Dkt. Abbas wafungieni Prime Time kwa ujinga wa Fally Ipupa kukanyaga fedha yetu. Serikali itoe tamko kali

Rufiji dam

JF-Expert Member
Feb 20, 2020
2,012
2,000
Nalaani kwa mara nyingine tena kitendo cha Fally Ipupa (msanii wa muziki kutoka DRC) kudharau, kupuuza na kufedhehesha sarafu yetu hadharani/jukwaani.

Alipofanya kitendo hicho mara ya kwanza akiwa Dar es Salaam, niliandika na kulaani sana.

Nilitarajia waandaji wa maonesho yake wangemuonya na kumkemea kuhusu tabia yake hiyo ya utovu wa nidhamu. Hawakufanya hivyo, na kitendo kilekile amekirudia tena akiwa jijini Mwanza safari hii kwa dharau kubwa zaidi.

Pamoja na matumizi yanayoeleweka, sarafu (currency) ni sehemu ya nembo, alama na utambulisho wa taifa letu. Sarafu (iwe ya noti , shaba, au silver nk) ni sehemu ya TUNU za taifa! Kitendo cha kuidhalilisha sarafu ya nchi hadharani (kama alivyofanya Fally Ipupa), ni kulidhalilisha taifa!

Miaka ya 60, raia mmoja wa Uingereza alionekana akichana hela (noti ) ya Tanzania akiwa uwanja wa ndege akijiandaa kuondoka, alikamatwa na kuchukuliwa hatua stahiki.

Pale Mwanza, Fally Ipupa akiwa jukwaani kwa kutumia mguu wake anaonekana akizisukumiza (mithili ya taka) noti mchanganyiko alizokuwa ametuzwa na mashabiki wake ukumbini. Kitendo hicho amekifanya kwa dharau kubwa mno!

Katika noti zile zilizosukumwa kwa mguu na Fally Ipupa, ilikuwemo noti ya shilingi 1000 ambayo kwa heshima ina picha ya baba wa taifa hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambaye leo tarehe 14/10/2021 tunaadhimisha miaka 22 ya kifo chake.

Kwa nchi inayoheshimu mila, tamaduni, na desturi zake, Fally Ipupa ama angekuwa mahabusu au ndani ya gari la polisi akiwa ametiwa pingu mikononi akipelekwa uwanja wa ndege kurudishwa kwao kwa nguvu (repatriation).

Kanda Bongoman alijaribu kuleta dharau zake pale Kenya miaka ya 90), alishushwa kwa nguvu akiwa jukwaani na kuamriwa kuondoka haraka kurudi kwao!
Koffi olomide alidhani yuko ‘’Aeroport Ndjili ‘’(uwanja wa ndege wa Kinshasa) kumbe yuko uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta (Kenya), akafanya upumbavu wake pale! Wakenya hawakuangalia umaarufu wake au wingi wa mvi zake kichwani na kidevuni, akapigwa pingu na kurudishwa kwao! Upumbavu wake akafanyie hukohuko kwao!

Naomba mamlaka zinazohusika zimchukulie hatua kali Fally Ipupa na wote walioandaa maonyesho yake yote. Na Fally Ipupa apigwe marufuku kufanya maonyesho Tanzania, dharau zake akazifanyie hukohuko kwao Congo-Kinshasa.
FB_IMG_1634277050172.jpg
 

Janja weed

JF-Expert Member
Nov 20, 2020
1,333
2,000
acha ujinga wewe amekanyaga amezisogeza we hukuona hiyo video alikua kama anazikusanya kisha akaja jamaa akazichukua ni baada ya yule bidada aliyecheza naye kuupiga mwingi,

Upuuzi wa sijui hela imekanyagwa sijui nini ni huku kwenye nchi zetu masikini tu otherwise ni ushamba unakusumbua mleta uzi, fally ana hela za kutosha na tunamwita kila mara kwa mahaba yetu wala hatuhitaji anaishi ufaransa na DRC
 

mwandiga

JF-Expert Member
Dec 5, 2011
1,504
2,000
Nalaani kwa mara nyingine tena kitendo cha Fally Ipupa (msanii wa muziki kutoka DRC) kudharau, kupuuza na kufedhehesha sarafu yetu hadharani/jukwaani
Hilo ni kosa la jinai. Huenda hakuna mlalamikaji. Nenda kituo cha polisi cha karibu utoe malalamiko yako
 

Rufiji dam

JF-Expert Member
Feb 20, 2020
2,012
2,000
acha ujinga wewe amekanyaga amezisogeza we hukuona hiyo video alikua kama anazikusanya kisha akaja jamaa akazichukua ni baada ya yule bidada aliyecheza naye kuupiga mwingi, upuuzi wa sijui hela imekanyagwa sijui nini ni huku kwenye nchi zetu masikini tu otherwise ni ushamba unakusumbua mleta uzi, fally ana hela za kutosha na tunamwita kila mara kwa mahaba yetu wala hatuhitaji anaishi ufaransa na DRC
Ujinga wangu ama wewe tafuta ya onyesho la Mwanza halafu uje ukenue mdomo hapa.
 

Rufiji dam

JF-Expert Member
Feb 20, 2020
2,012
2,000
akanyage anavyoweza...

hii mambo ya kuweka emotions kwenye vitu hasa vitu vya kipumbavu wanasiasa wanavyokwambia uvipende kwa niaba yao ni usenge..
Umeshatumia lugha ambayo haina afya acha waje wenye kujua kutumia kauli kama yako nafunga mjadala rasmi na wewe.
 

Janja weed

JF-Expert Member
Nov 20, 2020
1,333
2,000
akanyage anavyoweza...

hii mambo ya kuweka emotions kwenye vitu hasa vitu vya kipumbavu wanasiasa wanavyokwambia uvipende kwa niaba yao ni usenge

Uzalendo ni usenge wa wanasiasa tuisaidie serikali kazi zake

Wewe hukutakiwa kuongea chochote,serikali ndio inawajibika kua emotional na kumtafuta huyo Ipupa

Cha ajabu wewe ndio unaisaidia serikali kua emotion on its behalf,huna kazi kufanya?

Cha ajabu mtoto wako au ndugu yako akiumwa au chochote haupo emotional namna hii...useless human beings!

Weka mpaka wako na serikali....serikali ni another person,unaisaidia kulia wakati ingetakiwa ilie yenyewe huko

Wewe hela zako?Au kimbelembele tu?Unachapa hela wewe?Ni mali za serikali sio zako,ila upo hapa unatujazia server tu kuisaidia serikali kulia...mawananchi sometimes hua majinga sana
mwambie mkuu , maana naona katoka povu kweli kisa hela ya madafu sijui nini, nakwambia prof Asaad aliposema kuna vichaa wengi hakukosea maana anaona tunavyohangaina na mambo ya ajabu ajabu, utakuta hata hela ya bando ana unga unga sijui tukoje yaani
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom