Dk. Ulimboka aombewa ulinzi "The Amnesty International", Ubalozi wa TZ Afrika Kusini wahaha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dk. Ulimboka aombewa ulinzi "The Amnesty International", Ubalozi wa TZ Afrika Kusini wahaha

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by palalisote, Jul 4, 2012.

 1. palalisote

  palalisote JF-Expert Member

  #1
  Jul 4, 2012
  Joined: Aug 4, 2010
  Messages: 8,352
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 0
  MWENYEKITI wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania Dk. Steven Ulimboka ameombewa ulinzi kwenye Shirika la Kimataifa la Kutetea Haki za Binadamu la Amnesty International.Vyanzo vya habari vya kuaminika kutoka ndani ya jopo la wataalam na jumuia hiyo kwa nyakati tofauti vimeliambia Tanzania Daima Jumatano kwamba wamelazimika kuomba ulinzi wa kimataifa ili kukabiliana na watu wabaya wanaotaka kumdhuru.Vyanzo hivyo vilisema watu waliomdhuru wanataka kummaliza kabisa ili kuficha ukweli kwani kabla ya kuondoka Dk. Ulimboka alieleza ukweli wa tukio hilo hivyo wabaya wake hao wanatumia baadhi ya watumishi wa ubalozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini kuhakikisha wanampata.

  "Hii ya kuomba ulinzi ni ‘latest'; Amnesty International ni wabishi lakini katika hili wameombwa naamini watakubali kumlinda… maombi yamepelekwa jana."Kabla ya kupelekwa Afrika Kusini Dk. Ulimboka alieleza ukweli wa tukio zima kuanzia walivyomkamata na mateso waliyompa hadi walipotaka kumzika akiwa hai."Wameshajulikana sasa wanatumia ubalozi wetu kutaka kupenya kwenda kumwona hospitalini ndiyo maana haisemwi yuko hospitali gani… ukweli ni kwamba usalama wa Dk. Ulimboka uko hatarini," kilisema chanzo hicho cha kuaminika.Bila kujua kwamba hizo ni habari chanzo hicho kiliendelea kueleza kwamba akiwa njiani kuelekea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Dk. Ulimboka aliwataka viongozi na madaktari wengine ndani ya jumuia kupigania haki zao.Kwa mujibu wa chanzo hicho mwenyekiti huyo wa jumuia aliwasihi waliobaki wasikubali damu yake imwagike bure, wahakikishe maslahi ya madaktari yanaboreshwa.

  "Msikubali damu yangu imwagike bure; endeleeni kupigania haki zenu…," chanzo hicho kilimnukuu Dk. Ulimboka.Hata hivyo ilielezwa kwamba jumuia hiyo ilishirikiana na Kituo cha Sheria na Haki za Binaadam (LHRC) kuomba ulinzi huo kutoka Amnesty International.

  Chanzo: Tanzania Daima


  WAKATI HUO HUO

  "Taarifa tulizozipata kutoka Afrika Kusini zinasema kwamba, hali ya Dk Ulimboka imezidi kuimarika tofauti na alivyokwenda, figo zimeanza kufanya kazi ingawa kwa polepole na amefanyiwa vipimo vingine," alisema Dk Kabangila na kuongeza:

  "Pia ameanza kuzungumza, anawatambua watu vizuri na zaidi amewaomba Watanzania wamuombee apone haraka."
  Awali, chanzo kimoja cha habari kilidokeza kwamba hali ya Dk Ulimboka imeimarika kutokana na kupatiwa huduma za matibabu kwa haraka kwa kufanyiwa pamoja na vipimo vingine, kile cha usafishaji damu na figo (Dalysis), mara kwa mara. Kabla ya kuondoka nchini, Dk Ulimboka alifanyiwa usafishaji huo mara mbili.

  Madaktari walisema kuwa, kipimo hicho kililenga kupunguza kiwango cha sumu iliyoonekana kwenye damu, ambayo haikutambulika mara moja kama ilitengenezwa ndani ya mwili au vinginevyo kwa kuwa hakuna kipimo cha kubaini tatizo hilo nchini.


  Chanzo: Mwananchi   
 2. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #2
  Jul 4, 2012
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,655
  Likes Received: 35,416
  Trophy Points: 280
  Ningekuwa karibu ningejitolea kumlinda mimi mwenyewe na labda hiyo ingenipa fursa ya kuua walau CCM mmoja. Licha ya hivyo, lazima tu nitaua mCCM kabla sijafa. I hate them with a passion.
   
 3. Viol

  Viol JF-Expert Member

  #3
  Jul 4, 2012
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 18,982
  Likes Received: 1,088
  Trophy Points: 280
  kitaeleweka tu,sijui watatokaje kwenye hii ishu,wameshikwa pabaya
   
 4. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #4
  Jul 4, 2012
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,315
  Likes Received: 5,609
  Trophy Points: 280
  Ukweli utajulikana tu tena mapema sana!!Mungu awe na wenye heri!amen
   
 5. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #5
  Jul 4, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,202
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Tukae Mkao wa kula ndio hapo Fundi Stella Manyanya atakapothibishiwa watesaji ni wao wenyewe
   
 6. Gwangambo

  Gwangambo JF-Expert Member

  #6
  Jul 4, 2012
  Joined: Jun 30, 2012
  Messages: 3,655
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 145
  Oooh! Lord of Mercy, we thank thee for the health of our, Beloved Brother Ulli, may your Mighty hand protect him against evil spirits of CCM, PM and JK.. Ameeeen!!!!!!!!
   
 7. Laurence

  Laurence JF-Expert Member

  #7
  Jul 4, 2012
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 3,106
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Hakika wataumbuka hawa wahuni wa hiki Chama cha Magamba kwa uhuni walomfanyia Dr Uli.
   
 8. m

  mahoza JF-Expert Member

  #8
  Jul 4, 2012
  Joined: Mar 11, 2012
  Messages: 1,242
  Likes Received: 411
  Trophy Points: 180
  Mh tunamuombea apone haraka. Dua zetu ziko nawe.
   
 9. m

  mwinukai JF-Expert Member

  #9
  Jul 4, 2012
  Joined: May 3, 2011
  Messages: 1,448
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Stella Manyanya alisema aliwaona walivaa magwanda kama ya CHADEMA hapa mkuu wa mkoa lazima aumbuke kirahisi
   
 10. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #10
  Jul 4, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  swala la ulinzi lipo wazi sana na wala halihitaji mahojiano,ni lazima kuwe na watu wa kumlinda kabla ya watekelezaji kukamilisha kusudio lao
   
 11. N

  Ninaweza JF-Expert Member

  #11
  Jul 4, 2012
  Joined: Dec 14, 2010
  Messages: 7,183
  Likes Received: 1,184
  Trophy Points: 280
  Liwalo na liwe
   
 12. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #12
  Jul 4, 2012
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  When GOD says NO, who will be against? Get well soon Dr. Ulimboka! Hakika watu wengi tunatamani kuona viongozi wetu wakiwajibika kwa hili hata kama ni baada ya serikali hii kumaliza muda wake. Viongozi wetu lazima watambue kuwa "what goes away, comes around".
   
 13. Jakubumba

  Jakubumba JF-Expert Member

  #13
  Jul 4, 2012
  Joined: Mar 5, 2011
  Messages: 1,627
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Nakuunga mkono, ila kuua sio vizuri, tuungane tuwatoe madaraka tu
   
 14. Loy MX

  Loy MX JF-Expert Member

  #14
  Jul 4, 2012
  Joined: Mar 26, 2012
  Messages: 1,263
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  kwa style hii sijui kama tutafika.
   
 15. Lyimo

  Lyimo JF-Expert Member

  #15
  Jul 4, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,828
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Tunaomba Mungu uendelee kutenda miujiza yako kwa Dr.Ulimboka. AMEN
   
 16. I

  IWILL JF-Expert Member

  #16
  Jul 4, 2012
  Joined: Jun 2, 2011
  Messages: 311
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  you spoke with my heart, wameua ndugu yangu. uzuri ninawajua, nawafanyia timing and it will be historical event.
   
 17. fyddell

  fyddell JF-Expert Member

  #17
  Jul 4, 2012
  Joined: Dec 19, 2011
  Messages: 2,082
  Likes Received: 774
  Trophy Points: 280
  Tuwatoe madarakani na kuwapandisha kizimbani kwa madudu yote waliyofanya kwenye nchii yetu bila kusahau utaifishwaji wa mali zao walizojilimbikizia.
   
 18. marejesho

  marejesho JF-Expert Member

  #18
  Jul 4, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 6,539
  Likes Received: 830
  Trophy Points: 280
  Tunaomba Mungu umlinde Dr Ulimboka
   
 19. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #19
  Jul 4, 2012
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Usihofu tutafika tu.

  Sisi tulio tumia taa za chemli kufanya home tunajua principle ya taa iliyokaribu kuzima kwa kuishiwa mafuta.
  Inajiongeza mwanga mara dufu kwa sekunde chache kisha hiyooo! Gizaaaaaaaaaaaa
  Huku ni kujitutumua kwa mwisho kwa serikali ya CCM kabla ya kufa kifo cha mende.


   
 20. K

  Kiumbo JF-Expert Member

  #20
  Jul 4, 2012
  Joined: Feb 4, 2012
  Messages: 561
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Mungu akiamua hakuna wa kupinga. Haki ya mtu haizibwi kabisa bali huchela. Mungu aendelee kumlinda dr.Uli. Na taarifa ziende kwa eng.Matunguu, na magamba yote. Hasira na uchungu wa madaktari na wananchi zinawarudia.
   
Loading...