Dk Slaa: Tuhuma za Lwakatare kuteka waandishi zimepikwa

Hakuna ukomboz usio na vikwazo.
Dhuluma, uonevu, hofu, hakuna wa kumwamin, ulemavu wa kudum, damu kumwagika, KIFO n.k. Hiv ni vitu ambavyo hutokea nch ikiwa kwenye tishio la kubadil uongoz/ utawala ama pale maslah ya watu wazito (mafisad) yanapotishiwa.

Mwananch ndo huamua uamuz wa kweli na wa kudumu.

Tuwe makin sana kusikiliza, kutafakar na kuamua.
 
Kwa kifupi Slaa anatuuliza

"WHO ARE YOU GOING TO BELIEVE? ME OR YOUR OWN EYES???"

 
SLAA ANADHANI MAHAKAMA NI YA BABU WAKE ANATAPATAPA BURE KWA MIPANGO ALIYOIFANYA YEYE NA WENZAKE.
Mungu ibariki Tanzania
rest in piece CHACHA WANGWE.
utatumika sana kama kondomu na karai la zege hatimaye utajitutia kutumika kwako huko
 
kama huna jibu kaa kimya! Mkuu bado upo analojia,tatizo huwa mnatumia akili kidogo bila kujua nini kitatokea mbele.Sura sio ishu ila validity ya ile video.Ila sikulaumu sana kwa sababu wewe ni mtumwa wa akili zako mwenyewe
Nyie CCM mna Polisi, JWTZ, UWT, TISS lakini unatakiwa ujue mtegemea Mungu siku zote usaidiwa na Mungu unachokishabikia mwisho wake utauona na CCM katika jumuia za kimataifa kwa hili ililolifanya litawaingiza katika hatia ya yote yaliyotamkwa katika hii Clip fake.

kweli mijitu humu ina mawazo finyu na hasira
hivi hiyo clip ni ya JF? au YouTube na kwanini aliyeiweka ndio atafutwe?
kwanini aliyeonekana (Rwakatare na waliyehojiana naye katika clip) wasihojiwe? km ni uongo iwe km ile ya Bush
Lakini kusema ni CCM, POLISI, JWTZ, UWT, TISS au MUNGU kuwa upande wa waliotuhumiwa ni upunguani kwani clip yenyewe inajieleza na haijatunwa mpaka dakika ya 19:01 jamaa anayempeleleza Lwakatare anaiangusha simu na ili asishtukiwe anaizia
sasa mnataka ushahidi gani? si muiachie POLISI? au mnataka FBI
 
FBI wapo michezo kama hiyo ni simple saana kuitatua wawape kazi ya uchunguzi ileweke mbivu na mbichi!!!
 
Kwa mtu mwenye akili zake nzuri akiambiwa kitu cha kijinga akakiamini hata yule anayemwambia ujinga ule humdharau. Unapoamua kumdanganya mtu lazima kwanza umpime unayemwambia kama atagundua kuwa ukisemacho ni cha uongo. Ukijiridhisha kuwa hana uwezo wa kuugundua uongo ule basi unaendelea na hadithi yako ya uongo. Lakini upo pia uwezekano wa kukosea kumtathimini mtu, ukadhani mtu huyu ni mjinga (under rate) kumbe huyu mtu sio mjinga kama unavyodhani. Ikitokea hivyo basi wewe ndiyo unayekuwa mpumbavu kwa kushindwa kuelewa weledi wa mtu.

Binafsi nadhani Polisi wanadhani watanzania wote ni wajinga wanaweza kutengenezwa uongo wowote na wakaukubali. Upo ushahidi mwingi unaonyesha raia wakibambikiwa kesi mbalimbali zikiwemo za mauaji ili kukidhi mahitaji yao tofauti tofauti.Hapa uadilifu wa Polisi unatia shaka kama ni kweli kila mara wanasema ukweli. Ingalikuwa uadilifu wa polisi tu ungalikuwa ndiyo unaotiliwa shaka, ingalikuwa nafuu, lakini uadilifu wa viongozi wa juu pia unatiliwa shaka.

Kiongozi wa polisi anapofanya jambo tofauti na uadilifu unavyomtaka afanye kitaaluma ya polisi, je kiongozi wake anachukua hatua gani? Polisi anapomkamata kiongozi wa chama cha upinzani ili kukidhi mahitaji ya kisiasa ya kiongozi wa chama tawala, kiongozi husika yupo tayari kumwambia polisi kuwa jambo alifanyalo sio sahihi kimaadili. Polisi anaweza kuwa anajua kuwa sio sahihi lakini anafanya tu ili kumfurahisha bwana mkubwa kwa lugha rahisi anajipendekeza. Jukumu la kiongozi mwadilifu anapaswa kumkemea polisi huyu.

Utamaduni huu umezoeleka Tanzania kiasi kuwa wafanyakazi hawaangalii tena maadili ya kazi wanaangalia matakwa ya kiongozi. Kiongozi mkuu akitaka wananchi wabambikiwe kesi watafanya hivyo, akitaka wateswe, wapigwe na kutupwa mstituni watafanya hivyo. Baadaye watabuni na kuandaa wenyewe hata bila kutumwa na mtu maana upepo ndivyo unavyovuma. Hapa ndipo tulipofika.
Hatimaye serikali haitaaminika tena hata kama kuna ukweli. Inasadikika kuwa serikali ina mkono mrefu.Maana yake Serikali haishindwi na kitu.

Ikishindwa ni kwamba haitaki au la uhalifu huu unainufaisha serikali. Serikali inaposhindwa kuwakamata akina Kamhanda RPC Iringa kwa mauaji ya Mwangosi, inaposhindwa kuwatia nguvuni waliokuwa wakimfuatilaia Dr. Mwakyembe toka Tunduru hadi Dodoma licha kupewa taarifa, inaposhindwa kuwakamata waliomtesa Dr. Ulimboka licha kuwataja na namba zao za simu kujulikana na matukio mengine mengi, Watanzaia hatuna lingine zaidi ya kuamini kuwa serikali inahusika.

Inapokuja kumkamata Lwakatare kwa tuhuma ya video watu wenye akili wataamini mambo mawili. Kwanza kwa kuwa utamaduni wa kubambikia kesi wananchi ili kukidhi matakwa fulani Lwakatare pia atakuwa amebambikiwa kesi hii kwa kuwa yupo chama cha upinzani. Ni kesi ya kisiasa. Pili Serikali inataka kuwaacha wahusika iliowatuma ili kupoteza lengo ili wananchi waache kufuatilia wahusika wasijewakabainika na Serikali ikaumbuka.

Wananchi, kwa muda mrefu,wameonyesha kupoteza imani na serikali kiasi cha kuituhumu kuwa inahusika na matukio haya mabaya. Ikiwa serikali pia inatuhumiwa,inawezekanaje ikajichunguza yeyewe, Who can be a judge on his own case? Huo ni usanii.
Upo utetesi kuwa maadam Serikali imewekwa madarakani na wananchi basi hapana shaka kuwa wananchi wana imani nayo. Lakini nyuma ya pazia kuna malalamiko kuwa Serikali iliiba kura kwa kutumia Polisi na TISS hawa hawa wasioaminika.

Upo ukweli kuwa Serikali zinazoingia madarakani kwa hila haziishiwi na migogoro na serikali potofu huishi kwa upotofu ikudhani kuwa wanachi wataiheshimu kwa vitisho. Kwa kwaida wananchi huendelea kudai haki yao hadi serikali dhalimu inapoangushwa. Hakuna mahali popote duniani ambapo serikali imepata kudumu kwenye madaraka kwa ubabe

i cant wait to see this,ts better that way they must come clean,ni chama tunacho kitegemea sasa kwa uchafu uliojitokeza ni lazima viongozi wanuie kutusafisha mind zetu kwa uchafu uliyojitokeza and tujuwe if it was framed or whatever,na rai yangu ni kwamb kwa mleta thread hii unapaswa kutu-updates atleast,hope protocol itazingatiwa
 
Watanzania lazima tuwe wakweli na wawazi tusiwe watumwa wa siasa kwani siasa ni mchezo mchafu

Hii video ukiiangalia na kuisikiliza vizuri,huyu jamaa ni kweli anapanga mikakati ya kuhujumu mtu,wala hi video sio fake,huyu jama1 amekiri kwenye video kuwa amepewa "assigment",sasa cha kujiuliza hii mipango aliyokuwa akipanga ni ya kutoka kwenye chama chake au ni yake mwenyewe binafsi

Nakubaliana na wewe kwamba ni kweli video inasema amepewa "assignment" nakubali pia intuition yako kwamba inaweza kua mipango yake binafsi na sio ya chama ama ikawa ni ya chama- kitu ambacho kama itathibitika kua hivyo nitakilaani kwa uwezo wangu wote, kwakua hakiendani na iliyo mikakati ya CHADEMA katika kupigania haki., lakini nadhani kabla hatuja fika huko bado iko haja ya kujiridhisha si tu kwamba video hii ni authentic au ya kweli haija undwa lakini pia kama yaliyokua yakizungumzwa kwenye video hiyo hata kama video hiyo ni halisi yalikua yakielekezwa katika utekaji wa Ng. Kibanda? kwakua kama nilivyo sema video hii bado iko vague sana., kwanza iko robo, halafu haitoi hasa mantic ya kurecodiwa kwake hata content yake haija kamilika., haitaji utekwaji wa kibanda wala jina lolote., labda niseme tu kazi hii tuiachie polisi, ambao wame kua trained kukabili mambo kama haya na kutafuta ukweli ulipo jificha, kama wataifanya kazi hiyo pasipo kuingiliwa na nguvu nyingine yoyote,.. inawezekana Lwakatare akwa na hatia., lakini ni mapema mno kuamua hivyo!
 
Any prudent man anajua hii siyo case.
CCM iko kwenye critical condition mpaka inatumia mafia tactics kutimiza matakwa ya kisiasa.
Ukweli utajulikana na uongo utabaki uchi.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Huyu mzee vp,mara hana imani na polisi mara anataka polisi wafanye uchunguzi. Kwanini asisema kama hiyo video ni ya kweli au sio? Akae akijua jua kuwa hii video itaondoka na wengi.kama CCM ilikua inatafuta sababu ya kuwamaliza cdm basi hii sababu ni tosha kabisa

Nakuomba utambue ya kuwa kazi ya kichwa sio kufuga nywele tu,lazma uktumie kufkiri sana na kama uktaka kujua utmamu wa watz hawa ni kwenye hili la video ya kutengeneza,hata ukimchukua mtoto wa darasa la tano mwenye akili timamu hawezi kukubari kamwe ila utashangaa wenye digrii wanasapoti igizo hilo mithiri ya tamthiria ya kichina.
 
Kuwa mkweli watawala siasa zimewashinda

Nakubaliana na wewe Mkuu ,na ndio maana mimi sio muumini wa chama chochote kile cha siasa,kwani nimegundua zamani sana kuwa wanasiasa wetu wa Tanzania hawako kwa ajili ya uma bali wako kwaajili ya matumbo yao
 
Janja ya nyani hii mnafikiri mtatusahaulisha upuuzi wenu.ngoja niorodheshe hapa kwa herufi kubwa,MATOKEO FORM IV,UMEME,MAJI,UFISADI BOT,MALIASILI,BANDARI,MANISPAA,KILIMO,MADINI,MWANGOSI,UAMSHO,PONDA,MAUAJI MWANZA,UDINI,HAYA YOOTE NI MKIA WENU MACCM HAUWAACHI NG'O!
 
Tunaweza kuwabeza wapelelezi wa polisi lakini tukumbuke kwamba hawa ni 'trained criminal investigators'. Wanajua kuhoji na wanaweza kumhoji Lwakatare chochote kuhusu yeye na CHADEMA kwa ujumla na wanaweza kuzitumia au kuzigawa hizo taarifa wanavyotaka.Tusisahau unapozungumzia Kurugenzi ya Ulinzi na Usalama ya CHADEMA unazungumzia nini.. unazungumzia kitovu cha mikakati yao ya sasa na mbeleni ambayo ni ya tashwishi kwa watawala.Ukiweza kuisambaratisha Kurugenzi hii kwa kuonyesha kuwa yenyewe au watendaji wake si watu wema 'then' unamaliza kazi ...
CHADEMA kwa sasa kama inanuia 'kupona' kuliko wakati mwingine wowote inapaswa kuona hatari iliyo mbeleni na kuanza kujipanga katika 'kubetua' mitego ya ki-propaganda inayoelekezwa kwake.Kitu cha muhimu ni CHADEMA kutambua kuwa 'this is for real' na kudhibiti vitendo vya makada wake ambavyo vinaweza kufanya Dola iweze kuwafikia na kuwatoa 'nje ya mstari' wa mapambano.
 
Ni kama umekubari akili yako ichezewe eti? Mimi si MwanaChadema na sipo ktk chama chochote kile cha siasa. I only care about my work and what I earn after working. Hata hivyo, you do not need a forensic scientist to tell you kuwa ile ni FAKE by any definition. Umeona wapi mtu anaandaa uharifu na anapenda awe recorded? Awe recorded kwa faida ya nani? Nani am-record? Ili taarifa zimfikie nani? Hivi, unajua hata wewe wapo wanaoweza wakapata sura yako ukiwa katika mambo yako na waka-mute sauti yako na kukulisha maneno makali huku ukionekana unatechezesha midono yako ili ionekane ni wewe unayetamka hayo yanayozungumzwa?

Ukiona timing ya tukio, utabaini kuwa ni kuchezea akili za watu. Wasiwasi wangu ni kuwa kwa mtazamo kama huo wa kwako, inawezekana mpaka leo unaamini yule Mkenya wa watu maskini wa Mungu ndiye kweli aliyemteka Dk Ulimboka hata baada ya ukweli kujulikana. Timing ya tukio hili la Kibanda halitoi nafasi kwa Chadema kuwa ndio waliolipanga kwani ni siku chache tu tangu Kibanda awahame na kwa maana hiyo, ni rahisi kwa yeyote kuhisi kuwa ni Chadema. Sidhani kama Chadema wangekuwa na uwezo mdogo kiasi hicho. Nasema kuwahama Chadema kwasababu kama Mhariri Mtendaji wa gazeti lenye links na viongozi wa Chadema, ni dhahiri kuwa Kibanda alipata kufahamu mambo mengi ya Chadema kiundani na sidhani kama Chadema wangemfanyia unyama mapema namna hii. Kama Chadema wangekuwa na nia hiyo, wangesubiri angalau miaka miwili ili watu wasahau kwanza kuwa Kibanda huyu kipindi fulani alikuwa connected na Chadema. Hii ni fix ili tufikiri kama unavyoifikiri wewe.

i cant wait to see this,ts better that way they must come clean,ni chama tunacho kitegemea sasa kwa uchafu uliojitokeza ni lazima viongozi wanuie kutusafisha mind zetu kwa uchafu uliyojitokeza and tujuwe if it was framed or whatever,na rai yangu ni kwamb kwa mleta thread hii unapaswa kutu-updates atleast,hope protocol itazingatiwa
 
Mi naamini video ni ya kweli, tatizo ni kwa nini wanasema ni ya mauaji? Ukiisikiliza vizuri kwa kutulia hakuna mahali iliposemwa kaue waandishi au kawateke wanahabari, mahali pekee pabaya ni pale lwakatare anaposema awekewe dawa ya usingizi halafu aachwe baadae akishtuka atajua yupo hatarini na hivyo ataacha kutuhujumu (chadema) na ataendelea na kazi zake za uandishi.

mi naamini kwa video hii ni vigumu kumbana lwakatare kwa sababu kwanza anasikika akisema huyu asidhuliwe kwa namna yoyote, anasema haina haja ya kumdhuru kwa sababu sio lengo letu
kuhusu igunga na morogoro hakuna mahala amesema au kutaja kuhusika kwake katika matukio hayo.
Anyway, tusubiri
 
Back
Top Bottom