Dk Slaa: Tuhuma za Lwakatare kuteka waandishi zimepikwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dk Slaa: Tuhuma za Lwakatare kuteka waandishi zimepikwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mkusa, Mar 14, 2013.

 1. Mkusa

  Mkusa JF-Expert Member

  #1
  Mar 14, 2013
  Joined: Dec 14, 2010
  Messages: 538
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa amezungumzia video aliyorekodiwa Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama hicho, Wilfred Lwakatare na kusema ni ya kutungwa na vyombo vya dola.

  Dk. Slaa pia amelituhumu Jeshi la Polisi kufanya mchezo mchafu kwa maslahi ya kisiasa.

  Alikuwa akizungumza na waandishi wa habari Makao makuu ya chama hicho kufafanua suala la kushikiliwa kwa Lwakatare.

  Dk. Slaa, alilalamikia jeshi la polisi kuwa limekuwa likitumika kisiasa huku akitoa mfano wa chama hicho kuwa kimekuwa kikitaarifu jeshi la polisi kuhusu mambo hayo lakini halijawahi kuchukua hatua.

  Alisema jeshi la polisi halijawahi kuchukua hatua stahiki kwa suala la mauaji ya Daudi Mwangosi kumwajibisha Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Iringa aliyesimamia na kufanikisha kifo cha mwandishi huyo wa habari, jeshi la polisi pia halikuchukua hatua za kumhoji Dk. Stephe Ulimboka baada ya kuteswa na mtu anayedaiwa kuwa ni Afisa wa usalama wa Taifa wa Ikulu, hali kadhalika hawezi kushangaa ikiwa jeshi la polisi halitaacha kumhoji Absalom Kibanda.

  Amesema, jeshi la polisi limekuwa likitoa taarifa za kukichafua chama, akikumbushia suala la Mwangosi, alisema kuwa mara tu baada ya tukio la Mwangosi kuuawa, jeshi la Polisi kupitia kwa Kamishna wake lilitoa taarifa kuwa alilipuliwa na kitu kilichorushwa kwake akikimbilia kujisalimisha kwa polisi akitoka kwa wafuasi wa Chadema, jambo ambalo lilikuwa sio kweli.

  Hivyo alisema, Mkurugenzi wa ulinzi na usalama wa Chama hicho kuhusishwa kwa sakata la sasa la mkanda wa video uliopo katika mtandao na Kibanda ni mwendelezo tu wa kukihujumu chama, unaoratibiwa na Usalama wa Taifa, huku ukitekelezwa na jeshi la polisi.  Source: Dk. Slaa: Video ya Lwakatare ni feki! | Fikra Pevu | Kisima cha busara!

  My Take:

  Dr Slaa, Binafsi nina Imani Kubwa sana na CHADEMA, na hakuna kitu ambacho kitatoa Imani yangu kwa CHADEMA.

  Nina uhakika wa Asilimia Nyingi hii issue ina Connection na Kauli za CCM thru Mwigulu Nchemba na Mzee wa Gombe
  Hata kama hii issue itakuwa ni kweli, mimi bado nitakuwa CHADEMA Damu kabisaaaa.

  Ila Ombi langu, ninaomba sana tena sana,kwa hii issue, tunaomba Bw Lwakatare atakapotoka Kizuizini, atoe Tamko la Kukanusha hili Jambo, ama kwa Lugha nyingine.
  Aseme chochote kuhusiana na hili suala

  ====== VIDEO=======

   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 2. Character X

  Character X JF-Expert Member

  #2
  Mar 14, 2013
  Joined: Nov 22, 2012
  Messages: 332
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  NINA IMANI NA CHADEMA., NINA IMANI NA founding motives ZA CHADEMA NINA IMANI NA LWAKATARE., ziko sababu za kimsingi za kumuhoji Ng. Lwakatare kuhusiana na video hii,. lakini sio kuhusiana na tukio la kuteswa kwa Bw. Kibanda, wataalamu wa Forensic Sciences watakuambia kwamba traces za involved parties kwenye scene yoyote ya namna ile lazima huonekana katika eneo latukio na ndizo huongoza kuelekea kwa suspect (mshukiwa) lakini sio kutoka kwokote halafu kuhusisha na tukio flani tu eti kwasababu linaonekana kuelekeana.

  Video inayo ongelewa haionyeshi beyond reasonable doubt kwamba kinacho ongelewa pale ni KUTEKWA NA KUTESWA KWA MUANDISHI WA HABARI.,

  ndugu zangu tusikubali kuchezewa vichwa na watu flani wanaotumia hongo na pesa chafu kuchafua nia ya dhati yakuleta mabadiliko nchini.
  yako mambo mengi sana yakujiuliza kabla hauja amua kuchukua video hii kama UKWELI USIOPINGIKA.

  1. kwanini Bw. Lwakatare akubali kuwa recorded kama anafahamu anapanga uhalifu?(kwasababu kwenye video inaonekana anafahamu kwamba anakua recorded)

  2. Aliye record Video hii ana uhusiano gani na Bw. Lwakatare? je, ndiye aliye kua anatumwa kutekeleza uhalifu huo? (as it is supposedly assumed to be), na je? kuna prints zozote zinazo onyesha connection kati yake na zilizo patikana eneo la tukio, je? ni mwana chadema mwenzake aliye amua kumsaliti? hapa the question WHY (kwanini) must be given sufficient and eloquent answers. kama ndiyo kwanini amsaliti kiongozi wake? je? amelipwa na mtu? kama ndio ni nani? na kwanini? ilikufikia malengo gani? lakini ilikupata majibu kamili au ilikujiridhisah kwamba majibu yanayopatikana hapa ni sahihi:

  3. aliye iweka you tube apatikane., (kwa sababu anaweza kupatikana) aeleze mazingira ya kuipata, ilikuwa peleka hadi kumpata aliye tengeneza video hiyo atakaye eleza madhumuni ya kui record. na kwanini alichagua kuweka huko badala ya kuifikisha mahali husika. kama alilipwa kufanya hivyo aeleze alilipwa nanani. aeleze pia video hiyo kihalisia ilikua inazungumzia nini hasa (maana bado iko vague tu haiwezi kumfunga mtu, yanaweza kua nimaelezo akipiga stori na baada ya kutegwa nakuulizwa aelezee matukio ya namna iyo hua yanapangwaje., kumbe mtu katumwa anakurecord afu unauzwa hivi hivi na watu walafi wa madaraka

  NDUGU ZANGU "Critical thinkers" hapa we need to be really critical, siondoi kabisa uwezekano kwamba Nd. Lwakatare anaweza kuhusishwa kwa namna moja au nyingine na tukio lile kwa kupatikana kwa video hiyo, lakini lazima niseme wazi kwamba nina imani na CHADEMA, nina imani na Bw. Lwakatare na motives za CHADEMA pamoja na strategies zake kuelekea kuchukua 2015 Na hii SIYO MOIJA YA STRATEGIES za chadema!

  mwisho;
  haya ni mawazo yangu ambayo siyo lazima ya influence mawazo ya mtu mwingine yeyote..
   
 3. bushman

  bushman JF-Expert Member

  #3
  Mar 14, 2013
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,333
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Kwani hatujui tunalijua hilo ndio maana ccm walijua wenyewe wameingia msituni wameua swala kumbe wameibuka na bonge la nyani.walijua video hii ingewapa mlango wa kuchomokea!!!!!!!!!!
   
 4. sulphadoxine

  sulphadoxine JF-Expert Member

  #4
  Mar 14, 2013
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,264
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  WAKATI Jeshi la Polisi nchini ikiendelea kumshikiria Mkurugenzi wa Usalama na Ulinzi wa Chadema Willifred Lwakatale kwa mahojiano zaidi kwa siku ya pili, Katibu Mkuu wa chama hicho Dk Willibroad Slaa amesema tuhuma hizo ni za kupikwa. Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam,Dk Slaa alisema kwamba tuhuma zinazomkabili Lwakatale ni za uongo na zimepikwa, hivyo wanaitaka jeshila la polisi kuendelea na uchunguzi wa suala hilo na wakikamilisha kazi yao wampeleke Mahakamani.

  "Hizo tuhuma ni za uzushi, hazina ukweli hata kidogo, zimepikwa hivyo tunaiomba Jeshi la Polisi kuendelea na kazi yao na mwisho wamfikishe Mahakamani kwa sababu huko ndipo tutakapo pata ukweli juu ya suala hilo"alisema Dk Slaa.

  Mkurugenzi huyo alikamatwa na Polisi jana kwa tuhuma za kuhusika katika njama za kumteka na kumtesa Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF) na Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya New Habari Absalom Kibanda.

  Mbali na tuhuma za kumteka Kibanda,pia anahojiwa kwa tuhuma ya kushiki njama mbalimbali za mauaji pamoja na mateso ya Mussa Tesha aliyemwagiwa tindikali Igunga na lile la morogoro ambapo kijana mmoja alifariki katika vurugu za maandamano ya chadema, ambapo polisi walitoa taarifa kuwa kijana huyo ameangukiwa na kitu kizito. Pamoaja na kuandaa njama za kumteka Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Mwananchi Denis Msacky ambazo bado hazijatekelezwa.
   
 5. toxic9

  toxic9 JF-Expert Member

  #5
  Mar 14, 2013
  Joined: Nov 6, 2012
  Messages: 6,116
  Likes Received: 8,939
  Trophy Points: 280
  i cant wait to see this,ts better that way they must come clean,ni chama tunacho kitegemea sasa kwa uchafu uliojitokeza ni lazima viongozi wanuie kutusafisha mind zetu kwa uchafu uliyojitokeza and tujuwe if it was framed or whatever,na rai yangu ni kwamb kwa mleta thread hii unapaswa kutu-updates atleast,hope protocol itazingatiwa
   
 6. mchambuzixx

  mchambuzixx JF-Expert Member

  #6
  Mar 14, 2013
  Joined: Nov 11, 2011
  Messages: 1,294
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 145
  yaani wewe ndugu yangu ile video tu inaonekana ni ya kutengeneza bado unatka chama kikjisafishe ukitaka kujua undani wa tukio lakuteka waandishi wasikilize kina bashe polisi ni wajinga na wanatumika kama kondom ...wewe hebu angalia hilo tukio mtu badala ya kupeleka polisi anapeleka JF hapa wa kukamatwa ni mwigulu huyu ndo suspect number one na anajua mpango mzima wa KIBANDA tokea aseme anayo video hajaitoa anakuja kuitoa baada ya tukio ..kama ww great thinker unaelewa ninachomaanisha
   
 7. mary mary

  mary mary JF-Expert Member

  #7
  Mar 14, 2013
  Joined: Dec 21, 2012
  Messages: 871
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Katika yoooote maandamano ya kuisimamisha Nchi yako pale pale....CCM msitupotezee lengo letu. Mapambano yanaendelea
   
 8. Shinto

  Shinto JF-Expert Member

  #8
  Mar 14, 2013
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 1,781
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Hakuna haja ya kuumiza kichwa humu, ukweli anajua Rwakatare!
  1. Ile video ni ya kughushi au ya kweli
  2. Katumwa na CDM au la
  3. Anaihujumu CDM au anatii maelekezo
   
 9. F

  FUSO JF-Expert Member

  #9
  Mar 14, 2013
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 12,684
  Likes Received: 3,049
  Trophy Points: 280
  hii kitu waipeleke haraka mahakamani, ili mbivu na mbichi ijulikane, yaani chama cha upinzani kianze kuwauwa waandishi wa habari? kwa lipi hasa walilofanya?

  Chama kinachotaka kuingia madarakani, chama kinachotaka kuwakomboa wananchi kianze kuua waandishi wa habari? aisee hii kitu ukifikiria kwa makini utaona kuna magepu mengi sana kwenye hili dili -- loop holes kibao.

  Msihofu: Ngoma ikifika mahakamani kuna softwares zinaweza kabisa kungamua kwamba hiyo video ni ya ukweli au mtu kachomeka maneno. hapa ndipo watu wataumbuka unless mahakama ikatae ushahidi kwa namna hiyo utumike.
   
 10. THE BIG SHOW

  THE BIG SHOW JF-Expert Member

  #10
  Mar 14, 2013
  Joined: Feb 28, 2012
  Messages: 13,946
  Likes Received: 1,910
  Trophy Points: 280
  Character X,

  mawazo yako hayapingwi,
  ila yamepotoka sana,na yamejawa na mihemko ya kiitikadi ya chama zaid,na kukosa uzalendo wa kitanzania,
  1.haijalishi kama lwakatare alikua anajua kama anarekodiwa ama la,hilo ni juu yake yeye,sisi tunapima uzito wa kile anachokizungumza na mazingira halisi tunayopitia katika nchi yetu kwa sasa,
  either alifanya vile intetionally or otherwise,lkn katika kile alichokisema ana stahiki kuhojiwa na tuyapime majibu yake
  2.kila mtu ana iman na chadema hapa?
  We vp?kwani chadema ni mtu mmoja mmoja au taasisi ya watu fulani?
  Iweje mtu akifanya makosa eti tuache kuhoji kisa tunakua tunakichallange chama?hiyo haingii akilin kbs,
  3.tuache mihemko isiyo na misingi
  lwakatare amewapa kazi ngum sana chadema unless awe na maelezo ya kutosha ya kushibisha njaa zetu za akili..
   
 11. Remote

  Remote JF-Expert Member

  #11
  Mar 14, 2013
  Joined: May 20, 2011
  Messages: 15,260
  Likes Received: 1,950
  Trophy Points: 280
  Mambo ya mwigu.lu
   
 12. F

  FUSO JF-Expert Member

  #12
  Mar 14, 2013
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 12,684
  Likes Received: 3,049
  Trophy Points: 280
  mliambiwa CDM itakufa before 2013, na mwingine akasema ana video ya viongozi wa CDM wakipanga mauaji -- so join the dots then unapata kitu.
   
 13. Tetty

  Tetty JF-Expert Member

  #13
  Mar 14, 2013
  Joined: Jan 6, 2012
  Messages: 26,400
  Likes Received: 17,579
  Trophy Points: 280
  Lakini polisi wnagemtafuta na aliyeiweka kwenye mtandao ili atuelezee watanzania nani alimpa na ina maana gani.Vinginvyo hatutamtendea haki Lwakatare.Hebu tuione kwa upande wa pili huyu mtu hajaongea hayo yaliyowekwa kwenye hiyo clip na mpaka saa hizi anashikiliwa na polisi ni sahihi?

  Na clip yenyewe inaonyeshwa imetengenezwa ili kuharibu utu wa watu wengine.Watanzania tumuogope mungu kwenye matendo yetu hasa yale ya siasa chafu za kuharibia utashi wa watu wengine.
   
 14. W

  WESTON MAHINYA Member

  #14
  Mar 14, 2013
  Joined: Mar 14, 2013
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jeshi la polisi wasipelekeshwe na wana siasa da siasa bana
   
 15. Mau Mau

  Mau Mau JF-Expert Member

  #15
  Mar 14, 2013
  Joined: Dec 30, 2012
  Messages: 602
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 60
  NINA IMANI NA CDM
  wanapambana sana kuichafua chadema lakini siku zote MUNGU ni mkubwa na hashindwi, ninaamini huu ndo mwisho wao, hili litawaanika wao
   
 16. m

  majebere JF-Expert Member

  #16
  Mar 14, 2013
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 591
  Trophy Points: 280
  Huyu mzee vp,mara hana imani na polisi mara anataka polisi wafanye uchunguzi. Kwanini asisema kama hiyo video ni ya kweli au sio? Akae akijua jua kuwa hii video itaondoka na wengi.kama CCM ilikua inatafuta sababu ya kuwamaliza cdm basi hii sababu ni tosha kabisa
   
 17. Mystery

  Mystery JF Gold Member

  #17
  Mar 14, 2013
  Joined: Mar 8, 2012
  Messages: 8,695
  Likes Received: 8,419
  Trophy Points: 280
  Hawa Polisi ni watu wa ajabu sana, kinachoonekana hapa ni kutaka kutwist mambo. Kila mtu anajua kuwa tukio la kutekwa na kuteswa kwa Dr Ulimboka, kuna mfanano wa hali ya juu, na hili tukio la Kibanda. Nitataja mambo machache yanayofanana, wote wawili waling'olewa meno na kucha na hao watekaji, na wote wawili waliteswa katika kiwango cha hali ya juu sana na watu waliowatesa wanaonekana dhahiri wamepitia mafunzo ya kijeshi, kitu kinachoonyesha, upo uwezekano mkubwa kuwa watekaji wa Dr Ulimboka, ndio hao hao waliomfanyia unyama Kibanda!!

  Sasa, kama Dr Ulimboka aliwaeleza kuwa yupo tayari kuwasaidia Polisi, ili watu waliomteka wakamatwe, ni kwa nini wao Polisi, hilo wanaligomea, na wanaendelea kumng'ang'ania chizi wa Kenya, ambapo Dr Ulimboka amewahi kutamka wazi kuwa huyo siyo miongoni wa waliomteka?!

  Katika tukio la Kibanda, tumemsikia Kibanda mwenyewe akisema,alimsikia mmojawao wa waliomfanyia unyama huo,akimuuliza mwenzake, vipi afande, tumshuti?! Huo bado haujawa ushahidi kuwa majeshi yetu yalihusika?!

  Sasa, kwa ushahidi huo, ambapo Dr. Ulimboka alitamka wazi kuwa mtu wa mwisho kukutana naye siku anatekwa alikuwa Ramadhan Ighondu wa Ikulu-TISS, ni kwa nini Polisi hadi leo wanashikwa na kigugumizi cha kumkamata huyo Ramadhan Ighondu, hadi limetokea tukio la kuumizwa kwa Kibanda,ambalo lina mfanano wa kiasi kama cha asilimia 98?

  Upo ushahidi wa wazi kwa sasa kuwa Jeshi la Polisi na vyombo vingine vya ulinzi na usalama, havipo tena kutekeleza wajibu wake namba moja, ambao ni kuwalinda raia na mali zao, badala yake wamegeuza kuwa jukumu lao la kwanza kwa sasa, ni kutekeleza matakwa ya watawala, na mbaya zaidi,hata kama watawala hao wataviagiza vyombo hivyo vya ulinzi na usalama, viyaondoe maisha ya baadhi ya raia wema, vyombo hivyo vya ulinzi na usalama wanatekeleza amri hizo haramu bila kusita!!
   
 18. makavulaivu

  makavulaivu JF-Expert Member

  #18
  Mar 14, 2013
  Joined: Dec 29, 2012
  Messages: 402
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  CCM WANAZO KILA SABABU ZA KUFANYA UMAFIA WOWOTE KWAGHARAMA ZOZOTE NA KWA TECHNOLOJIA YEYOTE KWASABABU IMANI YA WANANCHI DHIDI YA CCM ILISHAPOTEA NA IMEZIDI KUDIDIMIA NA KUONGEZA HOFU YA KUPOTEZA DOLA KWENYE UCHAGUZI UJAO.najiuliza pia polisi nao walitumia YOU TUBE ku establish kosa au mwigulu aliwapelekea hiyo video? Natarajia Mwigulu nae aunganishwe polisi kwa mahojianao
   
 19. Mimibaba

  Mimibaba JF-Expert Member

  #19
  Mar 14, 2013
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 4,566
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Anayeweza kusema ukweli wa video ni CCM kwa maslahi ya CCM. Ila kama sheria ilivyo ikiwa si ya kweli kuna watakaoilipia ghali zaidi ya mil 80 zilizoitengenezea
   
 20. W

  WESTON MAHINYA Member

  #20
  Mar 14, 2013
  Joined: Mar 14, 2013
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kaka da kweli imani yako safi
   
Loading...