Mzito Kabwela
JF-Expert Member
- Nov 28, 2009
- 18,857
- 7,615
Matokeo ya Uchaguzi mkuu yaliyotangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) yalijaa utata, Mwanahalisi limegundua.
Taarifa kutoka ndani ya NEC, vyama vya siasa na baadhi ya wagombea, zinasema matokeo yaliyotolewa yanatofautianma na kura halisi zilizopigwa.
Kwa mujibu wa baadhi ya mawakala wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), matokeo mikononi mwao yanatofautiana sana na yale yaliyotangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC)
Matokeo mikononi mwa mawakala kutoka mikoa 18 ya Tanzania Bara na mitatu ya Zanzibar, hadi juzi jumatatu yanathibitisha kuwepo kwa tofauti kati ya idadi ya vituoni na ile iliyotangazwa na NEC.
Katika jimbo la Hai, mkoani Kilimanjaro matokeo yaliyotangazwa na NEC yanaonyesha kuwa CCMimepata kura za Urais 35,910 huku Chadema ikionyeshwa kupata kura 18,513. Lakini matokeo ambayo yamekusanywa na mawakala wa Chadema yanaonyesha CCM imepata kura 20,120 huku Chadema ikipata kura 26,724.
Katika jimbo la Karatu Mkoani Arusha, hesabu za NEC zinaonyesha CCM imepata kura za urais 24,382 huku Chadema ikipata kura 41 tu angalau kwa mujibu wa matangazo ya Televisheni. Bali kwa mujibu wa matokeo yaliyokusanywa na mawakala ambayo yamesainiwa na mawakala wa vyama vinavyoshiriki uchaguzi na msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo CCM imepata kura 24,364 na Chadema ilipata kura 43,137
Jimbo jingine ambalo matokeo yake yamejaa utata ni Geita, mkoani Mwanza. Matokeo yaliyotangazwa na NEC katika jimbo hilo yanaonyesha kuwa CCM imepata kura 17,792 na Chadema imeambulia 3,989. Lakini Matokeo mikononi mwa mawakala yanaonyesha kuwa CCM imepata kura 30,960 na Chadema kura 15,736. NEC ilikiri kuwapo kwa kasoro katika jimbo la Geita na ilikubali kufanyia Marekebisho.
Katika jimbo la Ubungo Mkoani Dar es salaam matokeo ya NEC yameipa CCM kura 68,727 na Chadema kura 65,450. Hata hivyo kwa mujibu wa matokeo mikononi mwa mawakala yanaonyesha kuwa Chadema imepata kura 72,252 na CCM kura 70,472.
Uchunguzi wa Mwanahalisi umebaini kuwa licha ya tofauti ya matokeo ya vituoni na yale ya NEC, matokeo katika baadhi ya maeneo hayakurekodiwa kwenye karatasi za tume, rasmi kwa shughuli hiyo. Gazeti limeona matokeo yaliyorekodiwa kwenye karatasi za kawaida na magamba magumu ya makasha, ingawa zimegongwa mhuri inayoonekana kuwa ni ya Tume. Matokeo ya aina hii yanashurutisha kuwepo ujenzi wa shaka juu ya usalama wa kura na uwezekano wa matokeo kughushiwa
Mwanahalisi limeelezwa kuwa mbali na kasoro hiyo ya kutokuwapo kwa fomu za kurekodia matokeo, katika baadhi ya majimbo yaliyofanya uchaguzi, majumuisho ya kura za urais hayakufanyika.
Gazeti hili lilitaka kujua maoni ya Dk. Slaa juu ya taarifa kuwa kuna maeneo ambako majumuisho ya kura za urais hayakufanyika naye alijibu " wewe unazungumza hilo; matatizo yaliyopo katika uchaguzi huu ni mkubwa sana. Kuna Uchafu mwingi. Ndio maana sisi tunasisitiza kuwa hatuwezi kukubaliana na matokeo yaliyotangazwa" Anasema " Tunaendelea kukusanya nyaraka zote za uchaguzi na si muda mrefu ujao, tutaeleza dunia ni kitugani kilifanyika, wapi na akina nani walihusika. Tutaeleza pia hatua gani itafuata baada ya hapa"
Gazeti hili lina taarifa kuwa baadhi ya majimbo ambako matokeo ya Urais hayakutangazwa ni Kiteto, Segerea, Muheza, Kibakwe, Kinondoni, Ilala na Moshi Vijijini.
Kutoka Morogoro taarifa zinaeleza utata wa aina yake. Kati ya wapiga kura 422 waliotarajiwa kupiga kura katika kituo cha shule ya msingi Msufini, kata ya Msufini Manispaa ya Morogoro HAKUNA HATA MMOJA ALIYEKUWA NA SHAHADA YA KUPIGIA KURA
NUNUA MWANAHALISI LA LEO TAREHE 10/11/2011 UONE JINZI CCM WALIVYO NA TAALUMA YA MWAKA 47 YA KUIBA