DKK 45 za ITV

Nicholas

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
25,260
7,195
Ktk mwendelezo namarudio ya dkk 45 za ITV tumeshuhudia jinsi kipindi hiki kinavyotaka jijenga ili kije fanya kazi ya CCM kuelekea 2015.Wanasiasa wa CCM na wafanyakazi wa taasisi ambazo CCM wanadhani kuwa wanazisafisha au hata kujivunia wamekuwa wakirudia rudia sana.Sidhani kama ni vibaya JF wakipiga kambi siku hiyo na kuchambua vitu critically.
 
J3 ijayo ni Wassira tena,ambaye alipata ujumbe wa NEC kwa kutaja CDM chama chenye karama, hata masikini hupata nafasi ya kugombea ushindi ktk uchaguzi akiwa upande wa CDM.Sasa hivi hata ndani ya CCM usipojiambatanisha na CDM huwezi shinda kirahisi.Unaweza pata taabu kama Membe.

hiyo ndio CCM ktk parasitic relationship na vitu vyote vinavyoizunguka.Kuanzia malia sili zetu hadi mahusiano na vyama vingine.Tukamasikilize kesho na kuweka vyem kumbukumbu anapoanza bwatuka umbea, na ujinga miwngine ambao JK anauita "kutete chama wakati wapinzania wakieneza uongo".
 
Ktk highlight mojawapo ya vitu atakavyojibu ni ufisadi, sijui km mdomo utafunguka vyema vyema ingawa kipindi hiki ni kama self test.

Pengine bado ana moto wa mkutano uliomchagua na maelekezo ya presidaa kuwa naow apite nyuma ya M4C wakisema serikali imefanya hivi na hivi. Sijui watasemaje kuhusu ufisadi waliouanzisha?

Watasema kuwa wamepiga hatua kubwa kuutokomeza wakati wao ndio waliouleta?
 
Ktk mwendelezo namarudio ya dkk 45 za ITV tumeshuhudia jinsi kipindi hiki kinavyotaka jijenga ili kije fanya kazi ya CCM kuelekea 2015.Wanasiasa wa CCM na wafanyakazi wa taasisi ambazo CCM wanadhani kuwa wanazisafisha au hata kujivunia wamekuwa wakirudia rudia sana.Sidhani kama ni vibaya JF wakipiga kambi siku hiyo na kuchambua vitu critically.

CCM itatumia kila kitu kujihakikishia kubaki madarakani na itafanikiwa,lakini ikumbuke haitodumu milele itakufa tu.
 
Mi huwa naangalia Jenerali on Monday na Mikasi! Hiki kipindi ni cha kipuuzi tu

Si mbaya kumbana kwa kila semacho.CCm wamefaidi sana uelewa mdogo wa watu,kwa kuzuia vyanzo vya habari vyenye maana na kuwawekea vya hovyo.Huwezi amini watanzania pekee ndio watu wanaoona kitu kwa macho yao ila hawaamini hadi waambiwe na watu fulani.

Watu hawajawahi ona vurugu za CDN ila wanaamini viongozi wakisema, watanzania ndio wanaoamini vyanzo vyote vya habari ni vya kichonganishi hadi vihalalishwe na serikali, watu hawaamini kuwa ARV fake zilitolewa na vyombo vya serikali hadi walipokiri,ila bado tena CCM wakirudi na kusema CDM wanawachonganisha na raia wapo wengei wataamini haswa wana CCM na wengine ktk free community.

Ni jukumu la wapenda mabadiliko kutumia lugha nyepesi kupunguza au kuundolea nguvu huu upuuzi wa CCM.Ni vizuri tuanangalie ili tujue zaidi kuusu hila za CCM.Ingawa waondesha kipindi wanaweza jisikia kuwa palatforma imekuwa na hiyo hata kuvuta mtangazo,kabla hawajaja gundua kuwa ni audience ya kuwaua.
 
Mie naamini mwandishi kukipenda chama fulani siyo mbaya. la msingi ni kujipambanua tu. Baada ya hapo ni kufuata maadili yote ya uandishi ikiwa ni pamoja na kuandika UKWELI au kujihusisha na Habari za ukweli za vyama vingine bila kujali ukweli huo ni mzuri au mbaya/
J3 ijayo ni Wassira tena,ambaye alipata ujumbe wa NEC kwa kutaja CDM chama chenye karama, hata masikini hupata nafasi ya kugombea ushindi ktk uchaguzi akiwa upande wa CDM.Sasa hivi hata ndani ya CCM usipojiambatanisha na CDM huwezi shinda kirahisi.Unaweza pata taabu kama Membe.

hiyo ndio CCM ktk parasitic relationship na vitu vyote vinavyoizunguka.Kuanzia malia sili zetu hadi mahusiano na vyamaM vingine.Tukamasikilize kesho na kuweka vyem kumbukumbu anapoanza bwatuka umbea, na ujinga miwngine ambao JK anauita "kutete chama wakati wapinzania wakieneza uongo".
 
Mie naamini mwandishi kukipenda chama fulani siyo mbaya. la msingi ni kujipambanua tu. Baada ya hapo ni kufuata maadili yote ya uandishi ikiwa ni pamoja na kuandika UKWELI au kujihusisha na Habari za ukweli za vyama vingine bila kujali ukweli huo ni mzuri au mbaya/

Kwa uduni wa waandishi wetu , wansiasa wanatumia media kujipatia umaarufu usiostahili.Wangekuwa wanaulizwa maswali magumu,na yanayoakisi fununu zilizopo uraiani ni wazi watawakilisha watu wengi na majibu yae yatakuwa yamejibu maswali ya watu wengi kam si wote.Na hivyo kulazimisha hawa wanasiasa kujietetea kwa hoja na si kutuwekea hadithi za watoto wadogo.

Ukimkuta mwandishi wa CNN au BBC anavyowahoji watu kama rais wa Iran,Waziri mkuu wa Israel, au wawakilishi wa China, na Viongozi wa Africa utaona kabisa jinsi wanavowapeleka ktk angle na mwishowe kuwapa ahsante na mkono wa furaha ila weny akili zao watajua nini si fununu tena bali ni ukweli na kipi ni zaidi ya hata watu walifikiri.
 
Wadau; Kwanza someni makala hii halafu angalia comments hapo chini.



JAJI LUBUVA NA UHURU WA TUME YA UCHAGUZI:
Uteuzi wa Tume unakinzana na msingi mkuu wa utoaji haki


NA HILAL K. SUED

Ukosaji wa umahiri na weledi kwa wengi wa wanahabari wetu kutoka vyombo vyote viwili vya habari – yaani vile vya machapisho na vya umeme – katika kufanya mahojiano na watu mbali mbali, hasa wakuu wa serikali na wa siasa si suala tena la mjadala.

Malalamiko mengi yametolewa na kuandikwa kwamba mara kadha wanahabari wanaoendesha mahojiano ya aina hii hujikuta ‘wanatekwa' na hao wahojiwa – yaani hawa ndiyo huongoza muelekeo wa mahojiano. Ni dhahiri kwamba ama mhoji huwa hajajitayarisha barabara kabla au humuogopa au kumuonea haya yule mhojiwa kwa kushindwa kumuuliza maswali ya ki-uchokonozi.

Haina tija yoyote kwa wasomaji/wasikilizaj/watazamaji wa mahojiano hayo kuona mhojiwa akijibu maswali ‘laini' na hivyo majibu yake kuwa ya kutarajiwa (expected responses).

Hata hivyo nakiri kwamba baadhi ya mahojiano huwa ni kwa lengo la kuuhabarisha umma tu katika masuala mapya au yenye utata kwa jamii, lakini hata hivyo mhoji inampasa kuwa mahiri kwa kujaribu ‘kumnasa' katika maeneo ambayo anaonyesha kuingiza hadaa.

Lakini katika masuala ya siasa, au yale yanayohusiana na siasa, ambayo mara kwa mara huzingirwa na utata (controversy) inampasa mhoji kumbana mhojiwa vilivyo kwa masuala ya kushtukizia nay a uchokonozi kwa lengo la kupima iwapo anaimudu vilivyo nafasi/wadhifa wake katika serikali au siasa.

Mhoji aliye mahiri zaidi inambidi ajitayarishe vyema -- kwa kupata habari/historia ya mhojiwa, iwapo kwa mfano ana kashfa huko nyuma au la.

Wengi wetu mtakumbuka aliyekuwa mhoji maarufu wa television ya BBC World – Tim Sebastian – na kipindi chake cha Hard Talk. Huyu bwana alikuwa kiboko maana ukikubali kwenda kuhojiwa naye, ujue kwamba historia yako yote kisha ijua na hivyo swali lake la kwanza tu linaweza kuwa ni dhoruba isiyoitegemea.

Miaka kadhaa iliyopita aliyekuwa rais wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa alikuwa mhojiwa wa Tim Sebastian na alikumbana na hayo. Wengi tuliona alivyokuwa anapandisha jazba jinsi kipindi kilivyokuwa kinaendelea. Mara nyingi mahojiano ya Tim Sebastiana hayakuwa yakiendana kwa ‘uswahiba' kama ilivyo kwa wahoji wetu hapa.

Wiki iliyopita, katika kipindi cha mahojiano cha ‘Dakika 45' kinachorushwa na ITV mhojiwa alikuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi, Jaji mstaafu Damian Lubuva. Ni mmojawapo wa watu muhimu sana katika medani ya siasa za Tanzania – hasa siasa za ushindani za vyama vingi na hivyo kukubali kwake kuhojiwa kuliashiria shauku kubwa kwa watazamaji.

Lakini mtangazaji alionekana hakuwa mahiri na kila mara alikuwa anauliza maswali ambayo majibu yake yalitarajiwa. Kwa mfano – katika swali kuhusu ‘uhuru' wa Tume ya Uchaguzi katika maamuzi yake kila mtu alitarajia jaji Lubuva kujibu kwamba Tume yake ni huru na maamuzi yake ni huru nay a haki na kwamba wananchi waendelee kuwa na imani na Tume.

Kama mwendesha kipindi angekuwa mahiri, na kujitayarisha vilivyo angemuuliza swali lifuatalo – swali ambalo linatokana na msingi mkuu wa haki (principle of justice) na Lubuva kama jaji mstaafu wa Mahakama ya rufaa anaufahamu vyema:

"Mheshimiwa Jaji, kama unakubaliana kwamba msingi mkuu na maarufu wa haki usemao "Si kwamba haki itendeke tu, bali pia ni lazima ionekane inatendeka" (justice must not not only be done but must also seen to be done) jee huoni kwamba Tume (NEC) yako, iliyoteuliwa na rais Jakaya Kikwete ambaye pia ni mkuu wa chama cha siasa kinachoingia katika ushindani mkuu wa kisiasa dhidi ya vyama vingine vya siasa, siyo huru?"

[Bila shaka aliyebuni ulazima kwa mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi kuwa na sifa za jaji wa Mahakama Kuu aliyafikiria masuala mbali mbali likiwemo hili la msingi mkuu wa kutoa haki.]

Kwa maneno mengine katika sehemu ya pili ya msingi huo wa haki nilioutaja hapo juu, haki haitaonekana kutendeka kwa sababu ‘mtoa haki' – yaani NEC iliteuliwa kwa namna ambayo kimuonekano wake haiwezi kutarajiwa kutenda haki.

Hilo ni moja, lakini kikubwa zaidi, na kwa kuzingatia msingi huo huo wa haki, ni uandikishaji wa wapiga kura. Tuache kwanza uchaguzi ujao wa 2015 (miaka mitatu kutoka sasa) ambao huenda ukaendeshwa kutokana na Katiba mpya inayotarajiwa, na hivyo kuwepo kwa namna mpya upatikanaji wa Tume ya Uchaguzi. Lakini katika kipindi cha mwaka mmoja au miwili ijayo hatuwezi kukwepa chaguzi ndogo za Ubunge na hapa majimbo yanayotarajiwa ni ya Sumbawanga Mjini, Arusha mjini na Igunga.

Sasa iwapo mara ya mwisho uboreshaji wa daftari la wapiga kura katika majimbo haya ulifanyika mwaka 2009 yaani takriban miaka mitatu iliyopita, jaji Lubuva haoni kwamba NEC yake itakuwa haitendi haki kabisa iwapo chaguzi hizo zitafanyika bila ya kuboresha daftari kwani mapungufu hayo yanatokana na ukosefu wa fedha kutoka serikalini?

Ni bora Lubuva angetamka bayana – na hili liwe kama onyo kwa serikali – kwamba iwapo serikali haitatoa fedha kuboresha daftari la wapiga kura, basi chaguzi hazitakuwa huru na haki. Kwa nini aogope kutamka hivyo bila kigugumizi, iwapo kweli yeye anadhamiria kutenda haki katika Tume yake?

Ukweli ni kwama serikali itakuwa imewanyima malaki ya raia wa Tanzania ambao wamefikisha umri wa miaka 18 katika kipindi cha tangu 2009 – hivyo katika mazingira haya iwapo uchaguzi utafanyika basi dhana ya kwamba uchaguzi utakuwa umefanyika kwa uhuru na haki itakuwa ni uongo mkubwa.

Kwa maoni yangu iwapo jaji Lubuva anataka Watanzania waendelee kuiamini Tume yake, basi ni vyema akaipigia kelele serikali masuala haya tena hadharani – kwamba serikali inafinya demokrasia kutokana kwa kisingizio cha kukosekana fedha.

Kukosekana fedha, kama nilivyotaja, ni kisingizio tu kwa sababu serikali ina matumizi mengi tu yasiyoleta tija, tukiacha ufisadi, wizi na uporaji wa fedha na mali za umma kama inavyoripotiwa kila mwaka na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Serikali.

Isitoshe hakuna haja ya kutaja kwamba kuminya haki hii ya kidemokrasia kunaweza kuitumbukiza nchi katika ghasia kubwa.

Hata hivyo miaka kadha iliyopita aliyekuwa makamu Mweyekiti wa Tume ya Uchaguzi, Jaji Augustino Ramadhani aliwahi kushangaza watanzania katika kongamano moja la masuala ya siasa alipokiri hadharani kwa kusema kwamba kwa muono wake, NEC siyo tume huru – kutokana na upatikanaji wake.

Lakini alisisitiza kwamba hayo yachukuliwe kama ni maoni yake binafsi siyo ya Tume yenyewe ambayo yeye alikuwa makamu mwenyekiti wake. Jaji Lubuva ana ubavu wa kumpiku jaji huyo mwenzie haidhuru katika matamshi tu?

Source: Mtanzania Jumapili of 18.11.2012





My take:


Kwanza ningeshauri MODs wasiondoe thread hii lakini waiboreshe heading yake – iwe kwa mfano: "Jee Kipindi cha ‘Dakika 45 ITV' kinasaidia kuelimisha umma au.." or something like that.

Kuhusu makala hiyo hapo juu nakubaliana na mwandishi kwamba mwendesha kipindi siyo mweledi na hatumii umahiri wa kutosha kuwabana wahojiwa hasa katika masuala yenye utata ya kitaifa – na mara nyingi huwaachia kumiliki mahojiano. Ni kweli hushindwa kubuni maswali ya uchokonozi.

Mfano wa mwandishi wa makala (highlighted in red) ni mzuri sana katika mapungufu yaliyotokea katika Kipindi cha Dak 45 cha wiki iliyopita ambapo mhojiwa alikuwa jaji Lubuva, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi (NEC).

Huo mfano pia umenikumbusha mwandishi mmoja ambaye ni mhariri wa gazeti moja maarufu hapa nchini kumuuliza Jk swali la hoivyo hoivyo kuhusu sakata la kutekwa kwa Dr Ulimboka hasa pale gazeti la Mwanahalisi lilikuwa tayari limeanika kila kitu, na nani mhusika – Rama Ighondi afisa mwandamizi wa Usalama wa Idara ya Taifa.

Katika mkutano na waandishi wa habari Ikulu baada ya Jk kuruhusu maswali mhariri alimuuliza: "Mheshimiwa Rais ni kweli serikali yako inahusika katika utekaji wa Dr Ulimboka?"

Of course lazima JK ajibu kwamba la hasha serikali yake haihusiki.

Angekuwwa mahiri, huyo mhariri angelijenga swali lake kuwa hivi: "Jee Mheshimiwa Rais, Rama Ighondu ni afisa wa usalama katika serikali yako?" or something like that.

Hapo Jk angehangaika na body language ingemsuta tu.

Mimi naelekea kukubali kwamba kipindi hiki cha Dak 45 ITV kina lengo la kujaribu kusafisha wakubwa. Ikumbukwe kwamba katika miaka ya 90 hawa hawa ITV walikiua kipindi cha Kiti Moto kilichokuwa kinarushwa na DTV baada ya kuchukuliwa na ITV.


Hicho kipindi kilikuwa kiboko kweli kweli kwani wahojiwa kweli walijikuta wamekalia kiti moto katika muda wote wa kipindi (mwendeshaji alikuwa Pascal Mayalla).

Mahojiano yalikuwa yanafanyika kwenye ukumbi na wananchi wa kawaida tu walikuwa wanakwenda na waliruhusiwa nao pia kuuliza maswali.

Lakini hata hivyo katika mazingiura ya sasa nisingependa kipindi cha mfumo huo wa uendeshaji kirudi kwa sababu mhojiwa anaweza kulipa watu wake ili wajae ukumbini ili wamuulize masuali ya hovyo hovyo.









 
Ni kipindi cha kingese sana mbona dr.wa ukweli,kamanda mbowe hawaitwi,ni kipindi cha wasira,membe,na sita.
 
Marksman
Nashukuru kwa mchango wako mpana.Kweli heading inaweza isiwe sahihi kwa sasa,ila nimejaribu ifupisha ili next time isitokee nikajikuta nimeweka thread nyingine kama "JK ktk dk 45 za ITV live" halfu kesho nyingine,wakati kwa ujumla ni kipindi cha kushape watu na mitazamo ayao juu ya ccm .Hii inaweza isiwe shida kwa space lakini ikawa shida kwa wasomaji .Kuna kitu kinaitwa information overloading and searchability. Mtu anaweza kuwa thread nyingi na ndefu kiasi ch akumfanya asijue ipi aipe kipaumbele na ipi asiisome kabisa.

Najaribu ifanya iwe rahisi ili iebebe vipindi vingi vinavyo na watu wawe na mapana ya kutoa mitazamoa yao.pengine tunaweza ona pattern fulani ktk mahojiano na majibu yao na kuweza jua wanaelekea wapi.Si busara kuwa na data nyingi halafu haziwezi tusaidia pata secondary data.
 
Anaanza jisifia kwa barabara, anasema siku nyingi kigoma hakukuwa na barabara , as if si CCM ilikuwa kipindi hicho.
 
gamba linasema kilimo kinachangia kwa asilimia 4.5 ila kikifikia asilimia 6 kitakuwa sehemu nzuri.Waktai mhandishi anataka clarification hiyo asilimia 6 inakuweje?kwa kuongezeka watu au?Gamba likasema watu wakiongezeka ktk kilimo.

Hajui kuwa watu wapo ktk kilimo kwa asilimia kubwa sana na kinachomatter hapa si watu wengi ila production kuongezeka na mchango wake kwa pato uwe mkubwa.
 
Bado alia na "Approval ya Slaa kwa kila watendalo" km rais wake anadai kuwa Slaa anawapunja sana marks. Sishangai kwanini walijisikia ahueni pale Selasini alipowapongeza na baadaye mbowe.

CCM wana very low esteem mbele ya CDM.Lazima ktk kila itu wawa tag CDM.Then wanafanya follow up huku wakilazimisha kukubalika.Wish siku nyingine Dr. N Mbowe wawe Likizo.Sijui watajipiga vichwa chini?

Magufuli alijipendekeza vibaya sana kwa mbowe pale Bungeni alipokuwa kaiwakilisha Hotuba ya Wizara yake.Same kwa Jk akiwa ktk mkutano wa CCM, wassira naye bado analia na Dr.
 
dkk 45 ni Malecela tena, marudio yake ya kuchekesha.Like father like son.
 
Back
Top Bottom