Dkt. Abbas wafungieni Prime Time kwa ujinga wa Fally Ipupa kukanyaga fedha yetu. Serikali itoe tamko kali

Rufiji dam

JF-Expert Member
Feb 20, 2020
3,767
8,683
Nalaani kwa mara nyingine tena kitendo cha Fally Ipupa (msanii wa muziki kutoka DRC) kudharau, kupuuza na kufedhehesha sarafu yetu hadharani/jukwaani.

Alipofanya kitendo hicho mara ya kwanza akiwa Dar es Salaam, niliandika na kulaani sana.

Nilitarajia waandaji wa maonesho yake wangemuonya na kumkemea kuhusu tabia yake hiyo ya utovu wa nidhamu. Hawakufanya hivyo, na kitendo kilekile amekirudia tena akiwa jijini Mwanza safari hii kwa dharau kubwa zaidi.

Pamoja na matumizi yanayoeleweka, sarafu (currency) ni sehemu ya nembo, alama na utambulisho wa taifa letu. Sarafu (iwe ya noti , shaba, au silver nk) ni sehemu ya TUNU za taifa! Kitendo cha kuidhalilisha sarafu ya nchi hadharani (kama alivyofanya Fally Ipupa), ni kulidhalilisha taifa!

Miaka ya 60, raia mmoja wa Uingereza alionekana akichana hela (noti ) ya Tanzania akiwa uwanja wa ndege akijiandaa kuondoka, alikamatwa na kuchukuliwa hatua stahiki.

Pale Mwanza, Fally Ipupa akiwa jukwaani kwa kutumia mguu wake anaonekana akizisukumiza (mithili ya taka) noti mchanganyiko alizokuwa ametuzwa na mashabiki wake ukumbini. Kitendo hicho amekifanya kwa dharau kubwa mno!

Katika noti zile zilizosukumwa kwa mguu na Fally Ipupa, ilikuwemo noti ya shilingi 1000 ambayo kwa heshima ina picha ya baba wa taifa hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambaye leo tarehe 14/10/2021 tunaadhimisha miaka 22 ya kifo chake.

Kwa nchi inayoheshimu mila, tamaduni, na desturi zake, Fally Ipupa ama angekuwa mahabusu au ndani ya gari la polisi akiwa ametiwa pingu mikononi akipelekwa uwanja wa ndege kurudishwa kwao kwa nguvu (repatriation).

Kanda Bongoman alijaribu kuleta dharau zake pale Kenya miaka ya 90), alishushwa kwa nguvu akiwa jukwaani na kuamriwa kuondoka haraka kurudi kwao!
Koffi olomide alidhani yuko ‘’Aeroport Ndjili ‘’(uwanja wa ndege wa Kinshasa) kumbe yuko uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta (Kenya), akafanya upumbavu wake pale! Wakenya hawakuangalia umaarufu wake au wingi wa mvi zake kichwani na kidevuni, akapigwa pingu na kurudishwa kwao! Upumbavu wake akafanyie hukohuko kwao!

Naomba mamlaka zinazohusika zimchukulie hatua kali Fally Ipupa na wote walioandaa maonyesho yake yote. Na Fally Ipupa apigwe marufuku kufanya maonyesho Tanzania, dharau zake akazifanyie hukohuko kwao Congo-Kinshasa.
FB_IMG_1634277050172.jpg
 
acha ujinga wewe amekanyaga amezisogeza we hukuona hiyo video alikua kama anazikusanya kisha akaja jamaa akazichukua ni baada ya yule bidada aliyecheza naye kuupiga mwingi,

Upuuzi wa sijui hela imekanyagwa sijui nini ni huku kwenye nchi zetu masikini tu otherwise ni ushamba unakusumbua mleta uzi, fally ana hela za kutosha na tunamwita kila mara kwa mahaba yetu wala hatuhitaji anaishi ufaransa na DRC
 
Nalaani kwa mara nyingine tena kitendo cha Fally Ipupa (msanii wa muziki kutoka DRC) kudharau, kupuuza na kufedhehesha sarafu yetu hadharani/jukwaani
Hilo ni kosa la jinai. Huenda hakuna mlalamikaji. Nenda kituo cha polisi cha karibu utoe malalamiko yako
 
acha ujinga wewe amekanyaga amezisogeza we hukuona hiyo video alikua kama anazikusanya kisha akaja jamaa akazichukua ni baada ya yule bidada aliyecheza naye kuupiga mwingi, upuuzi wa sijui hela imekanyagwa sijui nini ni huku kwenye nchi zetu masikini tu otherwise ni ushamba unakusumbua mleta uzi, fally ana hela za kutosha na tunamwita kila mara kwa mahaba yetu wala hatuhitaji anaishi ufaransa na DRC
Ujinga wangu ama wewe tafuta ya onyesho la Mwanza halafu uje ukenue mdomo hapa.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom