Dk. Willem Jacobs: Hatutakiuka makubaliano yoyote tuliyoweka na Tanzania katika malipo

Leo uongozi wa juu wa Barrick Mines Tanzania umepata fursa ya kukutana na Mheshimiwa rais Magufuli na kueleza yaliyo moyoni mwao,

moja ya mambo ambayo wameeleza ni kumshukuru Magufuli kwa msimamo wake usiotetemeshwa na mabeberu pia na nia yake ya dhati katika kuwaletea maendeleoa watanzania wa hali ya chini,

akaendelea kueleza kwamba hakutakuwa na mabadiriko yoyote katika makubaliano ya awali,
1.300 USD millions watazilipa
2.Mgawanyo wa asilimia 50 kwa 50 katika faida kama ilivyoelezwa hapo awali,
View attachment 1027332
Unaamini mashairi ya Msigwa? Wajinga tu ndo mtaendelea kudanganywa - juzi mliandika pia shairi kama hili kwamba kuna kampuni Kenya imeamua kununua korosho yote Mtwara na Lindi - mmeachwa na jambajamba msijue la kufanya dadeki...na wakati mwingine mlidai Benki ya Dunia imeamua kuachia mkopo wa dola mil.300, baada ya siku 2 WB wakawakanusha mkaachwa tena na jambajamba!
 
Tuliambiwa hivyohivyo mwaka uliopita, lakini mpaka sasa hatujapata hata senti.

Ni style ya mwanaume anaendelea kuimbisha, ooh nitakujengea gorofa, nitakununulia gari, ooh nitakupa hela, demu anashangilia tu!
 
Hii ni habari njema, ila kwa mujibu wa taarifa hii, the settlement is inayozungumziwa hapa ni settlement ya yale makubaliano ya kile kishika uchumba cha US $ 300 milioni za goodwill, kuunda Kampuni mpya, na kugawana 50/50 economic benefits na sio profits kama tulivyo elezwa, ila bado sijasikia waki mention anything kuhusu the principal ile US $ 190 Billion dollars ya Noah zetu.

Kwa vile ahadi hiyo ilikuwa ni unconditional kuonyeshea goodwill, na hapa kati yamesemwa mengi, Barrick ili waonyeshe they are gentlemen, wasinge ongea chochote kabla ya kukabidhi kishika uchumba chetu, ndipo mengine yote yafuate.

P
 
Wewe kuangalia ngozi hakuna tofauti na ukaburu, acha ubaguzi wa rangi ni mbaya sana
Kwa hiyo unataka kuniambia Lissu au wapinzani wakiongea na hao wanaonekana ni mawakala wa mabeberu ila viongozi wakiongea nao si mawakala wa mabeberu?
 
Mnatuchanganya sana. Barrick mines wanasema watalipa. Acacia anauza mali zake kwa mnada. 2020 Acasia anafunga shughuli zake, mgodi hautakuwa na faida tena. Makinikia kimkataba bado ni mali ya Acacia. Kuna kesi karibu 30 kwenye mahakama za kimataifa. Mimi naona kizungu zungu.
 
moja ya mambo ambayo wameeleza ni kumshukuru Magufuli kwa msimamo wake usiotetemeshwa na mabeberu pia na nia yake ya dhati katika kuwaletea maendeleoa watanzania wa hali ya chini,
Nimekumbuka kuwa hawa ni "wanaume" na si "mabeberu" (Kwa sauti ya JPM na britanicca).LoL
Sasa ile invoice ya kodi tutalipwa? Au Tushukuru tu na hicho kishika uchumba (Sauti ya P.)
 
Back
Top Bottom