Dkt. Abdallah Possi alijiuzulu Ubunge mara baada ya kuteuliwa kuwa Balozi. Polepole atajiuzulu?

Mkuu hawezi kuiacha hiyo nafasi labda aikatae na aondoke nchini, vinginevyo ataonekana msaliti na anataka kuleta taharuki.

So huyu ndg kesho atavaa kaunda suite yake ya brown au nyeusi na ataenda kula kiapo mapema sana.

Although nitasikitishwa endapo kapewa hiyo nafasi ili kumfunga mdomo na baadaye kumtupa nje kisiasa, itakuwa nia ile ile ya kuwavunja miguu omba omba wakati huna uwezo wa kuwapa msaada.
Unajua watu wengi huwa wanadhani kuwa hujuma kwa nchi mpaka tu mtu aisababishie nchi hasara kubwa ya kifedha au apange shambulio la ajabu; siyo kweli!
 
So huyu ndg kesho atavaa kaunda suite yake ya brown au nyeusi na ataenda kula kiapo mapema sana.
Hii ndiyo dress code mteule anapokwenda kuapishwa kama balozi, au? Kama ni ndiyo basi sikuwahi kulijua hilo!
 
Hakutakiwa kuteuliwa Nohodha kabla ya polepole kujiuzulu
Mama bado anazo nafasi zake za kutosha kwa wabunge wa kuteuliwa na hivyo halazimiki kusubiri mmoja ajiuzulu kwanza halafu ndiyo ateue mwingine. Atakayojiuzulu Polepole itajazwa na mtu mwingine. Ya Nahodha nayo ni nafasi nyingine tofauti na ile atakayojiuzulu Polepole
 
Dar es Salaam. Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu aliyekuwa akishughulikia Walemavu, Dkt. Abdallah Possi amemuandikia Spika wa Bunge barua ya kujiuzulu.

Uamuzi huo wa Dkt. Possi umekuja siku tatu baada ya Rais John Magufuli kumteua kuwa balozi.

Spika wa Bunge, Job Ndugai alithibitisha kupokea barua ya kujiuzulu ya mbunge huyo jana na kueleza kuwa nafasi yake imebaki wazi.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Bunge, Spika Ndugai tayari amemuandikia barua Rais kumfahamisha juu ya kujiuzulu kwa Dk Possi kama mbunge wa kuteuliwa.

Polepole utajiuzulu au nawe utaandikuwa Barua kama Mh Job Ndugai alivyoandikiwa!
Si ingekuwa bora zaidi kusema kanuni zinasemaje kuliko kukariri alivyofanya mmoja kama vile kitendo cha huyo mmoja ndiyo kimeweka sheria ya kufuata.
 
Dkt.Joni ni hivi.

Rais anaweza kuteuwa wabunge wa kuteuliwa kumi kwa mujibu wa katiba ila hana uwezo wa kutengua.

Mpaka leo hii Rais ameshateua wabunge 11.Ilibidi Pole pole ajiuzulu ubunge kabla ya kuteua mbunge mwingine.

Je Polepole akigoma kujiuzulu itakuwaje??

Tanzania tuna mamlaka, hatuna Katiba.
 
Mbona kipindi cha jpm, kuna jamaa alikata u DC!!na duniani kote mbona watu wanakataa teuzi, huku kwetu ni nadra kutokana na njaa!!
Namkumbuka, yule alikuwa raia wa kawaida tena mfanyakazi wa Tigo.

Polepole sio raia wa kawaida, ameteuliwa kisiasa, na lazima aende. Akikataa, anajua gharama yake.
 
Wahuni ndiyo anawajua sasa, ubalozi wenyewe aweza dumu mwaka, akarudishwa kujaa kukaa benchi, huku wenzake wakila mema ya nchi!
Eeeeh muosha akioshwa!
Polepole hakujua kuwa wahuni ndio walioshika mpini.......kwa kifupi Polepole ameondolewa kisayansi.....
 
Nchi wakati wa JPM ilikuwa inaendeshwa kihunihuni tu pamoja na huyo Ndugai wake utenguliwaji wa posi ilikuwa hivi:

Kwa mjibu wa katiba rais ana uwezo wa kuteuwa wabunge wa kuteuliwa 10 tu, kwa bahati mbaya au bila kujua Rais alifanya uteuzi wa mbunge mwingine ikawa wabunge wa kuteuliwa wakawa 11 na hapo hapo kushituliwa kwamba kavunja katiba, papo hapo akatengua uteuzi wa A. possi wa uwaziri na kushauriwa ajihuzuru ubunge na baadae kulamba ubalozi wa UGERUMANI.
Katiba inaruhusu kuteua wabunge kumi ila kipindi Cha JPM wabunge walikuwa hwajafika kumi ila Katiba inataka angalau wabunge nusu yake wawe wanawake hivyo akawa ameshateua wabunge sita wakiume hivyo ikawa raised ndo akamteua poss kuwa baloz
 
Kwani kuitwa balozi ilhali wallet haina pesa kuna faida gani? Ubunge unalipa kuliko ubalozi.
Mkuu mbunge hamfikii Balozi kwa lolote
Hadhi
Mkwanja
Mafao baada ya kustaafu

Balozi ataendelea kulipwa 80% ya stahiki zake zote hadi siku anaingia kaburini

Sema kisiasa na kwa hulka ya polepole ni kama wanampoteza kiaina
 
Kikatiba Rais hana mamlaka ya kutengua uteuzi wa mbunge aliyemteua

Namna nzuri ndio hii sasa
Unatupiwa fupa la ubalozi ili utoke mwenyewe kisha baada ya mwaka unatemwa mazima
Wahuni sio watu wazuri kabisaa
 
Kikatiba Rais hana mamlaka ya kutengua uteuzi wa mbunge aliyemteua

Namna nzuri ndio hii sasa
Unatupiwa fupa la ubalozi ili utoke mwenyewe kisha baada ya mwaka unatemwa mazima
Wahuni sio watu wazuri kabisaa
HYo Katiba bado ina matobo ndo maana watawala wanaitumia vizur kufanya siasa. Hya hawez tengua Hpo kafanya nini kma si kumtengua?? Lazma uangalie kwa jicho la tatu...
 
Back
Top Bottom