kifupi kirefu
JF-Expert Member
- Oct 29, 2018
- 539
- 3,507
Katika utawala wa JPM mwanamke aliyekabidhiwa kazi ngumu na akaimudu bila kujitutumua au kuonyesha ule uwanawake au kuonyesha kukwamishwa na mfumo dume ni Kamishna Jenerali wa Uahamiaji Dkt. Anna Makakala.
Nikiangalia taasisi anayoongoza hatua ilizopiga kwenye huduma, nikifuatilia kauli zake mbele ya vyombo vya habari na nikiangalia idadi ya malalamiko ya raia dhidi yake nataka nisema wanawake wanaweza.
Kwa mwonekano huyu Mama inaonyesha aliteuliwa akiwa bado mdogo sana, nadhani Hadi Sasa Hana miaka 50 lakini amesimama imara sana. Kuongoza vyombo vya dola ndani ya mkikimkiki wa JPM ukatoka bila kutunishiana misuli na wananchi ni busara kubwa sana.
Niliona tuhuma nyingi za uraia zikifikishwa kwake lakini sijawahi msikia akitoka adharani kutoa kauli zakutisha, always hoja zimekuwa zikijibiwa na wasaidizi wake hii ikiwa ni njia yakuepusha kuichafua taasisi.
Nimwombe mama Samia Suluhu, Rais wa Jamuhuri ya Muungano ya Tanzania ajipe muda kuibua akina Makakala wengi watakaomsaidia.
Hongera Makakala, umefanya kwa sehemu kubwa na umevuka salama endelea na busara hiyo hiyo kwa utumishi wako ndani na nje ya Idara ya Uhamiaji.