Dkt. Abbas, unapigwa changa la macho juu ya Makandarasi wa Maji

Umemaliza kila kitu Mkuu Jidu La Mabambasi 👏👏👏

Tutaongea vyote lakini tatizo liko pale pale, Ucheleweshaji wa malipo.

Tatizo la Wizara ya Maji inaidhinishiwa Bajeti na Bunge labda 820B lakini zinazotolewa hazizidi 300B, mwisho wa siku lawama zinakwenda kwa Watendaji eti Vilaza.
Wanadhani utatumika muujiza gani kutekeleza miradi pasipo na fedha kutolewa kwa wakati?

Zamani wasimamizi wa miradi walikuwa wanapewa hela ya kusimamia ~Supervision siku hizi unakuta hakuna hela za Supervision wanapata, inafikia muda Project Manager hawezi kwenda site kwa kukosa Dizeli au hata Usafiri. Kwa muktadha huu ni ngumu kupata matokeo Chanya kwenye Sekta.

Ukitaka kuona hili angalia miradi ya Tanroads, unakuta jamaa wana magali hata 3 kwenye mradi mmoja then angalia ya Maji uone kichekesho.

Me nadhani matatizo ya Sekta ya Maji yanatengenezwa kutoisha ili kuwafanya Watawala waendelee kupata Kura za kwenye Chaguzi zao.
Kweli kabisa mkuu.
Halafu utafikiri haya matatizo wanasiasa hawayaoni.
Ndiyo maana tunaisfia Wizara ya Ujenzi na kuiponda hii ya Maji katika kutekeleza miradi kwa weledi.
 
Ukiona mwanasiasa anatafuta mchawi wa kumsukumia lawama kwa kushindwa mradi, eti ni mkandarasi, ujue kashindwa kazi!
Ni kweli, haya matatizo ya Sekta yanatengenezwa. Solution zipo lakini wameamua kukaa kimya.

Ni suala la kuita kikao na Makandarasi wa miradi ya Maji then wanakupa hints

Baadaye unaitisha kikao na Wataalamu wa Sekta watakupa changamoto zao

Mchawi wa miradi ya Maji anajulikana
 
Kweli kabisa mkuu.
Halafu utafikiri haya matatizo wanasiasa hawayaoni.
Ndiyo maana tunaisfia Wizara ya Ujenzi na kuiponda hii ya Maji katika kutekeleza miradi kwa weledi.
Ni kweli, walichoweza wa Ujenzi licha ya mazingira yao ya kazi kuboreshwa lakini pia wameweza sana kujitenga na Siasa.

Sekta ya Maji na Siasa ni kama Uji na Mgonjwa 😀
 
Ni kweli, walichoweza wa Ujenzi licha ya mazingira yao ya kazi kuboreshwa lakini pia wameweza sana kujitenga na Siasa.

Sekta ya Maji na Siasa ni kama Uji na Mgonjwa 😀
Ha ha ha!
I hope yule mtaalam wa kuwatua ndoo kina mama, Mh Juma Aweso-Waziri wa Maji, apitie hapa!
 
Ni kweli, haya matatizo ya Sekta yanatengenezwa. Solution zipo lakini wameamua kukaa kimya.

Ni suala la kuita kikao na Makandarasi wa miradi ya Maji then wanakupa hints

Baadaye unaitisha kikao na Wataalamu wa Sekta watakupa changamoto zao

Mchawi wa miradi ya Maji anajulikana
A good way forward.
 
View attachment 1720724

Kama kuna Wizara ngumu kwa makandarasi nchi hii, basi ni Wizara Ya Maji.

Wizara hii haijielewi katika fani ya ujenzi.

Matatizo waliyonayo wizara hii ni tofauti kabisa na wizara nyingine.

Ni ukweli usiopingika kuwa Makandarasi wabobezi na wanaojielewa hawachukui kazi za Wizara ya Maji.

Ukitaka kupigwa Tanganyika Jacki na mwanasiasa basi unachukua kazi za Wizara hii.

Wizara ya Maji kuna uozo mwingi sana katika procurement za miradi yake ya Ujenzi.

Miradi mingi haina design(usanifu) za kina.

Miradi mingi ya Maji haina fedha za miradi na zikiwepo hazifiki kwa walengwa.

Sababu rahisi za kujieleza kwenye uso wa umma ni kuwalaumu makandarasi!

Hatuoni tarumbeta hizo na visingizio kwenye miradi inayotekelezwa kwenye wizara zinazojielewa kama Wizara ya Ujenzi na TANROADS.

Wizara ya Maji imelalamikiwa sana juu ya very poor Project Management katika idara ake zote, ile kumlaumi mkandarasi kwa kiasi fulani kinaeleza kushindwa kwa mwenye mradi(Wizara ya Maji) kwa ujumla.

Mtu usipojua kuendesha baiskeli, na inakuangusha kila mara, njia rahisi kujieleza ni kusema baiskeli ni mbovu.

Lakini kiuhalisia wengine wanaendesha baiskeli hiyo kwa weledi tu, haiwaangushi, tatizo ni kukubali kuwa hujui kuendesha baiskeli!
Ndiyo wizara yetu ya Maji

Sasa tukiona magazetini, hasa gazeti la serikali Daily News, ati Msemaji wa Serikali naye anaingia mkumbo wa kutoelewa kiini cha tatizo, ndo lile lile linaitwa passing the buck!

Dkt. Abbas changa la macho hilo!!
Nakupe heko kwa maelezo yako. Ila ningeomba labda utumegee matatizo ya wizara, mashirika, na wandarasi katika hii sekta ya maji. Mimi nimeshuhudia miradi miongi ya maji kufa, na hii ni tangu wakati wa serkali ya hayati mwalimu. Miradi hii ilihujumiwa na viongozi wakishirikiana na viongozi, lakini hata raia nao walihusika katika kuhujumu miundo mbinu ya miradi. Mfano wangu ulikuwa sehemu fulani ambao wananchi walikuwa wanachimua mabomba kutengeza bangili za wakina mama. Kuna sehemu nyingi mkandarasi alipewa kuchimba lambo, lakini akaishia kuchimba shimo tu, akachukuwa pesa akaambaa (huenda alishirikiana na viongozi) na hadi leo hata shimo halipo.
 
View attachment 1720724

Kama kuna Wizara ngumu kwa makandarasi nchi hii, basi ni Wizara Ya Maji.

Wizara hii haijielewi katika fani ya ujenzi.

Matatizo waliyonayo wizara hii ni tofauti kabisa na wizara nyingine.

Ni ukweli usiopingika kuwa Makandarasi wabobezi na wanaojielewa hawachukui kazi za Wizara ya Maji.

Ukitaka kupigwa Tanganyika Jacki na mwanasiasa basi unachukua kazi za Wizara hii.

Wizara ya Maji kuna uozo mwingi sana katika procurement za miradi yake ya Ujenzi.

Miradi mingi haina design(usanifu) za kina.

Miradi mingi ya Maji haina fedha za miradi na zikiwepo hazifiki kwa walengwa.

Sababu rahisi za kujieleza kwenye uso wa umma ni kuwalaumu makandarasi!

Hatuoni tarumbeta hizo na visingizio kwenye miradi inayotekelezwa kwenye wizara zinazojielewa kama Wizara ya Ujenzi na TANROADS.

Wizara ya Maji imelalamikiwa sana juu ya very poor Project Management katika idara ake zote, ile kumlaumi mkandarasi kwa kiasi fulani kinaeleza kushindwa kwa mwenye mradi(Wizara ya Maji) kwa ujumla.

Mtu usipojua kuendesha baiskeli, na inakuangusha kila mara, njia rahisi kujieleza ni kusema baiskeli ni mbovu.

Lakini kiuhalisia wengine wanaendesha baiskeli hiyo kwa weledi tu, haiwaangushi, tatizo ni kukubali kuwa hujui kuendesha baiskeli!
Ndiyo wizara yetu ya Maji

Sasa tukiona magazetini, hasa gazeti la serikali Daily News, ati Msemaji wa Serikali naye anaingia mkumbo wa kutoelewa kiini cha tatizo, ndo lile lile linaitwa passing the buck!

Dkt. Abbas changa la macho hilo!!
Declare your interest tafadhali!
 
Kwa uelewa wangu mdogo ( as a layman) Jidu la Mabambasi( kwenye field ya Civil Engineering, matizo mengi ktk miradi yatasababisha na uzembe wa either parties, such as Client,or Engineer or Contractor. Kila party lazima iwe inawajibika ipasavyo kuanzia kwenye Design na Contract documentation, correct procurement process, competent supervision, smooth , and proper project financing including timely payments of contractor, service ,material supplier etc, according Conditions of contract ili kuwezesha mafanikio kwenye miradi. Sasa mie nafikiri mara nyingi, kwa juu juu wengi huwa tunakimbilia kulaumu mojakwamojà Contractor bila kuona tatizo hasa ni wapi? Ikichunguza kwa undani, unaweza kuta flaws zimefanyika, kuanzia kupata competent consultant( msimamizi wa mradi), or unakuta kulikuwa na tatizo kwenye Design(inaccurate) ,or kwenye procurement (in mproper process which results to awarding a contract to incapable contractor)na as result anakuwa anashindwa kufanya kazi, na pia tatizo laweza kuwa kwenye supervision team, or upande wa Client kutolipa certificates za Mkandarasi kwa wakati , kwa zile approved works. Kwa hiyo kumlaumu Contractor moja kwa moja linapotokea tatizo, huwa inafaa kujaribu kuangalia kwa uhalisia limesababishwa nani???
Thank you. Excellent analysis.
 
Miradi ya Maji sio kwamba inashida ya design la hasha.

Mkuu Jidu La Mabambasi ameeleza sababu za wazi zinazokwamisha utekelezaji wa miradi ya Maji uki compare na miradi mingine ya Ujenzi, kama umewahi kufanya Kazi ya Ukandarasi utaona utofauti.

Miradi ya Maji tatizo lake kubwa ni Ucheleweshaji wa Malipo, hii hupelekea miradi isikamilike kwa wakati, inafikia kipindi Una raise madai ya labda 300M, lakini utakuja kulipwa labda baadaya ya miezi 6 au mwaka.

Sote tunajua mradi unapochelewa kukamilika unakuwa na cost implication hasa kwa Mkandarasi, unaweza kuta wakati Una bid bei ya bomba la 3" ilikuwa pengine 1,500,000 lakini kutokana na ucheleweshaji wa malipo hence mradi kuchelewa ambapo utakuta bomba imepanda tena bei, kwahiyo itakulazimu mrudi tena mezani na kuanza kuitumia hela ya Contingency ambayo itapelekea gharama ya Mkataba kupanda.

Ndiyo stage hii wasiojua kinachoendelea kusema miradi ya Maji kuna Upigaji.

Mkandarasi kama analipwa kwa Wakati hutakuja kuona hizo mambo.

Jifunzeni kwa miradi inayofadhiriwa na Donnars kama UNICEF, World bank au Ukaid ambayo inafanywa kwa Force account mbona inakimbia, ni kutokana na Wafadhiri kuingiza hela kwa watekelezaji kabla ya kuanza kujenga.

Kwa hili unaona kabisa mwenye shida ni Serikali nasio Makandarasi.
Nafikiri ni kweli ucheleweshaji wa malipo unaleteleza miradi kutokamilika au kutokamilika kwa wakati. Ucheleweshaji wa miradi pia huongeza gharama za miradi maana ukichelewa miezi sita kulipwa, utakapolipwa gharama zitakuwa zimepanda (bei kuongezeka).
 
Na hiyo ndiyo sababu Kuu
 
Dah labda 2010 maana 2015 hata taasisi ya Jakaya Kikwete ilikuwa ipo. Kuna mambo yalikosewa na yalipatiwa tusiwasingizie wastaafu wote.

Tukisema hivyo maana yake kila kitu kimefanyika kuanzia 2015 sio? Ni hii miradi michache tu isitufanye tudharau na makubwa yakiyokuwepo kabla.
Kila kitu ni kigumu kama watendaji wake ni wagumu kufanya uchambuzi, kutengeneza bajeti stahiki, kuweka mpango kazi na usimamizi makini

Hata 2015 kurudi nyuma ilikua ngumu sana kupata kitanda pale Mwaisela, mgonjwa kulazwa chini ilikua kawaida sana ila sasa vitanda vipo tena vitanda safi
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom