#COVID19 Dkt. Akwilapo: Kwanini wathibiti Ubora wa Elimu Mashuleni hamvai barakoa?

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,806
11,968
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo ameshangaa kuona watu kwenye Mafunzo na Semina Wizara ya Elimu hawavai Barakoa wala kufuata kanuni za afya za kujikinga na Covid-19.

Ameonge hayo wakati akifungua Mafunzo ya Uthibiti Ubora kwa Maafisa Elimu Kata na Wakuu wa Shule katika Shule ya Msingi Mnazi mmoja. "Kwanini hamjavaa Barakoa na hamtumii Vitakasa Mikono, Mnadhani Corona haipo? Amehoji Akwilapo.

IMG-20211207-WA0014.jpg

Dkt. Leonard Akwilapo ametoa Maelekezo kwa Mafunzo na Semina zinazoendelea Nchini, Wahakikishe Wanafuata Taratibu zote za Afya za kujikinga na Maambukizi ya Corona sababu bado ipo. "Usalama wa afya kwanza" Amesema.

Dkt. Leonard Akwilapo amewagiza Wathibiti ubora wa Elimu kuhakikisha. Shule zinazingatia ratiba za kufunga na kufungua shule, Kamishina wa Elimu ndo Sheria imempa mamlaka ya kupanga Ratiba sio Mwanasia, au mtu yoyote. Amedia sasa hivi Shule zinaendeshwa ovyo ovyo kwani kila Shule inajipangia itakavyo.

Dkt. Leonard Akwilapo amesema Makuzi, malezi na Maendeleo ya mtoto kitaaluma, yanazingatia Vitu vingi. Kuna wakati Mtoto anatakiwa acheze, asome na apumzike. Lakini siku hizi Watoto Wanaamshwa saa kumi usiku wanaingizwa darasani kusoma, Mtoto hapati Muda wa kupumzika wala Kucheza. Watoto wanapigwa Viboko bila huruma. Hivyo ameagiza Wadhibiti ubora wa Elimu kulifanyia kazi. "Mafunzo haya yawe Chachu na ufanisi katika shughuli zenu za udhibiti Ubora". Amesema Dkt. Akwilapo.

"Kupitia hadhira hii nawaagiza maofisa uthibiti kipindi hiki cha likizo hakikisheni mnafanya msako kuwabaini wanaokiuka agizo hili la Serikali la kuwataka watoto wapumzike na katika kuweka msisitizo hilo tutazipa barua shule zote," amesema Katibu huyo.

IMG-20211207-WA0006.jpg

Naye Mkurugenzi wa uthibiti ubora Wizara ya Elimu Euphrasia Buchuma amesema Awamu ya kwanza elimu wakuu shule za msingi Nchi nzima 8096, Maafisa elimu Mkoa 26 Maafisa elimu taaluma 26 Maafisa elimu Wilaya wa shule za Msingi 180. Awamu ya pili wametoa Mafunzo kwa Waalimu Wakuu 7, 679 Nchi nzima Isipokuwa shule mpya. Pia Wametoa Mafunzo kwa Waratibu Elimu kata 3, 901 Vipo Vituo 164 Nchi nzima ambavyo vinatoa mafunzo hayo.

Euphrasia amesema Wakaguzi wa Shule sasa Wanaitwa Wadhibiti Ubora.

IMG-20211207-WA0028.jpg
IMG-20211207-WA0023.jpg
IMG-20211207-WA0021.jpg
IMG-20211207-WA0019.jpg
IMG-20211207-WA0017.jpg
IMG-20211207-WA0016.jpg
IMG-20211207-WA0008.jpg

IMG-20211207-WA0010.jpg

IMG_20211207_115341_455.jpg

IMG_20211207_091806_680~5.jpg
Dar es Salaam.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dk Leonard Akwilapo ametoa agizo kwa wathibiti wa ndani wa elimu nchini kufanya msako kwa watakaosomesha wanafunzi kipindi cha likizo.

Pia, Dk Leonard Akwilapo amesema kutatolewa kutatolewa barua kwa shule zote sa Serikali na binafsi kuweka msisitizo wa utekelezaji wa agizo hilo ambalo hivi karibuni Serikali ililitoa.

Hivi karibuni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Tamisemi), Ummy Mwalimu alisema kuwa wakati wa likizo wanafunzi wasisome bali wapumzike.

Leo Jumanne Desemba 7, 2021 alipokuwa akifungua mafunzo ya uthibiti wa ndani kwa maofisa elimu kata na walimu wakuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Dk Akwilapo amebainisha kuwa wathibiti wa ndani wa elimu nchini watafanya msako kuwabaini watakaofundisha wanafunzi wakati wa likizo.

Amesema maofisa elimu hao wamesoma somo la saikolojia na wanajua umuhimu wa mapumziko katika makuzi ya mtoto hivyo hawapaswi kufungia macho vitendo hivi.

"Kupitia hadhira hii nawaagiza maofisa udhibiti kipindi hiki cha likizo hakikisheni mnafanya msako kuwabaini wanaokiuka agizo hili la Serikali la kuwataka watoto wapumzike na katika kuweka msisitizo hilo tutazipa barua shule zote," amesema Katibu huyo.

"Ni muhimu kufuata ratiba za mihula ya masomo kwani kumeibuka siku hizi makamishna wengi wa elimu huko mashuleni mpaka wanasiasa, nasema kamishna ni mmoja tu wa elimu nchi hii anayepanga ratiba za masomo, hivyo ni vema ikafuatwa,"amesisitiza Katibu huyo.

Amesema hata tabia ya kuwaamsha watoto saa kumi usiku kusoma sio sawa na badala yake wanajikuta wanakariri badala ya kutafakari kile walichofundishwa
 
Last edited:
Msako waja kwa watakaosomesha wanafunzi likizo

Dar es Salaam. Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dk Leonard Akwilapo ametoa agizo kwa wathibiti wa ndani wa elimu nchini kufanya msako kwa watakaosomesha wanafunzi kipindi cha likizo.

Pia, Dk Leonard Akwilapo amesema kutatolewa kutatolewa barua kwa shule zote sa Serikali na binafsi kuweka msisitizo wa utekelezaji wa agizo hilo ambalo hivi karibuni Serikali ililitoa.

"Kupitia hadhira hii nawaagiza maofisa udhibiti kipindi hiki cha likizo hakikisheni mnafanya msako kuwabaini wanaokiuka agizo hili la Serikali la kuwataka watoto wapumzike na katika kuweka msisitizo hilo tutazipa barua shule zote," amesema Katibu huyo.

"Ni muhimu kufuata ratiba za mihula ya masomo kwani kumeibuka siku hizi makamishna wengi wa elimu huko mashuleni mpaka wanasiasa, nasema kamishna ni mmoja tu wa elimu nchi hii anayepanga ratiba za masomo, hivyo ni vema ikafuatwa,"amesisitiza Katibu huyo.

Amesema hata tabia ya kuwaamsha watoto saa kumi usiku kusoma sio sawa na badala yake wanajikuta wanakariri badala ya kutafakari kile walichofundishwa.

My Take
Sina shida na hoja ya serikali. Kero yangu ni kwa nini iwe lazima mpaka kwa mtu binafsi na mwanae? Kwani mwanangu akitwishwa mzigo wakati wa likizo mnapungukiwa nini?
Haya mahaba kwa nini msiyaonyeshe kwenye kuajiri walimu wa kutosha mpaka kusaza.

Darasa moja wanafunzi 100 kuna nini hapo? Vipi na sisi wazazi tuanzishe msako kwa waziri kuhusu watoto wetu 100 kujazana darasa 1?

Sisi tulioponea tuisheni tunajua unyeti wake. Kuna shule hazina kabisa walimu kwa baadhi ya masomo,inabidi ukasome tuisheni. Kuna hawa A Level mambo kibao mazito muda mchache,kwa government bila tuisheni hutoboi

Au kuna ajenda ya siri?
 
Kwa kweli kuna shida kabisa shule za serikali bila masomo ya ziada mwanafunzi hawezi pata chochote na kama wana uchungu namna hiyo kwanini wasiongeze walimu shuleni kwa ajili ya kuwasaidia watoto kipindi cha masomo walimu hawafundishi wazazi tunafuatilia maendeleo yao hadi shuleni lakini ni mameno matupu na siku hizi hata mithiani yao wanayoifanya hawapewi matokeo wakati hicho ndo kipimo kwa wanafunzi na wazazi mzazi akiona mtoto anafanya vibaya somo fulani (kwenye matokeo ya mthiani) ataangalia ni namna gani amsadie (Hatuutaki huo upendo wao wafanye kitu kingine) hii ni nchi huru sio jela au tuambiwe sasa watakuja kutupangia ni lini na lini tutakuwa tuna lala na wake zetu naona hilo kwa mbaali
 
mi naiunga serikali mkono asilimia 100,

yaani watu sijui wakoje? yaani mnatafuta visingizio hata kwa mtu ambaye anasomesha mtot shule iliyomaliza sylubus (utasikia mtoto asikae tu )

kwanza mi nakuambia , hao watu waliopata degree na masters degrees kwa kusoma 24/7 hata wakipewa ofices, wanakuwa sio wabunifu, kila kitu anataka kutumia nguvu na sio akili

ndo hao utawasikia'' basi ukitoka kanisani nitafute kuna jambo la haraka sana'' yaani anashindwa kuelewa kuwa hata kumtaka mtu afanye kazi siku ya mapumziko ni ishara kwamba wewe mwenyewe ambaye unajidhani ni '' boss'' haujajipanga vizuri.

Serikali haijapinga vituo binafsi vya tuition, manotaka watoto wenu wakae wansoma masaa 24 , wapelekeni. ila taasisi RASMI zisilamishe watu, maana bila kufanya hivyo, watu wanatumia mwanya kuendeleza hiyo suala la kusoma vitabu 24/7

afu jamani wote tumesoma, kipindi cha likizo , mtu unaamua, niksoma tuition gani, wapi na masomo gani, kuanzia labda saa 4 hadi saa 7 mwisho. yaani najipangia mwenyewe

lakini hii ya kuamrishwa , sijui shule hamna kufunga , afu hata kubadilisha mazingira ya shule kichwa kinafurahi jamani
 
Dar es Salaam.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dk Leonard Akwilapo ametoa agizo kwa wathibiti wa ndani wa elimu nchini kufanya msako kwa watakaosomesha wanafunzi kipindi cha likizo.

Pia, Dk Leonard Akwilapo amesema kutatolewa kutatolewa barua kwa shule zote sa Serikali na binafsi kuweka msisitizo wa utekelezaji wa agizo hilo ambalo hivi karibuni Serikali ililitoa.

Hivi karibuni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Tamisemi), Ummy Mwalimu alisema kuwa wakati wa likizo wanafunzi wasisome bali wapumzike.

Leo Jumanne Desemba 7, 2021 alipokuwa akifungua mafunzo ya uthibiti wa ndani kwa maofisa elimu kata na walimu wakuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Dk Akwilapo amebainisha kuwa wathibiti wa ndani wa elimu nchini watafanya msako kuwabaini watakaofundisha wanafunzi wakati wa likizo.

Amesema maofisa elimu hao wamesoma somo la saikolojia na wanajua umuhimu wa mapumziko katika makuzi ya mtoto hivyo hawapaswi kufungia macho vitendo hivi.

"Kupitia hadhira hii nawaagiza maofisa udhibiti kipindi hiki cha likizo hakikisheni mnafanya msako kuwabaini wanaokiuka agizo hili la Serikali la kuwataka watoto wapumzike na katika kuweka msisitizo hilo tutazipa barua shule zote," amesema Katibu huyo.

"Ni muhimu kufuata ratiba za mihula ya masomo kwani kumeibuka siku hizi makamishna wengi wa elimu huko mashuleni mpaka wanasiasa, nasema kamishna ni mmoja tu wa elimu nchi hii anayepanga ratiba za masomo, hivyo ni vema ikafuatwa,"amesisitiza Katibu huyo.

Amesema hata tabia ya kuwaamsha watoto saa kumi usiku kusoma sio sawa na badala yake wanajikuta wanakariri badala ya kutafakari kile walichofundishwa

Mwananchi
 
Daah watoto wao wanasoma shule nzuri, mitaala inaisha kabla hata ya mihula kuisha.

Wanetu wanasoma St Kayumbas, kumaliza mitaala huwa ni ndoto.

Lakini wanatuzuia tuwasaidie japo na wao wamalize mitaala.

Hivi ni nini hiki serikali hasa hasa wizara ya elimu inafanya?
 
Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dk Leonard Akwilapo ametoa agizo kwa wathibiti wa ndani wa elimu nchini kufanya msako kwa watakaosomesha wanafunzi kipindi cha likizo.

Pia, Dk Leonard Akwilapo amesema kutatolewa kutatolewa barua kwa shule zote sa Serikali na binafsi kuweka msisitizo wa utekelezaji wa agizo hilo

Mwananchi
Heee hadi private
 
Daah watoto wao wanasoma shule nzuri, mitaala inaisha kabla hata ya mihula kuisha.

Wanetu wanasoma St Kayumbas, kumaliza mitaala huwa ni ndoto.

Lakini wanatuzuia tuwasaidie japo na wao wamalize mitaala.

Hivi ni nini hiki serikali hasa hasa wizara ya elimu inafanya?
Kwani watoto wa Kayumba wanaformat tofauti ya kimasomo? Walimu wengine ni wazembe tuache kubisha
 
mi naiunga serikali mkono asilimia 100,
yaani watu sijui wakoje ??? yaani mnatafuta visingizio hata kwa mtu ambaye anasomesha mtot shule iliyomaliza sylubus (utasikia mtoto asikae tu !! )
kwanza mi nakuambia , hao watu waliopata degree na masters degrees kwa kusoma 24/7 hata wakipewa ofices, wanakuwa sio wabunifu, kila kitu anataka kutumia nguvu na sio akili
ndo hao utawasikia'' basi ukitoka kanisani nitafute kuna jambo la haraka sana'' yaani anashindwa kuelewa kuwa hata kumtaka mtu afanye kazi siku ya mapumziko ni ishara kwamba wewe mwenyewe ambaye unajidhani ni '' boss'' haujajipanga vizuri.
Serikali haijapinga vituo binafsi vya tuition, manotaka watoto wenu wakae wansoma masaa 24 , wapelekeni. ila taasisi RASMI zisilamishe watu, maana bila kufanya hivyo, watu wanatumia mwanya kuendeleza hiyo suala la kusoma vitabu 24/7
afu jamani wote tumesoma, kipindi cha likizo , mtu unaamua, niksoma tuition gani, wapi na masomo gani, kuanzia labda saa 4 hadi saa 7 mwisho. yaani najipangia mwenyewe ,
lakini hii ya kuamrishwa , sijui shule hamna kufunga , afu hata kubadilisha mazingira ya shule kichwa kinafurahi jamani
Shida hapa inaanzia kwenye lundo la masomo na mfumo mzima wa elimu ya bongo. Kinaachaliwa cheti,kila ngazi inadahiliwa kwa ufaulu mzuri. Wabadili system ili hicho unachotaka kifanye kazi
 
Back
Top Bottom