• Mpendwa mteja, tunakusihi jitahidi kuosha mikono kwa maji safi na sabuni mara kwa mara na kwa siku chache hizi jaribu kutulia nyumbani kuepusha maambukizi ya #CORONAVIRUS

Dkt Bashiru akabidhi msaada kwa mzee mstaafu Shabani Kanijo

Egnecious

Egnecious

JF-Expert Member
Joined
Jul 8, 2015
Messages
865
Points
1,000
Egnecious

Egnecious

JF-Expert Member
Joined Jul 8, 2015
865 1,000
DKT. BASHIRU AKABIDHI MSAADA KWA MZEE MSTAAFU

05 Februari, 2020

Katika kuadhimisha sikukuu ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi Katibu Mkuu wa CCM Dkt. Bashiru Ally amekabidhi vifaa mbalimbali ikiwemo mashine ya Kuchapa yenye thamani ya shilingi milioni moja na laki tano kwa mzee Shabani Kanijo (73) ambaye ni mstaafu katika kitengo cha Tehama CCM makao Makuu.

Mzee huyo alikuwa ni mtumishi wa CCM (TANU wakati huo) tangu mwaka 1965 na alistaafu mwaka 2004, ambapo baadae alianza kusumbuliwa na maradhi na shughuli zake nyingi za kujipatia kipato zikasimama kwa muda mrefu.

Mapema mwaka huu Mzee Kanijo alifika Ofisi ya Katibu Mkuu kuomba msaada hasa unaohusiana na taaluma yake ili aweze kujimudu na kujiendesha baada ya afya yake kuanza kuimarika, ambapo ombi lake kubwa lilikuwa ni kupata mashine ya kuchapa (Photocopy) kwa ajili ya kufufua steshenari yake iliyokuwa imesimama kwa kipindi chote cha ugonjwa.

Kama ilivyo utaratibu wa Chama Cha Mapinduzi kuwa karibu na makundi mbalimbali ya watu wenye uhitaji wakiwemo wazee, leo tarehe 05 Februari, 2020 Makao Makuu ya CCM Dodoma, Dkt. Bashiru amemkabidhi vifaa vyote vya steshenari ambapo mzee huyo ameishukuru CCM na kueleza kuwa,

“Ninaishukuru sana CCM kwa kuendelea kuwa karibu na sisi wazee, lakini zaidi naipongeza kwa kufanya mambo ambayo wakati wote yalikuwa yakipigiwa kelele na wananchi, sasa hata wapinzania hawana ajenda tena.”

Ameongeza kwa kuuliza kuwa,’’ Hao wapinzania wanataka nini tena? Kama hata wao mambo waliokuwa wanayataka CCM chini ya Rais Magufuli imeyafanya yote.”

Aidha Katibu Mkuu amesisitiza kuwa, ni vema vifaa hivyo ama msaada wowote unaotolewa na Chama utumike kwa malengo yaliotarajiwa na sio vinginevyo ili msaada huo uwe na tija na Chama kiendelee kusaidia wengine zaidi kwa kadri ya uwezo na mahitaji ya wenye uhitaji.

Ikumbukwe kuwa, leo ni siku ya kuzaliwa kwa CCM ambapo Chama hiko kinatimiza miaka 43 tangu kuundwa kwake kutoka vyama vya ukombozi vya TANU na ASP terehe 05 Februari, 1977.

Imetolewa na;
Afisa Habari
Ofisi ya Katibu Mkuu
CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)
2297033_IMG-20200205-WA0005.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
K

kigogo warioba

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2015
Messages
5,064
Points
2,000
K

kigogo warioba

JF-Expert Member
Joined Jul 11, 2015
5,064 2,000
sasa badala wampe fungu la kutosha mzee wa watu alieipigania ccm mpaka kazeeka, wanampa vitendea kazi! sasa kwa uzee huo si atatapeliwa na mitoto yake?
 
Waterloo

Waterloo

JF-Expert Member
Joined
Nov 30, 2010
Messages
18,261
Points
2,000
Waterloo

Waterloo

JF-Expert Member
Joined Nov 30, 2010
18,261 2,000
Hii mngepeleka kwenye gazeti la Uhuru na mzalendo hapasiyo mahala pake.
 

Forum statistics

Threads 1,405,217
Members 531,945
Posts 34,481,056
Top