiondolewa madarakani,sasa unataka ayatangazie wapi,chumbani?

Ilani sio Msahafu, inaweza kutekelezeka kwa kiwango fulani na si lazima iwe asilimia 100.

Hii hali ya kisiasa mnaiona,na vyama vyetu mnaviona,hivi kuna tishio ya ushindani wa kufa na kupona katika nchi hii,kiasi ambacho tuwe na uoga kwamba hautakuwa huru na haki?,mimi ntamuibia nani ana nini huyo?

Sitaki kufanya siasa za propaganda hapa, timu mnaziona? unaweza kabisa kuona ni timu gani itafunga mabao mengi? Katika mazingira ambayo kuna ushindani mkali ndio tahadhari inatakiwa kuchukuliwa,sasa jamaa anapigwa hadi mechi za mazoezi,unawasiwasi gani na refaa?

Dkt.Magufuli ametusaidia sana, kutumbua majipu, kusimamia serikali, kudhibiti matumizi mabaya ya pesa, tumetumia vizuri dola kubaki madarakani, kukusanya kodi dola hiyo hiyo ndio tunayoitumia, tulikuwa kwenye bilioni 800 sasa hivi tuko above trilioni 1


----
MAONI YA MDAU
Nimechanganyikiwa kabisa, Kumbe nguvu ya CCM Ni Dola? Katibu wetu mkuu apunguze kuongea Sana kwenye vyombo vya habari.

Kumbe Upinzani unapambana na Dola na CCM kwa Pamoja? Kwa hiyo CCM Haina Tena ushawishi wa kuchaguliwa bila Kutumia Dola?

Vidole vyangu kataa kuandika zaidi utakosea ngoja tu niishie hapa, ila Katibu mkuu naomba anaki zaidi kwenye shughuli za Operations hizi Media amwachie Polepole. Hii statement yake nimekuelewa vibaya? Au ndivyo anavyomaanisha?

Ndio naelewa ile kanuni ya RPC Arusha kuwa kama A=B na B =C basi C =A. Hapa alikuwa anaonyesha uhusiano uliopo Kati ya jeshi la Polisi na CCM. Kuna Mambo ya kuongea hadharani na Mengine Chumbani

Ole Mushi
0712702602
 
"Wanaosubiri sisi tulegelege kwenye kutumia dola kubaki kwenye dola watasubiri sana, hata Trump kumuondoa ngumu, kuna nafuu kubwa na faida kubwa chama kilichopo madarakani kutumia nguvu za dola kufanya mambo ya kujenga imani kwa wapiga kura ili kiweze kubaki madarakani"- Bashiru

"Aliye na dola ndiye ananufaika na dola ile kubaki madarakani, huo ni ukweli na hata CHADEMA ikiingia madarakana ikaondolewa kwenye dola ni uzembe wake. Kwasababu ana nafuu na faida ya kuendelea kubakia" - Dkt. Bashiru Ally, Katibu Mkuu
 
Return Of Undertaker,
Duh...............

Hatimaye wameamua kuukiri ukweli kuwa bila dola hakuna CCM!

Kweli vyama vya upinzani mna kazi ngumu sana kuking'oa hiko chama madarakani.........

Lakini maandiko yamenena Haki huliinua Taifa,na usipotenda haki hakika unajiangamiza

Hao watawala wetu wanapaswa kujifunza kwa kile kilichomtokea Mugabe, ambaye alamini kuwa "State Organs" vipo kumsimamia yeye, lakini ni vyombo hivyo hivyo vya dola ndivyo vilivyomtoa madarakani

Hao CCM wanatenda maovu yote hayo wakiamini kuwa "watabebwa" na Polisi

Lakini ipo siku inakuja hao hao Polisi, watawageuzia kibao na kuwaambia tuacheni tutekeleze majukumu yetu kwa mujibu wa Katiba ya nchi, ambapo tunatakiwa tuwe "neutral"

Hapo ndipo hiko chama kitatamani ardhi ifumuke na wafukiwe ndani kwa kukwepa aibu!
 
Loud and clear! Ujumbe umewafikia walengwa. Mikakati ya vyama vya upinzani ilenge kukusanya (mobilization) nguvu kubwa ya umma ili kupambana na genge hili la Bashiru linalo kiri waziwazi kuwa halina ushawishi kwa wananchi bali linatumia dola kubaki na mamlaka!
 
Ukweli Mchungu.

Sisi wananchi ndio tunaopaswa KUWABALANCE hao WANASIASA na kuhakikisha wanafuata MATAKWA YETU.

Huyo udhaifu wote TUME, TISS, JWTZ, POLICE or Whatever hata akiingia Mbowe hawezi Kuubadili Wakati UNAMPA FAVOR.

Atakachofanya ni kutumia UDHAIFU HUO kugandamiza walio chini yake, tena anaweza kufanya mambo MABAYA NA OVYO Kuliko Hata CCM.

= = =

Mfano Halisi: Waafrika waligandamizwa sana nyakati za ukoloni, walitumia nguvu, jasho na damu kujitoa kwenye makucha ya utumwa mpaka kupata UHURU.

Lakini baada tu ya kupata UHURU, STRUGGLE ikawa imeanza UPYA !

Wakaibuka WAKOLONI WEUSI WAPYA kina IDD AMIN, MOBUTU SESSEKO, BIA, DOS SANTOS, BABANGIDA. Afrika karibia yote ikawa ni VILIO TUPU na matarajio yaliyokuwepo YALIPOTEA.

Watu waliouawa na "wakombozi" weusi ni WENGI SANA. Walioweza wakakimbilia KULE KULE kwa wakoloni weupe tena TULIOWAFUKUZA KUOMBA MSAADA.

Mpaka sasa 21C MTU MWEUSI bado anagambizwa na MTAWALA WEUSI vile vile ANAPAMBANA KUJINASUA.

Suala hili ni WANANCHI TU NDIO W
 
Tatizo la Bashiru ni moja kapewa kazi ya kuwa mtendaji mkuu wa chama lakini yeye mwenyewe hajui siasa. Huu aliousema ni ukweli mchungu. Hakuna ubishi kwa alichokisema labda tu kwa jinsi ulivyowasilishwa..!
 
Back
Top Bottom