Dkt. Antony Dialo: Wizi na ukosefu auminifu chanzo cha biashara nyingi Tanzania kufa chini ya miaka 5 tangu kuanza

Rutunga M

JF-Expert Member
Mar 16, 2009
1,769
1,382
Nimemsikiliza asubuhi. Mkurugenzi wa Saharama media wakati akitoa mada katika club house moja iitwayo Mindset transformation. Akidai kuwa kwa uzoefu wake katika biashara na ujasirimali amebaini kuwa biashara nyingi zinakufa kwa sababu watazania wengi siyo waaminifu.

Amekwenda mbali na kusema kuwa wenye miradi wanatumia muda mwingi kushugulika wasiibiwe kuliko kushugulikia uendelevu wa miradi.

Ameeleza kuwa kupitia utafiti alioupata wakati akisaka PHD yake alibaini kuwa watu waaminifu kwa tanzania ni wapemba.

Msiklize kidogo hapa chini

Dialo-watz siyo waaminifu

Mjadala utaendelea kesho katika club hiyo hiyo hapo chini. kuanzia saa 12 asubuhi

MINDSET TRANSFORMATION
 
Wala hakuongopa.

Wizi upo damuni mwa mtanzania.

Awe amesoma au hakusoma.

Awe ameelimika au hakuelimika mtanzania anawaza wizi tu.

Na usipokuwa mwizi ukiwa muadilifu utaambiwa uache ujinga ujiongeze.

Ukimuajiri kijana akuuzie duka usipokuwa makini lako linakufa unalifunga yeye anakwenda kufungua lake kupitia pesa zako alizokuibia wakati anakuuzia dukani kwako.

Nchi ngumu sana hii.
 
Kweli kabisa
Hata umweke mkeo ataiba wakati ni biashara yenu
 
Sio wapemba TU,
Watu wengi wenye misimamo mikali ya imani ya kiislamu ni waaminifu Sana.

Nenda Kariakoo,
Biashara nyingi zinazouzwa na wale waislamu swala 5 kiukweli sijawahi dhulumiwa.
 
Sio wapemba TU,
Watu wengi wenye misimamo mikali ya imani ya kiislamu ni waaminifu Sana.

Nenda Kariakoo,
Biashara nyingi zinazouzwa na wale waislamu swala 5 kiukweli sijawahi dhulumiwa.
Wavaa kobazi..ni majini tu..ila wanao run show ni wachaga na wakinga.

#MaendeleoHayanaChama
 
Back
Top Bottom